Mjadala wa mila na desturi za kiafrika uwekwe mezani

Malima Chacha

Member
Oct 11, 2020
9
17
Afrika na Tanzania kiujumla tumekuwa na mvutano na mitazamo tofauti hasa pale inapotokea mjadala wa kusimamia MAADILI, Kumekuwa na makundi mawili makubwa yanayoibuka pale ambapo rungu la kuadhibiwa kwa uvunjifu wa ZINAZOITWA MILA NA DESTURI ZA KIAFRIKA linapowakuta washukiwa

Kundi la Kwanza,Kuna wanao jadili kwa mtazamo wa kiafrika na kidini zaidi

Pili, Kuna wanaojadili kwa mtazamo wa kimarekani & Dunia ya Sasa kiujumla kwa kuzingatia mabadiliko yake sayansi na teknolojia

Hizi pande mbili ni imekuwa ngumu kukutana kila moja inaona iko sahihi kwa mtazamo wake!

Jambo likifanyika MAREKANI huonekana ni sahihi, ndio maana Gigy alipovaa kinyago chenye maumbile ya MWANAMKE pale jamhuri stadium Dodoma kwenye show ya WASAFI FESTIVALS, BASATA walipomfungia watetezi wake waliibuka kusema "Ooh tunaua Sanaa mbona Lady Gaga pale U.S anavaa hakuna shida"

Mbunge wa Momba Condester katolewa bungeni sababu ya mavazi yasiyo na maadili, baadhi ya watu mashuhuri, wabunge ambao hawakuhudhuria kikao & baadhi ya watu. Makundi haya yamekuwa yakisambaza picha inayoonesha suruali yake kuonesha kwamba kaonewa wakati makundi yote hayakumuona liive na pia kutambua kuwa ipo tofauti Kati ya kati ya uhalisia na picha, makundi yote yanasahau kanuni za bunge zinaelekeza Nini!!!

Marcus Garvey aliwahi kusema "Watu wasiokuwa na utamaduni wao ni sawa na mti usiokuwa na mizizi" Kwa Sasa Afrika tunaelekea kuwa WAZUNGU WANAOISHI AFRIKA

Kwa Sasa, Tunapaswa kuwa na mjadala wa kuamua na kujadili Kama MILA na DESTURI za kiafrika bado zina maana au zimepitwa na Wakati

Bila Hivyo tutaendelea kurumbana kila uchao! La sivyo Taasisi husika zisimamie kanuni na taratibu bila hiyana wala kupepesa macho..!

Malima Chacha
 
Back
Top Bottom