Mjadala mkubwa ni kuhusu mchanga wa dhahabu,vipi kuhusu gesi?

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,453
Sometime nahisi kuwa Mtanzania ni Kama unakuwa na laana hivi!. Sijui tulimkosea nini Mungu. Sasa hivi ktk Social media zote mjadala mkubwa ni kuhusu mchanga ulio ktk makontena. Ripoti ya tume imetuambia kwamba tumeibiwa tena sana. Tunaamini kuwa tumeibiwa kila mahali ktk haya masuala ya uwekezaji. Swali la kujiuliza. Je. Hao viongozi waliotuingiza ktk wizi huu, wako hai au walishafariki?

Sasa hivi tunazungumzia juu ya mchanga wa dhahabu. Vipi kuhusu Gesi yetu ambayo wakati wa kampeni tulikuwa tukiahidiwa kuwa itatufanya Watanzania kuwa ktk uchumi wa Kati mpaka itakapofika 2020. Sasa hivi hata ktk huu mtandao wetu, ukiuliza tu juu ya ile ahadi, basi hata huo Uzi wako utafutwaa au kuhamishiwa ktk Jukwaa ambalo halina Wasomaji wengi.

Sasa basi ifike mwisho tuseme imetosha. Nakumbuka kuwa huu mkataba wa Gesi ulipelekwa bungeni ktk style ile ile ya hati ya dharura. Sijui walikuwa wanakimbilia wapi. Na Waziri Yule aliyekuja na hati ya dharura Leo tena yupo madarakani. Bado Watanzani tuliolaaniwa tunamwamini. Tukumbuke kuwa hii mikataba ya madini ambayo mpaka sasa inamtesa Raisi sheria zake zilitungwa bungeni kwa hati za Dharura,

Anyway hili la dhahabu ni kubwa lakini ni la Muda mrefu sana. Machungu yake yalishaisha. Swali ni Je. Ile gesi ya kutupeleka ktk uchumi wa Kati 2020 iko wapi?.
 
IMG_20170529_152239_049.jpg
 
Mm hawa jamaa nachokaga mpaka basi
Ni hatari sana Mkuu, sasa hivi ukizungumzia tu habari ya gesi unaonekana Kama mwendawazimu. Kama kweli tumeamua kusafisha, basi upelekwe mswada wa dharura bungeni wa kuwaondolea kinga ya kushtakiwa kwa hao Miungu watu waliolitia hasara Taifa hili bila kumbagua mtu. Other ways tunajidanganya. It's too much!
 
Ni hatari sana Mkuu, sasa hivi ukizungumzia tu habari ya gesi unaonekana Kama mwendawazimu. Kama kweli tumeamua kusafisha, basi upelekwe mswada wa dharura bungeni wa kuwaondolea kinga ya kushtakiwa kwa hao Miungu watu waliolitia hasara Taifa hili bila kumbagua mtu. Other ways tunajidanganya. It's too much!
Ufaransa kwenye karne 17 waliitoa serikali madarakani (swept away) kutokana kulewa na madaraka, matumizi mabaya ya mali za uma
 
WRSDDQ3FXDXQSXQX4AADSXFW2C21DXW22FF2AFFARW21AVR3AA3SA23WXDEWWZC2XDFEASR1DEDRDCSRFDFFFRds :-SS @):- @):- i
 
Kwenye mikataba kuna uwezekano mkubwa vikawepo vipengele vya kutunyonya kama mikataba mingine iliyosainiwa kuhusu maliasili zetu.

Lakini ni vyema watu wakafahamu kuwa gas ya mtwara ambayo viongozi tulionao sasa waliitumia katika kuombea kura kama ambavyo mtoa mada umesema, si sawa na hio tuitumiayo kinyerezi kutoka bomba la mtwara-dar. Gas hio inatoka onshore(pwani ya bahari ya mnazi bay). Kwa kiasi kikubwa bomba hili lilijengwa maalum kwa ajili ya mitambo ya kuzalisha umeme ya kinyerezi hivyo hakuna uhusiano na hio reserve kubwa ambayo imegundulika offshore(ndani ya bahari).

Kuna changamoto kubwa sana ili tuweze kufaidika na gas ya mtwara(endapo terms za mikataba zinaruhusu hilo). Zinahitajika specialized facilities za kuitoa chini ya miamba ya bahari baada ya hapo itapitishwa kwenye mabomba hadi nchi kavu ambapo itapokelewa na kuingizwa kwenye plant nyingine(LNG plant) itakayochakata(compress) hadi iwe katika hali ya kimiminika. Hivyo zitakuwa plant mbili onshore na offshore plants. Baada ya hapo itasafirishwa hadi mashariki ya mbali China na India kwenye soko kubwa na kiasi kidogo kitauzwa nchini.

Gharama za uwekezaji ni $15 billions (zaidi ya TRILLIONS 30 za kitanzania). Ni uwekezaji ambao hauhitaji kukurupuka na unaweza chukua hata zaidi ya miaka 5 kabla ya kuanza uzalishaji. Mwaka uliopita waliamua plant ya uchakataji ijengwe Lindi na eneo limeshapatikana ila kuna fidia lazima zilipwe kwanza.

Kwa kuhitimisha, liqudified natural gas(LNG) plant ya mtwara ni mradi uliokatika proposal bado haujaanzwa jengwa.

Ingia link hizi zitakupa ufahamu zaidi
Mtwara/Lindi|$15 billion|Onshore LNG complex|Proposed - SkyscraperCity
Mtwara gas plant project to take 7 yrs
Tanzania Liquefied Natural Gas Project - Wikipedia
19,000 acres available for LNG plant in Lindi
http://allafrica.com/stories/201411290431.html
LNG Facility in Tanzania - Oil4All
http://www.wentworthresources.com/pdf/agm/2007_05_Annual_General_Meeting.pdf
Mtwara gas plant project to take 7 yrs | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today
https://www.google.com/amp/s/www.fa.../tanzania-africa-news-lng-industry-33035/amp/
 
Back
Top Bottom