Mjadala - Kitabu cha unyama wa Paul Kagame: Behind the Presidential Curtain: Inside Out of real Paul Kagame

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Jana nilitoa link ya ku download hiki kitabu, kwa ambao hawaja download ingia JF Store, wandugu naomba msome vizuri hicho kitabu baadaye turudi kwenye mjadala hapa maana niliyoyasoma yanasikitisha.



Kumbe ndiyo maaana Museveni kamchoka,wanajuana nje ndani, na Kagame hizo tabia zake ni za hatari siye yule tunayemuona sisi, SO SAD.

Kitabu kina pages 110(hard copy)ila kwenye pc hapa inaniambia ni pages 302 ,kwenye page ya 71 tunaona kitu fulani kuhusu tabia ya Kagame(familiar )

--
--It was President Kagame himself who briefed his senior intelligence commanders to use the tactic of being friendly to those they were planning to kill, at some point they gave out sugar and salt, cooking oil and soap to the locals that our soldiers had looted from shops just to make them come out of the hiding only to be killed in the end.----

Ni kwamba mwaka 1992 katika mazungumzo ya amani Arusha,Rais Juvenal Habryimana alisema wakimbizi wa Rwanda walioko nje kurudi ni ngumu sababu hakuna ardhi ya kutosha kwa hiyo akawasambaza wahutu mipakani huko na kuwapa ardhi ili ionekane kweli pamejaa na pia sababu nyingine ilikuwa ni kuwapeleleza RPF waliokuwa wanavamia kutokea Uganda

So,trick ya Kagame ikawa ni kwenda kwenye vile vijiji na wanajeshi wake kujifanya marafiki zao wakiwapa sukari,chumvi,nguo,siku moja katika kijiji cha Kagitumba wakaitisha mkutano mkubwa wahutu wakajaa wake,waume kwa watoto,katikati ya mkutano askari wa RPF wakarusha risasi na mabomu ya kutosha wakaua maelfu ya wahutu.

Niko page ya 72 ila dah hadi hapo nilipofika jamaa aliua marafiki zake waliomsaidia kupindua nchi karibu 10 tena wenye vyeo vya juu jeshini akiwemo FRED RWIGEMA swahiba mkuu wa Museveni kiasi cha kusababisha mdogo wake Museveni meja Salim Salehe kwenda kuua mameja wawili wasio na hatia waliosingiziwa na Kagame kwa Musevni kwamba walimuua Rwigema

Jamaa alikuwa anawaogopa makamanda wa ukweli waliomtoa dikteta Habrayimana , walikuwa hawamkubali sababu hakupigana vita muda mwingi alikuwa masomoni Marekani alipopelekwa na Museveni.

Mwandishi anasema jamaa ana tabia ya kujifanya rafiki yako huku akikutafutia muda sahihi wa kufanya yake(does that sound familiar?
 
Katika page ya 73 mwandishi Noble Marara ambaye ni bodyguard wake wa zamani anazungumzia roho ngumu ya jamaa akiwa na wasiwasi mkubwa wa mambo mabaya aliyowafanyia wahutu hapo Rwanda na Congo.

Kagame ali fake shambulio in 1998 kuua raia waliokuwa wakiangalia mpira hotelini ili awasingizie Interahamwe lakini aliyepewa jukumu la kusimamia hilo(captain Kwizera) alilewa chakari, matokeo yake askari wa RPF waliojifanya Interahamwe walifika hotelini hapo wakashangaa kuona kuna wanajeshi wa RPF nao wanaangalia mpira wakapiga simu kwa wakubwa yakatolewa maelekezo wale askari waondoke hapo haraka.

Raia wajanja walivyoona zile movement wakshtuka nao wakasepa, waliobaki ndani baadaye walikufa maana ile hoteli iliungua ikabaki majivu. Baadaye radio Rwanda ilitangaza ya kwamba shambulio lilifanywa na Interahamwe

 
Mwandishi wa kitabu anasimulia jambo jingine kuhusu tabia ya Kagame ya kuamini kuua, anaogopa mabaya aliyoyafanya kwa watu siku ya mwisho yatamgeukia. Haishangazi kusikia wengine walifuatwa hadi South Africa kuuliwa, wengine are still on the run haswa jijini Kampala walipojificha.

 
Ukurasa huohuo(73) mwandishi Marara anasema ingawa kuna watu walikufa kwenye hilo shambulizi hotelini wakiwa wanaangalia kombe la dunia, Kagame alikasirika sana sbabu halikwenda kama alivyo-plan sababu ya uzembe wa captain Kwizera liyekuwa amelewa hivyo akagiza fimbo za kutosha na alitoa Presidential Jeep yake kwenda kuchukua hizo fimbo, akwaagiza luteni Nkubito na Aimee Claude kumcharaza Kwizera fimbo 100, akashuhswa cheo na kuswekwa ndani baadaye akafukuzwa jeshini

 
Katika ukurasa wa 79, bwana Marara anatuambia kuhusu kifo cha Asiel Kabiera, mshauri mkuu wa Rais Kagame ambaye kabla ya hapo alikuwa mshauri mkuu wa Rais Bizimungu kipindi hicho Kagame akiwa Waziri Mkuu.

Kabera anasifiwa na wengi Rwanda kwa kuwa na roho ya kibinadamu na alikuwa hapendi mambo mengi yanayofanywa na Kagame, ukiachilia mbali hilo pia alikuwa rafiki wa karibu wa spika wa Bunge Mr Kabuye ambaye baadaye alikimbia nchi kwa hofu ya kuuawa, spika huyo alikuwa anachukiwa sana na Kagame.

Mwandishi katika ukurasa huo anasimulia kwamba siku moja alikuwa anatakiwa kumpeleka mke wa Kagame kumtembelea mama yake, akiwa kwenye gari alisikia mlio wa risasi ukitokea karibu na Presidential Palace, akapiga radio call kuuliza wenzake kuna shida gani, kuna mwenzao akamuambia usijali kila kitu kipo sawa wewe endelea na safari yako na first lady. Baadye akaja kumuambia kwamba Mr. Kabera alikuwa ni msaliti so they sorted him out

 
Katika ukurasa wa 83, mwandishi anelezea jinsi Kanali Charles Ngoga alivyouliwa na Luten Dan Gapfiz kijana aliyetumika kwenye mauaji mengi lakini na yeye mwisho wake aliuliwa kwenye ajali fake maana alikuwa anajua siri nyingi sana za mkuu
Kisa cha kanali Ngoga ndicho cha kushangaza zaidi,aliuliwa simply SABABU ALIKUWA ANAGOMBANIA SOKO LA KUUZA MAZIWA YEYE NA KAGAME, maziwa ya Kanali Ngoga yalikuwa yanauza sana,mkuu akakasirika na kabla ya hapo magari y a kanali Ngoga ya kubeba maziwa yalishakuwa ambushed mara 6 na maziwa kumwagwa baadaye ikaonekana solution ni kumuuua.

Ukisoma hiki kitabu vizuri, mwandishi anadai hata majengo mengi marefu Kigali ni ya Kagame, inasemekana ni fisadi mkuu ila mjanja sana wa Public Relation haswa kimataifa, kajitengenezea image ya UMUNGU MTU, hata mwandishi anakiri yeye pia alifanya mabaya akijua ana serve nchi.

Yaani, hata wauaji wa Kagame wanaua kwa furaha wakiamini wanaua wasaliti wa nchi yao na hakuna mtu Kama kagame, kwao ni kama Mungu mtu na wafuasi wake wanaamini hilo

 
Jamaa ni katili sana ,nakumbuka kwny kitabu,kagame alikuwa anaendesha gari bahati mbaya akatapika ,sasa marara alikuwa nae ikabidi kagame asimamishe gari,akajifanya anaenda short call,huku marara anasafisha seat ,ile kurudi kagame akakuta jamaa anamalizia kupolish seat,kagame alimpiga kiwiko cha jicho full kuvimba kisa anamchelewesha,yaan jamaa hana shukrani ,nahisi huyu jamaa ana mental disorder syo kwa kuua huko
 
Maisha yenyewe yapo kasi sana Sina muda wa kusoma history za homosapiens wenzangu.mimi labda nitaongeza knowledge ya afya,nature,n.k ..nimechoka Sana vitu ambavyo havina uhakika
Mwenzako kafanya tafiti tena kutoka kwa mwandishi wa kitabu aliyeshuhudia.

Sasa unaposema 'vitu havina uhakika' inabidi utumie akili yako zaidi ufanye utafiti ili upate uhakika.


NOTE: Akili ikichoka muda wako wa kuishi siyo rafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…