Mizinga ya Bar maids

Mizinga ya Bar maids

severinembena

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2018
Posts
2,435
Reaction score
2,402
Niende moja kwa moja kwenye mada,
Kuna tabia ya bar maids karibia wote kuomba uwanunulie kinywaji hasa pale anapoona umekunywa pengine bia tatu na kuendelea.

Mara nyingi unapoagiza labda bia ya tatu au ya nne unakuta anakwambia "kaka/uncle vipi Mimi sinywi hata moja?" Au "kaka Mimi hata soda tu" au "Chenji si na Mimi ninywe soda?"

Hii adha nimekuwa nikikutana nayo Mara nyingi sana. Mwanzoni nilikuwa naona fresh tu baadae nimeona kumbe ni tabia yao karibia wote.
Kwa kifupi imekuwa kama ni haki yao kupewa kinywaji au uwaachie chenji na usipowapa basi siku nyingine ukienda hawakuchangamkii kukuletea huduma, sasa unajiuliza yeye yupo pale kwa kazi gani kama anachukia mteja asiyempa ofa au anayedai chenji?
Mfano Jana nilikuwa sehemu Fulani nimeagiza kinywaji nikakuta wahudumu wanamjadili mteja mmoja aliyefika. Mmoja ya wahudumu hao nilimsikia akisema " Akhaaa nenda kamhudumie wewe mi nasubiri wengine, mteja bahiri kama nini"!. Walinikera na nikawaeleza waziwazi kwamba kwa kufanya hivyo hawajui wajibu wao.

Kuna muda huwa nawapa tu na muda mwingine unakuta nina kahela ka bia mbili au tatu tu nimeamua nikapoze koo kidogo ila wao huwa hawatambui hilo. Naamini adha hii inakuta wenzangu wengi tu ila huwa hawasemi

NB: nimesema hili siyo kwa sababu mi mchoyo Bali hawa wauzaji kwenye Bar,Groceries au Pubs wanapaswa kutambua kuwa si haki yao kununuliwa vinywaji au kuachiwa chenji na Mara nyingine mteja anaenda kuwaunga mkono huku akiwa hayuko vizuri. Ili kukomesha hili wanywaji wenzangu muwe mnawaelimisha Hawa wahudumu hasa pale unapokutana na adha za namna hii.
Mwisho kuwasilisha,samahani kwa wale nilowakera kwa hili.
 
naielewa sana nyimbo yake ya MAMA YEYOO nadhani ndo nyimbo naweza isikiliza mara mbilimbili
 
Sasa mtu anakuhudumia ana njaa mshahara wenyewe elfu sabin, muwe na huruma na wenyewe watoe stress,
Kama huna hela kanunue bia Mangi shop kanywee chumbani kwako hawa wa bar waache wana wenyewe nawe siku ukizipata utawakuta!
 
Kwani hizo bar zinawatu maalumu Wa kunywa humo?
 
Aisee jiongeze. Hapo haombi bia Bali anaomba umnunue iyo kuomba bia ningia tu ya kukifanya ujiongeze. Wewe unafikiri wanamuomba kila mtu? Wanawaomba nyie wenye uelekeo wa kuwanunua
 
Hapo ndiyo mwanzo wa kusepa na mhudumu wa bar.
Huwa sichelewi mimi, ndiyo maana napenda nihudumiwe na mzuri
Niende moja kwa moja kwenye mada,
Kuna tabia ya bar maids karibia wote kuomba uwanunulie kinywaji hasa pale anapoona umekunywa pengine bia tatu na kuendelea.

Mara nyingi unapoagiza labda bia ya tatu au ya nne unakuta anakwambia "kaka/uncle vipi Mimi sinywi hata moja?" Au "kaka Mimi hata soda tu" au "Chenji si na Mimi ninywe soda?"

Hii adha nimekuwa nikikutana nayo Mara nyingi sana. Mwanzoni nilikuwa naona fresh tu baadae nimeona kumbe ni tabia yao karibia wote.
Kwa kifupi imekuwa kama ni haki yao kupewa kinywaji au uwaachie chenji na usipowapa basi siku nyingine ukienda hawakuchangamkii kukuletea huduma, sasa unajiuliza yeye yupo pale kwa kazi gani kama anachukia mteja asiyempa ofa au anayedai chenji?
Mfano Jana nilikuwa sehemu Fulani nimeagiza kinywaji nikakuta wahudumu wanamjadili mteja mmoja aliyefika. Mmoja ya wahudumu hao nilimsikia akisema " Akhaaa nenda kamhudumie wewe mi nasubiri wengine, mteja bahiri kama nini"!. Walinikera na nikawaeleza waziwazi kwamba kwa kufanya hivyo hawajui wajibu wao.

Kuna muda huwa nawapa tu na muda mwingine unakuta nina kahela ka bia mbili au tatu tu nimeamua nikapoze koo kidogo ila wao huwa hawatambui hilo. Naamini adha hii inakuta wenzangu wengi tu ila huwa hawasemi

NB: nimesema hili siyo kwa sababu mi mchoyo Bali hawa wauzaji kwenye Bar,Groceries au Pubs wanapaswa kutambua kuwa si haki yao kununuliwa vinywaji au kuachiwa chenji na Mara nyingine mteja anaenda kuwaunga mkono huku akiwa hayuko vizuri. Ili kukomesha hili wanywaji wenzangu muwe mnawaelimisha Hawa wahudumu hasa pale unapokutana na adha za namna hii.
Mwisho kuwasilisha,samahani kwa wale nilowakera kwa hili.
 
Mie nawaheshimu sana wahudumu wa bar kumpa bia moja mbili tatu sio shida, mtu anakudumia kinywaji ama chakula vizuri tu ata kama ndo majukumu yake , hapana aisee tuwape tu kiroho safi.
 
Mimi nikiingia bar. Nikiagiza beer namuambia barmaid na wewe chukua kinywaji chako. Ya pili hivyo hivyo mpaka ya nne. Ya 5 naanza kupima oil bila upinzani wowote. Ya 6 namwambia akamuage matron.
Bar sehemu ya ushenzi. Sasa wewe hata beer moja ya 2500 waiona expensive? Ninyi ndio ambao ukiona mtu amekaa na barmaid unafikiri anamtongoza.
 
Hapo ndiyo mwanzo wa kusepa na mhudumu wa bar.
Huwa sichelewi mimi, ndiyo maana napenda nihudumiwe na mzuri
Ha ha ha kuna mdau mmoja alianzisha Uzi unasema Asilimia cjui ngapi nimesahau kidogo ya wahudumu Wa bar wana HIV+, na alisema amefanya utafiti
 
Enzi zangu nilipokuwa napiga monde, mhudumu atakayenihudumia lazima naye apate kinywaji au chips mishikaki... Nilikuwa naona huruma anapokuwa ananiangalia tuu
 
Mimi nikiingia bar. Nikiagiza beer namuambia barmaid na wewe chukua kinywaji chako. Ya pili hivyo hivyo mpaka ya nne. Ya 5 naanza kupima oil bila upinzani wowote. Ya 6 namwambia akamuage matron.
Bar sehemu ya ushenzi. Sasa wewe hata beer moja ya 2500 waiona expensive? Ninyi ndio ambao ukiona mtu amekaa na barmaid unafikiri anamtongoza.
Sawa mtu mwenye pesa zake nimekuelewa
 
Back
Top Bottom