Mshana Jr, je mizimu inaweza kudhuru MTU asiewakwao..mfano umeoaa mke mwenye mizimu je mwanao aweza kuwa na mizimu Kwa sababu ya mama yake? Na je inarithiwa??!
HOW?
katika ulimwengu wa rohoni mwanaume na mwanamke wanapo ingia katika agano rasmi la ndoa, nafsi zao huunganishwa na kuwa kitu kimoja. Hii inawahusu hata wale wanao fanya tendo la ndoa bila agano rasmi ( wazinzi & waasherati ). Unapo fanya tendo la ndoa na mwanamke unakuwa umekubaliana kuunganisha nafsi yako na nafsi yake. Nafsi yako na yake zinaungana na kukamatana na kuwa kitu kimoja. Kama mtu huyo alikuwa na nuksi/mikosi/laana basi laana hizo zitakufuata na wewe. Nature ya nafsi ya mwanadamu ni " Electro -Magnetic " . Nafsi hizi zinapoingiliana kupitia " majumba" ( miili) yao, hukamatana na kuwa kitu kimoja.
Unapoenda kufanya tendo la ndoa na mke wa mtu basi kuwa na uhakika unaenda kubeba nuksi, mikosi na laana zote za mume/mwanaume wa mwanamke huyo. Ndio maana wayahudi enzi za agano la kale, wazinzi walikuwa wanapigwa mawe hadi kufa, kwa sababu ilichukuliwa kwamba ubaya na uovu wa tendo la zinaa si tu ulikuwa unawanajisi wahusika bali pia ulikuwa una inajisi nchi yote. uzinzi ilikuwa ni kosa kubwa sana sawa sawa na uhaini katika nyakati za leo.
Unapo fanya tendo la ndoa na mwanamke, tafsiri yake katika ulimwengu wa rohoni ni kwamba, unakuwa umeridhia na kukubali kuingia katika agano la kuunganisha nafsi yako na nafsi ya mwanamke ambae unafanya nae tendo la hilo la zinaa.
Haijalishi unajua kwamba unaingia kwenye agano au haujui ( Hata katika ulimwengu wa rohoni, kanuni ya Ignorantia juris non excusat " ignorance of the law has no excuse" ina operate. )
Mfano wa agano au mkataba huu ni sawa na mkataba unao ingia kila siku unapo enda kupanda daladala., Unapo kuwa umepanda dala dala actually unakuwa umeingia katika contract kati yako wewe na konda hata kama hujui kwamba umeingia kwenye mkataba. Mwisho wa siku utatakiwa kulipa consideration " malipo ya mkataba" ambayo ni nauli yako.
Vivyo hivyo unapo fanya tendo la zinaa na mwanamke basi jua umeingia kwenye agano la kuunganisha nafsi yako na nafsi yake na mwisho wa siku utatakiwa kulipa gharama za agano hilo ambazo ni pamoja na nuksi, mikosi, mabalaa, laana za ukoo, laana za familia nakadhalika.
Mind you, madhara unayo weza kuyapata sio lazima yawe spiritual katika namna unayo weza kuielewa wewe. Yanaweza kuwa physical but spiritual. Kwa mfano ukifanya zinaa na mwanamke mwenye virusi vya ukimwi maana yake ni kwamba na wewe utapata ukimwi. So mateso yake ya maradhi ya ukimwi yatahamia kwako pia.
Hata kwenye Bible imeandikwa kwenye kitabu cha Mithali 6:32 " Mwanaume Mzinzi hana akili hata kidogo, kwa maana ana i angamiza nafsi yake mwenyewe". Ana iangamiza vipi ? Ana iangamiza kwa ku iunganisha na laana, nuksi, mikosi, maagano mabaya ya kisheitwani.