Miziki kama bongo fleva na bolingo iwe rated 18

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,843
Reaction score
10,765
Wakuu amani itokayo juu iwe nanyi. Amina. Nashauri miziki ya baongo fleva na bolingo iwe rated above 18 ili iwekwe mbali na watoto. Huwa nasikitika sana kula niwapo safarini kuona aina ya miziki inayoonyeshwa kwenye mabasi, yaani ni aibu kubwa uwapo na watoto. Halafu ni nani aliyeweka utaratibu kuwa kila abitia anayesafiri ni mpenzi wa miziki hiyo ya kishetani? Mtu anapokata tiketi hatarajii kuwa kuna mziki humo, ingekuwa hivyo treni isingalipata abiria. Huu ni unyanyasaji kwa kundi fulani la abiria.

Nyimbo zote ni mapenzi tu, scenes za hovyo, ujumbe wa kuzimu, hii haikubaliki kabisa. Najua wapo wadau wa hayo mambo lakini hapa naongea kama mzazi, sio kijana wa ghetto. Kuvumilia ujinga huu ni kuwathibitishia watoto kuwa tunakubaliana na kile kinachoimbwa.

Pia kuna baadhi ya sinema ni za hovyo kupindukia. Nakumbuka kuna siku nikiwa safarini nikaona tamrhilia inaitwa KIMBURU kama sijakosea, yaani mwanzo mwisho inaonyesha jinsi kijana wa mjini alivyokwensa kijijini akawa anawalala mabinti na wake za watu huko. Haina fundisho hata moja, zaidi ya kuwapotosha mabinti na vijana. Sasa kama mna safari ndefu mtaitazama tamthilia hiyo hata mara tatu. Tumekuwa taifa la ajabu sana, lisilo na maadili.
 
"in my maserati"
video ya hii nyimbo inaanza kistalabu, mwisho mwisho chupi zinaanza. 🤣

Inshort niliamua kutofatilia kabisa kinachoendelea kwenye TV ndani ya Basi.
Kibaya kama ni mtoto huwezi kumzuiq kuangalia.
 
"in my maserati"
video ya hii nyimbo inaanza kistalabu, mwisho mwisho chupi zinaanza. [emoji1787]

Inshort niliamua kutofatilia kabisa kinachoendelea kwenye TV ndani ya Basi.
Kibaya kama ni mtoto huwezi kumzuiq kuangalia.
Na ndio hapo lilipo tatizo, watoto tunawazuia vipi?
 
Wakuu amani itokayo juu iwe nanyi. Amina. Nashauri miziki ya baongo fleva na bolingo iwe rated above 18 ili iwekwe mbali na watoto. Huwa nasikitika sana kula niwapo safarini kuona aina ya miziki inayoonyeshwa kwenye mabasi, yaani ni aibu kubwa uwapo na watoto. Halafu ni nani aliyeweka utaratibu kuwa kila abitia anayesafiri ni mpenzi wa miziki hiyo ya kishetani? Mtu anapokata tiketi hatarajii kuwa kuna mziki humo, ingekuwa hivyo treni isingalipata abiria. Huu ni unyanyasaji kwa kundi fulani la abiria.

Nyimbo zote ni mapenzi tu, scenes za hovyo, ujumbe wa kuzimu, hii haikubaliki kabisa. Najua wapo wadau wa hayo mambo lakini hapa naongea kama mzazi, sio kijana wa ghetto. Kuvumilia ujinga huu ni kuwathibitishia watoto kuwa tunakubaliana na kile kinachoimbwa.

Pia kuna baadhi ya sinema ni za hovyo kupindukia. Nakumbuka kuna siku nikiwa safarini nikaona tamrhilia inaitwa KIMBURU kama sijakosea, yaani mwanzo mwisho inaonyesha jinsi kijana wa mjini alivyokwensa kijijini akawa anawalala mabinti na wake za watu huko. Haina fundisho hata moja, zaidi ya kuwapotosha mabinti na vijana. Sasa kama mna safari ndefu mtaitazama tamthilia hiyo hata mara tatu. Tumekuwa taifa la ajabu sana, lisilo na maadili.
Nakazia
 
Tatizo wanaofanya kazi kwenye hayo mabasi ndio wanapenda hiyo miziki na tabia zao ni za ovyo sana. Ni ngumu sana kuwashawishi waweke mziki wenye maadili mazuri huku wao wakiwa ndio waovu.
 
Mabasi yasicheze hiyo miziki wala filamu kabisa.
Nyakati zimebadilika.
Siku hizi tunaweza kujiburudisha wenyewe Kwa simu, vitabu na visimbusi vyetu.
Unakuta unataka kulala kidogo, mara wanacheza singeli.
 
Back
Top Bottom