Mizani ya njia panda ya Himo

Mizani ya njia panda ya Himo

ulimboka

Member
Joined
Aug 23, 2009
Posts
36
Reaction score
0
Si mara ya kwanza kukuta msongamano wa magari makubwa ya abiria na yale ya mizigo yakishindana jinsi ya kupima uzito pale njia panda ya himo hasa nyakati za jioni na wakati mwingine kutokea kuifunga barabara hiyo kabisa. Hatima yake ni kujikuta unatumia zaidi ya masaa mawili hata kama haupitii mizani ndipo upate kuendelea na safari yako. Hii imenikumba hasa inapofika nyakati za jioni. Je hakuna namna ya kuweka mizani katika eneo ambalo litapunguza kero hii? Kuna sababu yoyote ya kuweka kipimo hiki hasa kwenye makutano ya barabara? Vipi kile cha pale mikese njia ya kwenda morogoro je wahusika hawawezi kuchota utalaamu hapo ili kupunguza kero hii? Wanajamii nisaidieni kuweka ubongo sawa. Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom