Miundombinu ya Barabara Nchini inaharibiwa sana

Nicholas J Clinton

JF-Expert Member
Mar 13, 2014
877
486
Serikali imekuwa ikutumia fedha nyingi za walipa kodi wa Tanzania kujenga Barabara na madaraja lakini utunzaji wake ni wa mashaka sana na kuna uharibifu mkubwa sana kwenye Barabara na madaraja.

Barabara za mitaani hizi ambazo zimejengwa na mradi wa DMDP na za miradi mingine hazina muda mrefu tangu kukamilika kwake ila zimearibiwa kingo zake, taa zinangongwa, petrol zinamwagwa Barabarani na hakuna anayejali Unakuta Barabara baada ya miezi mitano tangu imekamilika imeisha chakaa kwa kuaribiwa! Lakini hizi Barabara za mradi wa DMDP nyingi zinaaribiwa pia na Malori makubwa ya mizigo mizito na hakuna anayejali na unakuta kuna Alama zinaonesha kabisa Barabara ina uwezo gani katika matumizi yake!

Madaraja vile vile yanagongwa kingo zake, juzi nimepita daraja la Tanzanite kingo zake zimegongwa kabisa na kuna Camera pale! Madaraja mengi na Barabara zetu hazitunzwi kabisa na kuifadhiwa vyema mara baada ya kukamilika kwake.

Sina hakika kama tuna sheria ya kulinda miundombinu yetu inayotumia mabilioni mengi kutekelezwa, kama sheria hii ipo basi haifanyi kazi kabisa na kama hatuna sheria ya kulinda miundombinu basi ni wakati wa kutunga sheria hii ili kulinda miundombinu yetu watu wanaoharibu kwa namna yoyote ile wawajibike, na nishauri Serikali miundombinu yote inayotelezwa hapa Nchini wekeni Camera na hasa Mijini ni muhimu sana. Mradi wa BRT, SGR, Miradi ya maji, Barabara na madaraja wekeni CCTV ili angalau kudhibiti madereva watukutu na wasiyo jali kuhusu miundombinu hii.

Mwisho, Naishauri Serikali yetu kwenye upande wa Barabara za Dar Es Salaam. Jiji hili lina kasi kubwa ya ukuaji, ujenzi wa barabara na miundombinu mingine ilenge miaka 50 mpaka 100 ijayo au vinginevyo, mfano Barabara zote zinazoingia na kutoka kama Bagamoyo, Kilwa, Morogoro, na Nyerere Roads Barabara hizi ni muhimu sana kuzijenga au kuzipanua kwa njia nne sioni kama tunakadhi matarajio ya ukuaji wa Dar Es Salaam.

Mfano, Morogoro Road tayari upanuzi wake unaendelea lakini naambiwa kutokea Kibaha kwenda Chalinze itakuwa njia nne! Hapa mimi naona hapana Kibaha chalinze iwe njia nane au sita vile vile angalau sasa kutoka hapo kuelekea Morogoro inaweza kuwa njia nne.

Barabara ya New Bagamoyo hivyo hivyo ina miaka michache sana tangu ujenzi wake ila imezidiwa tayari, Barabara hii pia ipanuliwe kwa njia sita au nane ili Jiji lipumue tuwe na Barabara pana na zinapitika haraka sana, Kilwa Road pia inazidiwa tuangalie angalau kuijenga kwa njia sita au nane pia mpaka Mkuranga.

Na Barabara ya mwisho ni ile Nyerere wengine wanaita Pugu kutokea Gongo la mboto kwenda Kisalawe na Chanika mpaka kutokea Mbagala rangi tatu, hizi Barabara ni muhimu zinapanuliwe zaidi na ziwe za kisasa zaidi hata kwa kujenga na private sector lakini tuwe na Jiji ambalo miundombinu yeke ina hadhi ya ukubwa wake, kwa sasa bado sana ukitoa Km 19 Kimara Kibaha.

Nyerere Road pia kuna mradi wa BRT unapita Barabara hii ni muhimu iangaliwe vizuri kwa sababu ni moja ya Barabara zinazouza Jiji letu Kimataifa, mradi wa BRT unaopita design yake iwe tofauti na nyingine ili kuleta mandhari nzuri ya barabara hii.

Mradi wa BRT utaiweka Dar Es Salaam mahali pazuri zaidi kama mradi huu utakuwa bora na kuwaishwa na hapa Serikali niipongeze kwa mradi huu. Tuamue, tukiamua inawezekana Tanzania ni tajiri.
 
Hakuna Cha Nini Wala Nini barabara zinazojengwa Ni kwa ajili za kuombea kura tu , za kuzugia wananchi tu

Pili Ni upigaji wa viongozi ,
hapa waandisi wawahusiki kwa sababu wanajenga kutokana na maelezo ya viongozi wezi wa ccm

Mwisho hata izo mbovu wanazojenga roho zinawauma kweli, ila ilitakiwa inunue wapiga kura wajinga
 
Back
Top Bottom