iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Mimi ni mmoja kati ya watumiaji wa mabasi ya mwendokasi,hakika ni hatua nzuri tumepiga na nadhani baadae miundombinu hiyo itaboreshwa kwa kuweka reli na treni za kisasa za mjini zitakuwa zinasafirisha wananchi.
Jambo nililoliona ni kwamba abiria hujazana ndani ya mabasi hayo kwa wingi asubuhi na jioni,kitu pekee kinachokaguliwa ni tiketi,basi! Ni kweli watanzania ni wapenda amani,lakini hata watu wabaya wapo,nilikuwa napendekeza ukaguzi wa kiusalama pia uongezwe vituoni ili wenye nia mbaya wakose njia
Hii inaweza kufanywa pia katika miundombinu ya DART na miundombinu mingine mbali na ya DART kama
-kuondoa watu jirani na mitambo ya umeme Ubungo na nchi nzima,hata kama ni kwa fidia na kuweka security zones
-Madaraja kama Wami,Ruvu,Mkapa,Daraja la Mwalimu Nyerere,Simiyu,Kagera na mengine mengi makubwa na ya kimkakati,yasiachwe yakakaa bila uangalizi
-Mabomba ya kusafirisha gesi pamoja na Tazama, yawe kwenye mkakati wa kiusalama,ni sehemu ya raslimali za taifa ambazo zikipata madhara,taifa litaathirika
-Matenki ya mafuta pia yawekewe usalama zaidi,mafuta ni muhimu kwa taifa na pia yana milipuko,
-Njia za reli na maungio yake
-Mabwawa ya maji ya kuzalisha umeme
-Vituo vikubwa kama kariakoo, Stendi ya Mabasi Ubungo
-Bandari zetu zote popote pale ziwekewe ukanda wa kiusalama ambao viboti uchwara havitasogea wala kusogelea meli
-Majengo marefu
Binafsi nadhani hayo ni maeneo nyeti na yanafaa kuwekewa jicho la karibu sana na vyombo vya dola. Ni sehemu kuu zinazoingizia nchi mapato kila mtanzania mwenye nia njema azilinde