Miundo mbinu ya baiskeli na watembeao (pedestrian) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miundo mbinu ya baiskeli na watembeao (pedestrian)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'azagala, Jun 19, 2011.

 1. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Swali: Kwanini pamoja na umasikini wa waTanzania, miundo mbinu ya baiskeli na watembea kwa miguu haipewi kipaumbele?

  “Naomba wabunge wetu mtusaidie kuuliza maswali haya huko bungeni na wahusika wachukue hatua”


  Kwa wale waliotembea nchi mbalimbali za wenzetu hasa Ulaya watakubaliana na mimi kuwa kuna nchi ambazo zipo juu sana kimaendeleo na zimeimalisha miundombinu ya reli, barabara za magari, usafili wa maji (bahari na mito), barabara za kupita kwa baiskeli na vijia vya watembea kwa miguu.


  Zaidi ya nusu ya wananchi katika nchi hizo wanatumia baiskeli na kutembea kwa miguu katika mizunguko mijini na pia kuna taa za kuwaongoza. Wananufaika ifuatavyo;


  · Suala la kupunguza gharama (serving)
  · Suala la kupunguza uchafu wa mazingira
  · Kuweka miili katika hali ya kiafya - mazoezi

  Tanzania tunaishi katika umasikini ambao kwa kiasi kikubwa unachangiwa pia na kutumia gharama kubwa katika kusafiri (hasa Dar). Tegemeo kubwa katika mizunguko ya dar ni magari binafsi au madaladala. Kuna wachache wanaoweza kutembea na kutumia baiskeli lakini miundombinu kwa ajiri hiyo ni hafifu au haipo kabisa katika maeneo mengi. Kuna baadhi ya barabara ambapo kuna service road ila hazijawa rasmi kwa matumizi ya baiskeli na watembeao kwa miguu bali matumizi mbalimbali kama
  · - magari kupita humo,

  · -malori kupaki, au kufanya gereji

  · -bar au biashara nyingine nk


  100_0022.JPG
  kutoka kulia ni njia ya wapita kwa miguu, baiskeli, magari (katikati)
  baiskeli.jpg

  miundombinu.jpg

  ningependekeza kuwepo kipaumbele katika kuweka miundombinu hiyo katika miji yetu yote. Pia sehemu ambazo tayari ipo mf. Nyerere Road/Mandela nk basi ichorwe vizuri ijulikane na usimamizi uwepo ili isitumike vingine.
   
 2. Mwasi

  Mwasi JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 249
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kweli kabisa Mkuu naunga mkono hoja, hata mimi huwa najiuliza hii kitu sipati jibu .
   
 3. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  kutokana na hali yetu ya kiuchumi tulipaswa kuimalisha miundombinu hii ili kusaidia kupunguza gharama inayotokana na matumizi ya magari
   
Loading...