Mitungi ya gesi yalipuka Kigamboni

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Milipuko iliyosikika leo alfajiri ni mitungi ya gesi ambayo imelipuka na kujeruhi baadhi ya walinzi na wapita njia. kutokana na mueleko wa upepo inasemakana maeneo yatakayoathirika zaidi endapo isipothibitiwa ni Mbagala.

Kama kuna wanaofaatilia habari hii kwa undani tunaomba michango yenu, je ni uzembe kama ule wa mabomu au ni ajali ya kawaida??
 
Naona ma-ambulence na magari ya zima moto yanakimbilia huko mbona tangu imetokea ni lisaa na nusu sasa???
 
Last edited:
Habari za usubuhi kwa wale watu wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na wengine ambao kwao ni asubuhi kama kwetu.

Huku kwetu hali si shwari kwa kuwa asubuhi ya leo mida ya saa 7:10 hivi imesikika milipuko ya nguvu pande za Kigamboni, inasemekana kuna mitungi ya gesi imelipuka.

Mwenye habari zaidi atumwagie.

By the way am new in the jamiiforums so i hope to get a lot of company to you guys.
 
Duhh jamani mwenye news zaidi...
Vp hali ya majeruhi Nguli?

Kuna baadhi ya walinzi wameungua vibaya wamekimbizwa hospitali, na wapita njia wachache lakini sia ajabu ukasikia vyombo vya habari vikisema hakuna madhara yaliyojitokeza......
 
Walioshuhudia tukio wanasema ni hitilafu ya Umeme,wanaouza walikuwa bado hawajafungua.Ni vema vitu kama hivyo vikawa mbali na makazi ya watu.
 
Nimeamkua Kigamboni leo na mimeshuhudia iiile kadhia ya milipuko soma ishu kamili hapa

Mitungi iliyolipuka ilikuwa imehifadhiwa ktk duka la kuuzia gesi kwa matumizi ya nyumbani.
Mhusika aliyekuwa anajukumu la kufungua duka alifanya hivyo mnamo alfajiri saa moja na ushee hivi. Jamaa alikuwa anafungua duka huku sigara ikiwa mdomoni na alipofungua alikumbana na kasheshe la mlipuko baada ya gesi iliyokuwa inavuja kukutana na moto wa sigara. Kwa hiyo mhusika au muuzaji kwa jina jingine, aliumizwa sana na kishindo cha mlipuko na moto iliomuwakia sawia. Eneo la tukio ni hatua chache baada ya gati la pantoni kuelekea mjimwema. opposite na filling station ambapo mtungi mmoja uliolipuka ulitua jirani na kituo hicho pia. Fremu zilizopo jirani na duka hilo la gesi zimeungua chapachapa. Mpaka sasa ninapoandika waraka huu tanesco wanaendelea kutengeneza sehemu ya nyaya zilizoungua ili kurejesha umeme.

Kituko cha tanesco ni kwamba, sehemu ya juu ya nguzo ambayo ipo jirani na duka la gesi imeungua ambapo ni nyeusi kama mkaa ila walumendago wanaendelea kurejesha nyaya zilizoungua ambapo nilidhani wangebadili nguzo kabisa ili kuzuia madhara ya mbeleni....
 
Back
Top Bottom