Mitihani ya Suprementary

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,522
Reaction score
14,005
Heshima nyingi na za dhati kwa wanajukwaa wote!

Nina kijana wangu anasoma Mzumbe Chuo kikuu (Anasomea Sheria)
Naomba kujua hii mitihani ya Supplementary je inalipiwa pesa na kama inalipiwa ni kiasi gani?

Naomba kujua maana hawa vijana wa siku hizi mizinga mingi bila kujali hali ya mdororo wa uchumi kwa watanzania wengi.

Asanteni.
 
Mitihani ya suplimentary hailipiwi,au hata maana ya suplimentary haujui
 
Yawezekana lakini ninachojua kuwa uki-appeal ndio unalipia mkuu
 
Hiyo inategemea chuo unachosoma kuna ambao chuo kinahitaji kulipia hiyo mitihani ya marudio na kuna baadhi ya vyuo hawahitaji malipo kwa ajili ya hiyo mitihani, lakini huyo kijana wako hadi anapata supp alikuwa mgonjwa au ndio ukilaza wenyewe mkulu aliyosema?
 
labda kama mkiacha kushinda kwenye mikeka mnacheza bao kutwa nzima,,maendeleo uletwa na wananchi nyie wenyewe,,serikali inajazia tu
 
hahaha WE mdingi uko vizuri hawa dotcom hawa wanweza kukutembeza na viraka wakati wao wakishindana kutoka kimapenzi. Vyuo vingine havilipii hii mitihani sina hakika na mzumbe
 
kuna baadhi ya vyuo wanalipia nadhani. kama pale mwalimu nyerere walikua wanalipia.ila vyuo vingi hailipiwi
 
kwa sababu bwanamdogo ni mwanafunzi na anahitaji pesa (uskute dogo kapigika na hana chanzo cha mapato kingine) nadiriki kusema supp zinalipiwa na dogo atakua na supp nyingi kwahiyo mtumie mtonyo wa maana.
 
Hailipiwi asee dogo anataka kukupiga pesa
 
Mitihani ya suplimentary hailipiwi,au hata maana ya suplimentary haujui
Kuuliza sio Ujinga,najua hailipiwi wakati nasoma ilijuwa bure,mamabo hubadilika ndio maana nimeuliza mwenye current info.
[HASHTAG]#Jifunze[/HASHTAG] kujibu swali bila kuuliza swali!
 
kupata sup ni kawaida tu.ni somo kama masomo mengine .wewe bdo utafika tu chuo.komaa sana
 
Ni Supplementary
 
Umeeleweka mkuu
 
kwa sababu bwanamdogo ni mwanafunzi na anahitaji pesa (uskute dogo kapigika na hana chanzo cha mapato kingine) nadiriki kusema supp zinalipiwa na dogo atakua na supp nyingi kwahiyo mtumie mtonyo wa maana.
Hahahaaa naona umeamua umsaidie ili apate mtonyo wa kueleweka kutoka kwa mshua. Upo vizur mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…