Mitihani ya Maswali ya Kuchagua

hmtk

Senior Member
May 24, 2013
157
56
Kwa muda mrefu wadau wa elimu wamekuwa na malalamiko mengi kuhusu uendeshaji wa elimu yetu hasa ya msingi na sekondari. Baadhi ya mambo ambayo wadau/wananchi waliowengi hawakuridhishwa nayo ni:
1. Matumizi ya mfumo wa GPA badala ya Division katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu elimu ya sekondari.
2. Maswali ya kuchagua katika mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi.
3. Kushusha kwa alama za ufaulu kwa watahiniwa wa kidato cha 2, 4 na 6.
4. Wakati fulani serikali ilifuta masomo ya michepuo kama ya kilimo, biashara na ufundi, na michezo ikapigwa marufuku mashuleni.

Kutokana na malalamiko ya wadau/wananchi waziri wa elimu Prof. Ndalichako amerudisha mfumo wa division na ni uamuzi uliopokelewa vizuri na wananchi wengi. Pia, masomo ya mchepuo wa biashara yamerudishwa sina hakika kuhusu michepuo ya ufundi na kilimo. Na michezo naona siku hizi Umitashumta na Umiseta inafanyika kila mwaka.

Hoja yangu ni ukimya wa wadau kuhusu mitihani ya kuchagua kwa watahiniwa wa elimu ya msingi (darasa la 7). Utaratibu huu kwa ujumla wake unatoa matokeo yenye utata maana hata asiyejua kusoma anachaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.Huu ukimya ni kuwa tumeridhika au tunahisi kuwa hatutasikilizwa? Naamini viongozi weu ni wasikilivu, ni vema tukatoa msimamo/dukuduku letu katika mfumo huu wa mtihani wa kuchagua kwa wahitimu wa elimu ya msingi.
 
Huo mtihani wa kuchagua ni moja ya jipu katika Elimu. Tunapokea wanafunzi waliokuwa wanashika mkia, tunaanza kuwafundisha kuandika.
Lugha ya Kiingereza inakuwa adhabu kwao. Yaani serikali iyopita iliona ni namna bora ya kupunguza gharama ili hali watu wanajichotea mabilioni kwenye sekta nyingingine.
Cheap is expensive.
 
Back
Top Bottom