Mitihani,majaribu na changamoto kwa CCM

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Ccm inakabiliwa na mitihani,changamoto na majaribu mengi sana. Kuondokana na haya sio kazi rahisi kama wengi wa wanaccm wanavyofikiria.
Changamoto na majaribu haya,they have something called trade off yaani utatuzi wa changamoto au jaribu moja kunaweza kuzua changomoto nyingine au matatizo mengine makubwa zaidi. Nitafafanua changamoto hizo kama ifuatavyo
1. Nguvu ya Lowasa ndani ya CCM.
Inaonekana kuwa EL ana nguvu kubwa sana ndani ya chama hasa kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya chama na wenyeviti wa mikoa. Nguvu hii ya EL haiendi sambamba na safari yake ya matumaini,japo hajaweka wazi nia yake ya kugombea urais wa JMT. Kwa kuwa nguvu hii ya LOwassa haiungwi mkono na makada wengi wa ccm,inaweza kusambaratisha chama.
Ccm wana option mbili.
Mosi,kumtosa Lowasa. Hapa pana changamoto moja kubwa,ccm wakiamua kumtosa Lowasa watambue kuwa chama cha mapinduzi ndio mwisho wake kwa kuzingatia nguvu ya EL ndani ya chama.
Pili.kumpitisha EL kama mgombea wa urais. Katika hili pia kuna changamoto moja kuu,wale wote ambao wana mitazamo tofauti na EL kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka na wafuasi wao mfano SItta,Membe,Sumaye nk.
2. Nguvu ya upinzani(UKAWA).
Hakuna kipindi chochote ambacho upinzani umekuwa imara kama kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. Hakuna kipindi chochote ambacho chama cha mapinduzi kimekumbana na upinzani mkali katika uchaguzi wa serikali za mitaa kama mwaka 2014.
3. Kujisafisha
chama cha mapinduzi kinakabiliwa pia na changamoto ya kijisafisha kutokana na kashfa mbali mbali kama ESCROW,ujangili,madawa ya kulevya,rushwa nk. Hapa kuna chamgamoto moja kubwa,ccm haiwezi kujisafisha kwa sababu watuhumiwa wa ufisadi,wizi,ujangili ndio wenye nguvu chamani,ccm ikubali iwatose mafisadi,ikiwatosa ndio utakuwa mwisho wa ccm,au iwaache ili chama kiendelee kuporomoka.
Pia,uchakachuaji wa maoni ya katiba mpya ni pigo lingine kwa ccm. Wezi na mafisadi papa ambao ndio watuhumiwa wakuu wa ESCROW ndio walipewa jukumu la kuandika katiba pendekezwa,mtuhumiwa gani awezaye kujihukumu mwenyewe na adhabu ya kifo? Hakuna.
4. Mabadiliko.
Kwa kifupi,wananchi wamebadilika sana na mabadiliko haya sio ya kurudi nyuma bali ni ya kusonga mbele. Ccm haiwezi kuzuia mabadiliko. Hii ni changamoto kwa chama kinachotumia falsafa ya ujinga kama ccm.
5. Ugumu wa maisha.
Ccm inawakati mgumu wa kurudisha imani kwa watz baada ya kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtz kugonga mwamba na kufa kifo cha mende. Hii ni changamoto kwa chama cha mapinduzi.
6. Makundi ndani ya chama.
Ccm itakuwa na wakati mgumu kuamua nani asimame urais kwa sababu ya makundi yenye nguvu ndani ya chama. Kibaya zaidi makundi haya ni mahasimu. Kuna kundi la Lowassa,Membe,Sitta,Ngeleja,Mwandosya,Makamba Jr,Nchimbi,Kingwangala etc.
Hitimisho.
Ni vigumu kwa ccm kuvuka changamoto zote hiki. Chama hakipo salama. Chama lazima kijeruhiwe kwa namna yoyote ile,hakuna namna.
Time will tell.... Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom