Mguu wako usiingie kwa jirani yako ila kwa kiasi;
Asije akakukinai na kukuchukia.
Ukiyafikiri haya kwa kina, ikiwemo
1. Kuwapigia simu watu muda wa kazi kisha unasema nilikua nakusalimia tu.
2. Kuwatembelea watu mara kwa mara huku ukiwa hauna stori za maana unazokwenda nazo.
3. Kuvuruga ratiba za wenzio kwa sababu uwepo wako pahali walipo bila mwaliko rasmi yaweza kuwa nyumbani, baa n.k
4. Kulazimisha ukaribu na watu ambao dhahiri wanaonekana kutovutiwa nawe.
5. Kuazima chumvi, unga, mboga, hadi malapa ya kuogea (uswahilini)
Kamwe hautasutwa, wala kudharirika.