Mitaro ya maji katika eneo hilo imejaa taka na maji machafu yanayotoa harufu mbaya. Hali hii inatishia afya za wananchi, hususan wakazi wa eneo hilo.
Siku ya kwanza nilipoona tatizo hili, nilidhani labda wahusika wamejisahau kidogo na watalishughulikia. Hata hivyo, matumaini hayo yamepotea baada ya kushuhudia imepita wiki ya pili bila hatua yoyote kuchukuliwa.
Natoa wito kwa watendaji wenye jukumu la kusimamia usafi, hususan usafi wa mitaro katika eneo hilo, wawajibike ipasavyo badala ya kujifungia maofisini.