Mitandao ya simu kutuibia imekuwa ni kawaida

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Mitandao ya simu imechagua kutufilisi wateja na malalamiko yote tunayotoa.

Yaani wameona ni sawa kushusha viwango vya vifurushi ila kwa bei zile zile za zamani za vifurushi ili sisi tuumie mbwa hawa.

Unajiunga kifurushi 10GB ila zitakavyopukutika hautaamini. Wakati nakumbuka kipindi cha nyuma hapo nilikuwa naweka vifurushi natumia bila presha yoyote. 10GB za mwezi zilikuwa haziishi natumia hadi mwisho wa mwezi unakuta zimebakia GB 6 hadi 4 kwa matumizi ya kawaida ya kuperuzi instagram, Facebook, whatsapp na web pages za kawaida.

Kwa sasa mambo ni tofauti, wizi wa wazi wazi unafanyika......

Sijajua wenzangu kama mnapitia hii hali na kimsingi kuna watu wanapitia nipo nao karibu na nimewasikia wanalalamika....
 
Back
Top Bottom