Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,779
- 6,910
Hili suala limenitatiza kwa muda mrefu sana ila nimekuwa mvumilivu nikijua watu wa sales na marketing katika mitandao ya simu wakipevuka watabadilika. Leo uvumilivu umenishinda, nimeona niseme tu.
Katika biashara, kwenye mbinu za mauzo, ukiwa unaweka bei unajaribu kuhakikisha unamshawishi mnunuaji anunue bidhaa zako kwa wingi. Kwa maana hiyo, utaweka bei kiasi kwamba kila mtu anaponunua zaidi, kwa wakati mmoja, aone anapata unafuu wa bei kwa maana kiwango cha bidhaa anachopata kinaongezeka kwa rate kubwa zaidi ya pesa inayoongezeka. Hii logic inasound simple lakini utashangaa biashara nyingi hawaifuati.
Sasa inapokuja kwenye mitandao ya simu maana yake ni kwamba, kama kwa mfano unanunua kifurushi cha Tsh. 500 unapata dakika 5 za maongezi, inatakiwa wakiweka kifurushi kingine cha Tsh. 1000, mtu apate ZAIDI ya dakika 10 za maongezi ili impe motisha wa kununua kifurushi cha Tsh. 1000 badala ya kununua cha Tsh. 500 halafu arudi tena kununua kingine. Hii ni kwa sababu, kwa ushindani wa kibiashara uliopo, haujui kama mtu akimaliza kifurushi chake, atarudi kwako au atakwenda kununua kwenye mtandao mwingine.
Ona hvi vifurushi vya TTCL:
Mitandao karibu yote ilikuwa nao huu upungufu, wengine mnaweza kuthibitisha katika mitandao kama ya TIGO, Halotel na Airtel ila nimepitia hapa nimeona Vodacom waliliona hili wakarekebisha ila bado lipo katika vifurushi vya TTCL.
Ona hivi vifurushi vya Vodacom (baada ya kulitambua hili).
Nimewa single out watu wa mitandao ya simu, ila inawezekana huu uelewa haujulikani/hautumiwi na biashara za aina nyingi Tanzania.