Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Hata hivyo, kama ilivyo kwa kila fursa;fursa hii imekuja na changamoto zake. Moja wapo ni baadhi ya watumiaji wake kueneza habari za uongo, uchochezi, taharuki n.k ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi.Hii imekuwa ndio changamoto kubwa ya maendeleo haya.
Changamoto kubwa zaidi inakuja pale unapoanza mjadala juu ya namna ya kuishukulikia changamoto ya hapo juu. Shida inaanza pale tunapodhani tatizo ni mitandao ya kijamii yenyewe na wakati kimsingi, tatizo ni watu “Jamii yenyewe” . Kama jamii tukishakosea kutafsiri tatizo, maana yake pia tutakuja na mapendekezo ya ‘solution’ ambayo si sahihi vile vile.
Mitandao ya kijamii ni kama Ndege, Treni za umeme au basi. Vitu hivyo kwa u-asili wake, ni vitu vizuri lakini pia vinaweza kuleta maafa makubwa kama ikitokea kuna mtumiaji ambaye ana matatizo. Kwa mfano mlevi au kichaa akitumia chombo kimojawapo, anaweza kuua mamia au maelfu ya watu, na tumeshuhudia matukio kama hayo mara nyingi tu.
Hata hivyo, hatuwezi kusema, kwa kuwa kuna watu wenye matatizo wanaotumia vyombo hivyo; basi solution visitumike, au kwa kuwa vinabeba watu wengi na ikitokea madhara watu wengi wanaathirika ndani ya sekunde, basi tutafute viji - chombo ambavyo vitakuwa vinabeba watu wawili wawili ili hata ikitokea tatizo waathirike wachache. Nafikiri hapo kutakuwa na tatizo la kimtizamo.
Kwa hiyo mitandao ya kijamii ni muhimu sana hasa kama tunaamini demokrasia ndio mfumo bora kuliko mingine. Ni muhimu kuelewa kwamba chenye tatizo ni baadhi ya watumiaji na sio mitandao.Pia, Watumiaji tunaowaona ni ‘reflexion’ ya jamii tuliyo nayo; kwa hiyo, tukitaka kupata matokeo bora, tuongeze nguvu kwenye kubadili mitizamo ya kijamii kwani yale wayaandikayo watu mitandaoni, ni mwangwi wa yale wayawazayo vichwani mwao.