Mitandao isitumike kumchafua Rais

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Kwa muda mrefu mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kumchafua Rais JAKAYA KIKWETE kwa mambo ambayo hayahusiani kabisa na majukumu yake ya kuongoza serikali.

Yapo mambo mengi ambayo watu kupitia mitandao wamekuwa wakimchafua Rais na hapa nitatoa michango michache tu:-

1) Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mtoto wake aitwaye MWANAASHA KIKWETE yametumika sana kumchafua JK.
2) Thread iliyoletwa hapa JF na kichwa cha habari "Maswali mia moja kwa Rais KIKWETE" yakiwemo yaliyohoji ana wake wangapi na mengine mengi yalioonekana ni ya kumchafua Rais zaidi na hayakuwa ya kiutendaji.

Yapo mengine mengi ambayo kiukweli hata kurudia kuyaandika hapa hayafai.


Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/02/2012 katika ukurasa wake wa Tahariri (The Editorial page) mhariri ameandika kuhusu hili kwa kichwa cha habari "Mitandao isitumike kumchafua Rais". Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.

Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012

 

wanamchafua au wanasema ukweli?
 
pole ila nafikiri magazeti au media inaripoti yale ambayo yameshatokea na hata kama hayataandikwa bado hayatafutika....yatajulikana tu...big figures ni target za media and somehow that is the prize they have to pay for being "big." It happens everywhere sio Tanzania tu......
 
Ni kumchaua Jk....watoto wake wakubwa wanawajibika kwa taia lao kulipa deni hilo na wana kazi. Ninachokubaliana nacho ni kwamba kweli wamemchaua baba yao.
 
Tutamjadili, tutamkosoa na tutasemakweli, kama hataki tumjadili aachie ofisi.Mbona watu hawanijadili mimi, yeye kautaka urais basi akubali kuwa yeye ni kioo cha jamii akicheka anajadilwa,akikohoa anajadilwa akiumwa anajadiliwa, hakuna jinsi lazima tumchane live lakini bila kumkashifu wala kumtukana. UKWELI LAZIMA USEMWE.
 
Tanzania Daima kwa mara ya kwanza nawapongeza kuliona hili. Mitandao inatumika vibaya ingawa sio wakati wote.
 
JamiiForums is a 'User Generated Content' site

Hutaki unaacha.
1)Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.

Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012
 
JK angeweza hata kumpeleka mtoto wake nje na tusingejua yote haya. Amesoma shule za ndani kwa nini tusimpongeze kwa hilo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…