Nimefatilia kwa muda mitandao (websites) inayouza magari hapa Tanzania. Nimewasiliana na watu zaidi ya kumi wamekataa kuwa hayo magari hawayajui na wameshangaa simu zao kutumika katika hayo matangazo.
Wengine wamekubali kuwa hayo magari ni yao nikawaomba wanionyeshe yalipo au tukutane hawakuwa tayari kunionyesha wala kukutana nao, hivyo kupata wasiwasi kama sio wezi basi ni matapeli wa mjini.
Wapo walioweka magari ya kwenye website za nje kama cartradeview na beforward lakini nilivyowaambia wanitumie picha za karibuni kuonyesha kuwa hayo magari wanayo hawakuwa tayari kufanya hivyo.
Ipo haja ya jeshi la polisi kufuatilia hii biashara ya vitu mitandaoni (online sales) ikiwemo magari ya mitandaoni naamini wapo wahanga wengi wa matukio haya ya kitapeli au kuuziwa magari ya wizi. Nimejaribu kufuatilia Contact za hizo website hazifanyi kazi wala email zao hazijibiwi, hivyo ni muhimu TCRA TRA na Jeshi la polisi kufuatilia hii mitandao ya uuzaji vitu ili kujiridhisha kuwa sio mitandao ya kihalifu.