Mitaala ya Elimu bado ni tatizo

Mitaala ya Elimu bado ni tatizo

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,956
Reaction score
7,007
Wana bodi, nchi ndio maana ina mikosi mingi, haisogei. Tatizo ni watunga mitaala, wasimamizi na watendaji wetu.

Leo wife ambaye anafundisha darasa la tano geography, kaniomba nimsaidie kusahihisha mitihani ya kumaliza muhula darasa la tano geography.

Sasa nimepewa marking scheme, hivyo natakiwa nisahihishe kuifuata. Ila pepa ya kwanza nasoma swali kwa swali na nalinganisha jibu halisi na lililo kwenye marking scheme.

Nimeshtushwa kwenye swali kuwa, "Africa mashariki imeundwa na nchi_________
(a) Tano
(b) kumi
(c) mbili
(d) tatu.

Watoto wamejibu d) tatu, hivyo aliyejibu tano anatakiwa apewe kosa.

Hivi wizara ya elimu mmekuwa mkifumdisha watoto wetu upuuzi huu tangu 2009 hadi leo 2017 kweli?

Yaani hadi sasa wizara ya elimu hamtambui kuwa Rwanda na Burundi ni wanachama hai wa africa mashariki?

Yaani hata wabunge na maspika waliotoka burundi na rwanda kwenu walikuwa wanapoteza muda wao kwenye afrika mashariki?

Aisee, nchi yetu inaumwa sana, tena sana. Tuliko fika ni kubaya zaidi.

Sasa natamani waliojibu tano niwape vema na waliojibu tatu niwalime. Lkn ntakuwa nimewaonea, siyo kosa lao. Vitabu vyao vinawaelekeza hivyo.

Majanga.

9300034145e1cbc87089e976faca8ebf.jpg
 
Hao wengine wameomba kujiunga,kiuhalisia ni nchi tatu,na zimeunganishwa na ziwa victoria
 
as long as wanaojiita policy makers and curriculum developers wanakuna vitambi tu hawaoni tatizo acha liende hivo hivyo.

hujiulizi hilo bomu linalo tengenezwa la watoto kujibu maswali kwa kutia kivuli mtihani wa hisabati!!!
tutafika tu kwenye ulimwengu wa viwanda.
 
Kila kukicha mambo yanabadilika ...ila yaliyoandikwa hayabadiliki mkuu..saizi waziri wa elimu ni ndalichako na vitabu vyote vimeandikwa ivoo na wanafunzi wanaelewa ivoo...siku akitumbuliwa na kitabu kilisha andika ivoo..watoto watakuwa wanajibu according to kitabu kinavosema ...hatakama waziri ni mwinginee...hili tatizooo
 
Back
Top Bottom