Mitaala mibovu ya elimu ya Tanzania

Mitaala mibovu ya elimu ya Tanzania

tonnylee

Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
24
Reaction score
4
Katika dunia ya leo ya habari (information age) fedha ni muhimu sana. Je, ni kwanini mfumo wetu wa elimu hautoi fursa kwa wanafunzi kujua mfumo na tabia ya fedha katika dunia na uchumi wa kibepari (capitalism) ili kuzalisha watu huru (wanaojiajiri) badala yake mfumo wa elimu unatengeneza watu wanaotegemea kuajiriwa?

NAOMBENI WATU WALIO KWENYE SEKTA YA ELIMU WANIPE MAWAZO KATIKA HILI.
 
Ukierejea Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ndio utapata jibu ,sina muda tu ila ningei-attach hapa, ukiitazama kwa macho ya kawaida tu utagundua kuwa hii sera ni nzuri ila endapo tu itafanyiwa utekelezaji wa angalau 85%.Lakini shida inaanza katika utekelezaji wa sera yenyewe ,utekelezaji wa sera hii umekuwa ni mgumu sana na ndicho kitu kinapelekea tunashindwa kupata matokeo halisi ya sera, vifuatavyo ni vitu vinavyokwamisha maendeleo na utekelezaji wa sera
1. SIASA(hili lipo wazi kabisa katika mfumo wa nchi yetu,suala la kumpa mtu aongoze eneo ambalo hana uwezo nalo ndio umekuwa mwiba mchungu wa utekelezaji wa sera na mitaala yetu,mfano kuna mwaka hapo wizara ya elimu walichanganya masomo ya Chemistry na Physics kuwa somo moja ,wakafuta masomo ya biashara na kufuta michezo mashuleni.Lakini tukirejea hii sera ya elimu ya 2014 ambayo ilitamkwa wazi inataka walimu kuanzia ngazi ya diploma ina maana inafuta walimu wa cheti/Grade A lakini ilipotoka serikali iliyopita na kuingia iliyopo ikarudisha tena walimu wa cheti/Grade A vyuoni )

2.WATAALAMU(Kukosekana kwa wataalamu katika eneo husika ambao wangeweza kutoa ushauri katika maeneo ya uundwaji na utekelezaji sera na mitaala ambayo ni rafiki na mazingira na uchumi wetu ndio tatizo kubwa sana,matokeo yake wanasiasa wamekuwa na nguvu ya kutuyumbisha katika eneo hili)

3.UCHUMI WA NCHI
(A/Sera hii ilitaka mwalimu wa kiwango cha chini kabisa awe na elimu ya Stashahada/Diploma yaani kuanzia elimu ya awali na msingi,lakini naona suala la uwezo wa kifedha limepelekea hili kutofanyika,maana walimu hawa waliandaliwa lakini hawakuajiriwa na mpaka leo wapo mitaani hawana future.
B/Sera hii ilitaka ratio/uwiano wa darasa uwe ni 1:25 kwa darasa la awali na 1:45 kwa darasa la msingi na sekondari lakini habari imekuwa tofauti kutokana na ufinyu wa miundombuni na rasilimali watu ambao ni walimu,matokeo yake ratio ya sasa ni kawaida kukuta 1:90 < kwa darasa la awali na msingi pia sekondari)

Ikumbukwe Sera ndio ambayo inazaa mtaala>Mtaala ndio unazaa Wawezeshaji mtaala husika (Walimu), kama sera ni mbovu, basi itazaa walimu wabovu pia ambao ndio wanaenda kuandaa wanafunzi kule chini,
Kwa ufupi shida imeanzia hapo maana MBOVU INAANDAA MBOVU,huwezi lima nyanya ukavuna vitunguu,kama mwalimu mwenyewe anawaza kuajiriwa atamuandaaje mwanafunzi mwenye mawazo ya kujiajiri!!!!!

kwa mfano sasa hivi haijulikani ni sera ipi ya elimu inatekelezwa huko mavyuoni na mashuleni,maana kuna mambo yanayofanyika sasa hivi ni kinyume na sera iliyopo inavyotaka,sera haitaki grade A na pia sera haitaki mfumo uliopo wa elimu,sera ilitamka wazi Elimumsingi itakuwa ni ya madarasa 10 yaani mfumo wa sasa ni 2-10-2-3+ lakini mpaka sasa bado mfumo ni 2-7-4-2-3+ ambao ni wa sera ya elimu ya 1995

Ahsante
 
Back
Top Bottom