Mitaala chuo cha Polisi Moshi ipitiwe upya

Mitaala chuo cha Polisi Moshi ipitiwe upya

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,153
Reaction score
162,570
Kutokana na malalamiko ya wananchi dhidi ya utendaji kazi wa Jeshi letu la Polisi, pengine ni vizuri kupitia upya mitaala ya chuo hicho kuona hali ikoje.

Polisi wetu wanafanya kazi kutokana na mafunzo wanayopata hivyo basi huenda huko ndiko kwenye tatizo la msingi kama malalamiko haya ya wananchi yana uhalali.
 
kutokana........huenda.........
.
.
.hebu weka vizur hii ki2
 
kutokana........huenda.........
.
.
.hebu weka vizur hii ki2
 
Kutokana na malalamiko ya wananchi dhidi ya utendaji kazi wa Jeshi letu la Polisi, pengine ni vizuri kupitia upya mitaala ya chuo hicho kuona hali ikoje.

Polisi wetu wanafanya kazi kutokana na mafunzo wanayopata hivyo basi huenda huko ndiko kwenye tatizo la msingi kama malalamiko haya ya wananchi yana uhalali.

Mhmhhh hebu tuambie utendaji gani labda au mtaala gani ubadilishweeee!!
 
Shida iko kwenye vyeti vyao vya form four!! Rejea kagua kagua ya vyeti vyao na zoezi kuzimwa ghafla!! Kwa hilo tu ndo tatizo! Tumikia kafiri ilimradi tu upate ujira wako!!
 
Mhmhhh hebu tuambie utendaji gani labda au mtaala gani ubadilishweeee!!


Kitendo cha mtu mmoja aliyefungwa pingu mkononi kulizidi nguvu kundi la askari karibu kumi na kulazimika kumua kwa kummiminia risasi kimelivua nguo jeshi zima. Sasa kama raia wa kawaida wanayakamata majammbazi yakiwa hayana pingu wanayapiga mpaka yanakufa bila kutumia bunduki, mpaka hapo huoni kua kuna tatizo?
 
Kitendo cha mtu mmoja aliyefungwa pingu mkononi kulizidi nguvu kundi la askari karibu kumi na kulazimika kumua kwa kummiminia risasi kimelivua nguo jeshi zima. Sasa kama raia wa kawaida wanayakamata majammbazi yakiwa hayana pingu wanayapiga mpaka yanakufa bila kutumia bunduki, mpaka hapo huoni kua kuna tatizo?

hahahahaa uono wako ni mzurii but there is something hidden here :-!🙂:-🙂-$ sio kirahisi hivyo walikuwa wanatafuta sababu ya kumpiga chumaaa au we unaonajee jee ni kawaida kwa hilo kutokeaaaa?
 
hahahahaa uono wako ni mzurii but there is something hidden here :-!🙂:-🙂-$ sio kirahisi hivyo walikuwa wanatafuta sababu ya kumpiga chumaaa au we unaonajee jee ni kawaida kwa hilo kutokeaaaa?

wewe ndo great thinker mkuu
 
Mutoa maada hunakazi yakufanya pita hivi ukojoe ulale.unahoji mamulaaka hivyo we alivyokua anaandaa mauwaji ya watu wasiyokuwa na hatia we uliona safi bac muosha huoshwa
 
Mhmhhh hebu tuambie utendaji gani labda au mtaala gani ubadilishweeee!!
Kwa hisan ya Malisa Godlisten ...soma hii...
Wazungu husema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu nzuri.. "Liars must have a good memory"

Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa ya kuuawa kwa kijana Yahaya Omary mtuhumiwa wa milipuko ya mabomu Arusha. Polisi wanasema wamemuua kwa kumpiga risasi mguuni na kwenye ---- alipokua akijaribu kukimbia.

Lakini picha ya marehemu iliyoonekana baadae inaonesha kupigwa risasi ya tumbo. Sasa kwanini Polisi wamedanganya ni mguu na ----?? Wanataka kuficha nini?

Bila shaka Polisi walidhani picha ya mtuhumiwa akiwa kauawa haitaonekana.. hivyo wakaamua kudanganya ili kuhalalisha mauaji. Lakini hatimaye picha imeonekana akiwa kapigwa risasi ya tumbo, Polisi wameumbuka.

Pili, hivi mtu anayekimbia anapigwaje risasi ya tumbo? Alikua anakimbia kinyumenyume au? Maana kama kweli alikua anakimbia angepigwa risasi kwa nyuma si tumboni.

Lakini hii si mara ya kwanza jeshi la Polisi kuingia kwenye tuhuma za kuua watu wasio na hatia na kushindwa 'kujustify' mauaji hayo.

Mwaka 2006 aliyekua kaimu RPC wa mkoa wa Dar, Bw.Abdalah Zombe aliorganize mauaji ya wafanya biashara wa madini kutoka Mahenge Morogoro na kusingizia ni majambazi. Akafika mbali zaidi na kudai walikua wanarushiana risasi na Polisi.!

Lakini ripoti ya Tume ya Jaji Kipenka ikawaumbua Polisi maana ripoti ilionesha watuhumiwa wote walikua wamepigwa risasi visogoni. Ikabainika pia si kweli kuwa walikua wakirushiana risasi na polisi.

Huwezi kurushiana risasi na Polisi then upigwe risasi kisogoni.. Jaji Kipenka akawaumbua Polisi kwa kueleza kuwa wafanyabiashara wale walifungwa kamba mikono na miguu, kisha wakafungwa vitambaa vyeusi machoni ndipo wakapigwa risasi.

Halafu baada ya kuhakikisha wameuawa Polisi wakawapora jumla ya sh. mili.200 na madini waliyokua nayo. Kisha Zombe akaita mkutano na waandishi wa habari akasema kuna majambazi yameuawa yakijaribu kurushiana risasi na Polisi.

Ukatili, ukatili, ukatili wa kiwango cha kutisha. Yani uwakamate watu wasio na hatia, uwafunge vitambaa usoni, uwapige risasi, kisha uwapore mali na fedha walizonazo.. halafu bado uwasingizie ujambazi.. Kwa kweli Mungu wetu ni wa huruma sana lakini hii dhambi sijui kama inasameheka.

Mazingira ya kuuawa kwa wafanyabiashara wale yanafanana na mazingira ya kuuawa kwa kijana Yahya Omary anayedaiwa kulipua mabomu Arusha.

Kwanza inadaiwa alikua anakimbia, lakini risasi kapigwa tumboni. How comes? Mtu anayekimbia tulitegemea apigwe risasi mgongoni au maeneo ya nyuma ya mwili lakini si tumboni. Huu ni uongo wa kitoto kabisa.!

Polisi wanadai eti mtuhumiwa alikua mcheza karate na judo, hivyo alitumia mbinu zake za karate ili kuwakimbia Polisi.

Cha ajabu mtuhumiwa alikua hajafungwa Pingu mikononi wala miguuni. Hivi unaweza kumkamata mtuhumiwa wa kulipua mabomu tena anayejua kucheza "karate na judo" halafu umsafirishe bila kumfunga pingu? Hizi ni hekaya za Abunuasi.!

Halafu Polisi wanasema eti alitoroka akiwa chini ya Ulinzi mkali.. Hivi Ulinzi mkali ndo kumsafirisha mtuhumiwa bila pingu?? Uongo wa kitoto kabisa huu.!

Nashauri Rais Kikwete aunde tume kuchunguza mauaji ya kijana huyu kama alivyounda Tume ya Jaji Kipenka kuchunguza mauaji ya wale wafanya biashara wa Mahenge. Huenda kijana huyu ameuawa ili kupoteza ushahidi.!

Huenda Polisi wanamjua mhusika wa mabomu ya Arusha, na labda ni "kigogo mkubwa" ambaye hawawezi kumgusa.. Hivyo wameamua kumuua kijana Yahaya ili kupoteza ushahidi.

Nimeona vyombo vingi vya habari vikiandika habari hii kwa ushabiki. Vingi vimeonesha kufurahishwa na mauaji ya kijana huyu. Gazeti moja limeandika "ALIYELIPUA MABOMU ARUSHA AUAWA".

Hili gazeti sijui kama lina Mhariri, maana hii si habari. Huwezi kusema "aliyelipua mabomu arusha..." wakati haijadhibitika kama ni kweli alihusika au lah.!

Yahaya alikua mtuhumiwa tu na angefikishwa mahakamani ukweli ndio ungejulikana. Huenda si yeye aliyehusika na mabomu na labda hata hajui lolote kuhusu mabomu.. Labda Yahaya alikua na ugomvi na kiongozi wa serikali ndo akaamua kumbambikia hii kesi.

Na chombo pekee cha kusema ukweli ni mahakama.. Lakini serikali kwa kujua kesi ikienda mahakamani wataumbuka na itajulikana Yahaya hakuhusika na mabomu ya Arusha wakaamua kukatisha maisha.

Wakamuua kikatili kabla kesi haijaenda mahakamani. Wawakamsingizia eti alijaribu kukimbia. Kivipi alijaribu kukimbia wakati kapigwa risasi ya tumbo.?

Lakini magazeti yamemhukumu.. yamemuita muuaji.. mrusha mabomu.. mengine yamemuita jambazi sugu..

Nayaogopa magazeti ya Tanzania. Ni magazeti hayahaya yaliyowahukumu wale wafanyabiashara wa Mahenge waliouawa na Polisi wa Zombe. Magezeti yakaandika "MAJAMBAZI KUTOKA MORO YAUAWA DAR."

Lakini ilipokuja kubainika hawakua majambazi magazeti hayohayo yakaandika "KASHFA NZITO JESHI LA POLISI; WADAIWA KUUA RAIA WASIO NA HATIA NA KUWABAMBIKIZIA KESI YA UJAMBAZI"

R.I.P Yahaya Omary, binafsi siwezi kukuhukumu kama magazeti yanavyofanya, maana sijui kama ni kweli ulihusika na mabomu ya Arusha au lah.

Labda mahakama ingeweza kutuambia ukweli.. lakini kwa kuwa umetangulia MUNGU pekee ndio anajua ukweli.

Pumzika kwa amani Yahaya.. Hata waliokuua ipo siku nao watakufuata. Duniani sote tunapita.. hakuna atakayeishi milele.. ipo siku ukweli utafahamika na itakuwa kilio na kusaga meno kwa wote walioshiriki mauaji haya ya kinyama dhidi yako.!

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.!

Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.!
 
Last edited by a moderator:
Ukiisha ona hamna haki,kaa kwako jilie vyako usichokoze/usibugudhi wala kuziba mirija ya watu mirija ya watu watakufuta kwenye historia.
 
of course you are.. wale sio wajinga mkuuu, eti jamaa kawaambia ana mabomu kahifadhi Dodoma alafu wamuue kabla hajayatoa?? si hayo hayo mabomu yatawasumbua tena???

Hahahahaaaa daaa ndio ushangae na sio mabom yatawasumbua wao yatatusumbua sss.wao wanajua hata kukwepaa sisi jeee wamefanya kosa kubwa.ambalo limenifanya ni we na wasiwai juu ya hilo jamboo. but kama kuna kitu kinaendelea r i p marehem
 
Back
Top Bottom