RVR nyingi hapa bongo zimebadilishwa engine kwa kuweka ya corolla; tembelea karume soko la batiki pale Ilala utakutana na fundi mashuhuri wa RVR ukapate UHALISIA
Rvr itakulazimu kubadilisa injini, na ukishabadilisha tu utalazimika kurekebisha vile vyuma vilivyoshika matairi ya mbele.
Kwa kifupi sikushauri kununua hilo gari ni pasua kichwa.
Labda kama unataka kulinunua kwa ajili ya kuchezea gofu.
Nina rvr na imenipa shida hasa gearbox. Zina matatizo kwenye seal mojawapo ambayo baada ya muda hupasuka. Hata mimi nataka kubadilisha engine. Nimeambiwa engine ya rav 4 au corolla zinafaa, sina uhakika.