Mwl. Kaijage
JF-Expert Member
- Jan 3, 2015
- 216
- 214
Mfumo wa kuwa na Kiongozi Mkuu wa Chama (Party Leader) na Mwenyekiti wa Chama (Party Chairperson) ni mfumo mpya kwa siasa za Tanzania. Lakini mfumo huu umekuwa ukitumika kwenye nchi mbalimbali duniani na haujawahi kuleta mgongano wala hitilafu yoyote katika vyama husika.
ACT WAZALENDO katika kuitendea haki dhana ya Mabadiliko kimekuwa chama cha kwanza katika historia ya siasa za Tanzania kuanzisha mfumo huu.
Kazi na Majukumu ya Kiongozi Mkuu wa chama yameainishwa wazi katika katiba ya chama cha ACT WAZALENDO kama ambavyo Kazi na Majukumu ya Mwenyekiti wa chama yameainishwa katika Katiba ya chama pia.
Mfumo huu kwa siasa zetu za kitanzania ni mgeni ni ACT WAZALENDO imeandika historia kuwa chama cha kwanza kufuata mfumo huu.
Nchi kadhaa duniani wanafuata mfumo huu.
Mfano:
1: David Milliband
Huyu ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Conservative cha nchini Uingereza lakini sio Mwenyekiti wa Chama hicho.
2: Raila Omolo Odinga
Huyu ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ODM nchini Kenya lakini sio Mwenyekiti wa chama hicho.
3: Jacob Zuma ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ANC lakini sio Mwenyekiti wa ANC
Kiufupi mfumo huu umekuwa na tija kubwa kwa vyama vinavyoutumia kwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Chama ni:-
(i) Taswira na nuru ya chama ndani na nje ya nchi.
(ii) Ni mkuu wa siasa za chama, mshauri na muelekezaji.
(iii) Ndio msimamizi mkuu wa Sera, Itikadi, Falsafa na Mtazamo wa chama.
(iii) Ni mfano wa kuigwa ndani ya chama.
(iv) Ndio mtoa habari mahususi kwenye Mkutano Mkuu, Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya chama kuhusu hali ya kisiasa nchini na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.
ACT WAZALENDO imedhamiria kwa dhati kupambana na mfumo unaowafukarisha watanzania na shabaha yake kubwa ni kuchochea ujenzi wa taifa la kujitegemea lisilona unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na kwa kuzingatia misingi ya haki kwa watu wake wote.
Chama kimejiwekea misingi ambayo ni:-
1. Uzalendo
2. Usawa
3. Uwazi
4. Kupiga vita ubaguzi
5. Uadilifu
6. Uwajibikaji
7. Demokrasia
8. Uhuru wa Mawazo na matendo
9. Utu
10. Umoja
Katika kutekeleza misingi hii ACT WAZALENDO imeamua kuwa na mfumo wa uongozi ambao ni shirikishi na wa kugawana majukumu ndio maana kimeamua kwa makusudi kutumia mfumo wa kuwa na KIONGOZI WA CHAMA na MWENYEKITI WA CHAMA ili kuhakikisha kuwa Sera, Itikadi na Falsafa zake zinatekelezwa kwa vitendo na kuwakomba watanzania.