Mwemezi Farms
New Member
- Jul 9, 2025
- 4
- 3
Kama umekua ukihangaika kuanzisha kilimo cha tikiti maji lakini hufahamu pakuanzia, basi makala hii ni mahususi sana kwako.
Nasema hivo, kwa kua nimekua nikilima matikiti kwa muda mrefu tangu 2020 na hapa nitatiririka na misingi 5 ambayo itakuasaidia wewe kuanzisha mradi wa kilimo cha tikiti Maji.
Endapo utahitaji ufafanuzi wa aina yoyote, unaweza kuliza swali kwenye comment na nitakusaidia.
Sasa, tutiririke.
1. Soko:
Soko la matikiti maji ni makubwa + mengi kwa kua yanahitajika kwa wingi. Lakini, kuna changamoto hapa kwenye soko.
Soko la Uhakika limekua gumzo sana, wakulima wengi wamekua wakihangaika na swala zima la "Bei", na hii ni kutokana na kutokufahamu soko la zao hili vizuri.
Hapa nitakuandikia vitu kadhaa ambavyo huenda vikakusaidia kwenye utafutaji wa soko.
- Mlengwa/Mteja wako hasa ni nani?
Zingatia Yafuatayo:
i. Baada ya Mavuno ni nani atakaye nunua zao lako? Utauza jumla ama reja reja?
ii. Anapatikana wapi?
Ni vyema kufahamu mahala mteja/mlengwa wako anapo patikana ili kufahamu gharama za usafirishaji wa zao.
iii. Anahitaji mzigo kiasi gani?
Mlengwa wako, ana uwezo wa kukwambia kiwango/kiasi cha mzigo anachohitaji kwa msimu 1 ama hata mwezi.
Hii itakusaidia kuweka mikakati ya kilimo chako shambani.
2. Aina ya Kilimo.
Kuna aina nyingi za kilimo ambazo unaweza kutumia kwenye matikiti. Hapa chini nitakuorodhoshea aina chache na ww utachagua ya kwako.
i. Kilimo Hai (Organic Farming)
ii. Kilimo Mseto (Mixed Farming
iii. Kilimo Biashara (Commercial Farming)
iv. Kilimo cha kujikimu (Subsistence farming)
V. Kilimo cha umwagiliaji (Irrigation Farming)
iv. Kilimo Cha mvua (Seasonal/Rain farming)
Nikisema ni orodheshe ni vingi ila kwa leo, chukua hizo 6 zinakutosha.
Btw, kabla sijaendelea, ni kutaarifu kwamba, endapo unahitaji msaada kwenye maswala ya kilimo cha tikiti, ninapatikana kwa nambari +255 689 568 707.
Tuendele,
Misngi nambari 3 ni eneo unalohitaji kulima Tikiti Maji.
Iko hivi, eneo ambalo linafaa kulima tikiti maji ni eneo ambalo lina sifa hizi hapa;
i. Kichanga: jitahidi udongo wako uwe wa kichanga hii itasaidia kwenye ukuaji wa haraka + mbegu hautachelewa kutoka ardhini.
ii. Udongo unashauriwa kua na ph ya 5.5-7.5 ikiwa chini ama juu kutakua na changamoto kwenye matunzo + ukuaji wa zao la tikiti maji
iii. Hakikisha eneo lako lina fikika. Usafiri wa magari ni muhimu zaidi kwa kua baada ya mavuno utahitaji kuleta usafiri ili upeleke sokoni. Endapo eneo halifikiki utapata tabu + gharama za ziada za kudafirisha mzigo
mpaka hapa popcorns hazijaisha? Kaongeze nyingine uendelee kusoma.
4. Khali ya hewa.
Hapa, usipokua makini unaweza chekeshwa pasipo kutekenywa na kulia pasipo kupigwa.
Khali ya hewa huenda ikawa ni baridi, joto ama mvua.
Tanzania tunapitia misimu mikuu 3 na hiyo ni:
- Masika
- Baridi
- Kiangazi
- Vuli.
Kwenye misimu yote hii, una uwezo wa kulima ila, changamoto ya misimu hii yote ni mingi na kwa leo sitaweza kuziongelea maana ni parefu.
Cha muhimu unachopaswa kufahamu ni kwamba, tikiti haipendi baridi sana wala mvua nyingi.
Post ijayo nitakuelekeza khali ipi ya hewa ina faa zaidi kwenye kilimo cha tikiti maji.
Kwani niko namba ngapi, ni kama vile nimesahau, nikumbushe hapa chini kwenye comment ili niendelee.
Oooohhhh..... Nimekumbuka nipo kwenye msingi nambari 5, asante sana.
Sasa hapa kwenye huu msingi unaitwa Mbegu Bora.
Hapa kwenye mbegu Bora, itategemea na aina ya kilimo ambacho utahitaji kukifanya.
Hivyo, ni vyema ukafahamu kwamba, aina ya kilimo itaendana na aina ya mbegu.
Tena nimekumbuka, unakumbuka lile swala la "Soko"? Sasa huyo jamaa ndiye mwenye uwezo mkubwa wa kukusaidia kwenye mbegu.
Kwanini nimesema Soko litakysaidia? Kaa chonjo kwenye post zitakazo kuja nitakueleza.
Ila, chukua hii kwa urahisi na kwa kifupi sana.
Kuna aina nyingi za mbegu na hapa nitakuorodhoshea chache.
i. Mbegu za tikiti zisizokua na Mbegu (Seedless Watermelon)
ii. Mbegu za tikiti zenye Mbegu
iii. Mbegu za asili
🤣, ushachangajikiwa? Niambie umechanganyukiwa ukiwa wapi?
Tukutane kwenye post zijazo nitakazokua nina fafanua kila kipengele kwa kina.