Misiba yawa mtaji wa kisiasa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Sep 23, 2012.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  "Salaam kwa mkt wa CHADEMA MKOA WA MOROGORO.

  Dada yangu habari za jumapili, kwanza nikukumbushe kwamba leo ni siku ya ibada kwa kuwa natumai wewe ni mkristo, tufanye siasa, lakini daima mungu mbele.

  Nasikitika kutuma salamu hizi kwako, ambazo ni aibu kwako wewe kama mwenyekiti na pia chama chako kwa ujumla,

  Ndg mwenyekiti, makada wa chama chako ndg Juma Tembo na mwanasheria asiyejitambua ndg Tarimo wakiwaongoza vijana wengine katika siku ya juz, majira ya mchana, mtaa wa mkwajuni, kata ya kichangani, wilaya ya moro mjini, makada hawa walileta vurugu za hatari na zisizo na msingi wowote MSIBANI kwa kugombea mwili wa marehemu Amina Juma ambaye mama yake mzazi bi Annastazia ni kada wa chama cha mapinduzi CCM.

  Mmoja kati ya makada niliowataja hapo juu ambaye inasemekana ana mahusiano ya karibu na ya undani na bi Mchilo ambaye ni mama mdogo wa marehemu ndiye aliyekuwa kichochez kikubwa katika vurugu hizo za kijinga, ndg huyo kwakuwa alitoa hela ya mchele na nyama kwa ajili ya shughuli za mazishi, akichanganya na mahusiano yake ya karibu na familia ya marehemu alitumia nafasi hiyo kutaka kuugeuza msiba huo kama jukwaa la kisiasa na eneo la kisiasa la kufanya kampeni za CHADEMA.

  Juma tembo na tarimo waliagiza magari meupe Pick up nne zilizoandikwa M4C, ambazo kwa wakati wote zilikuwa zikirandaranda msibani, kilichotokea...

  1 wakati wa chakula makada hao waliwapanga vijana wa chadema kugawa chakula huku wakimuuliza kila anayekuja kuchukua chakula ajitambulishe kwamba yeye ni wa chama gani? Na akisema yeye ni wa CCM ananyimwa chakula, akisema chadema anapewa chakula kingi. Na akisema hana chama basi anaambiwa kuanzia leo ajiunge na CHADEMA.

  2 matusi na kashfa nzito zilitolewa na makada wa chadema hadharani huku watu wakiwasikiliza, matusi na kashfa hizo ziliekezwa kwa diwan wa kata hiyo komandoo John Waziri(ccm) Mhe Aziz Abood mbunge wa kudumu milele jimbo la morogoro mjini(ccm) viongoz mbali mbali wa ccm, na serikali ngaz ya wilaya mkoa mpaka taifa.

  3 makada wako walishinikiza, waligombea, walitukana na kulazimisha mwili wa mtoto huyo upandishwe kwenye moja ya magari yaliyoandikwa M4C.

  Chama cha mapinduz ccm kilipata mafanikio makubwa katika msiba huo kwa kuweza kuzidhibiti vurugu hizo za chadema kikiongozwa na katibu wa ccm wa kata hiyo bi subira mashaka, vijana wa uvccm wakiongozwa na kamanda wa kata hiyo ndg Hamis Zikatimu, ambao kwa kiasi kikubwa walihakikisha mwili wa mtoto wa kada wa ccm bi Annastazia unapandishwa kwenye gari la ccm. Kama mwenyewe alivyotaka na kusema huku akilia kwamba "nataka maiti ya mwanangu ipandishwe kwenye gari la ccm)

  Viongoz wa ccm wa kata hiyo walichukua hatua hiyo ya kuleta gari la ccm MAHINDRA kutoka ccm wilaya, baada ya kuona mlolongo wa magari ya chadema yakiwa yanazunguka hovyo hovyo msibani kinyume cha taratibu.

  Hekima na busara za vijana wa ccm ndizo zilizo sababisha kutokumwagika damu msibani hapo kwani wananchi wengi walikuwa wameshachukizwa na vurugu hizo za Chadema. Tuliwasihi greengard wetu wawe wapole na watumie hekima zaid ili watofautiane kimaadili mbele ya jamii na vijana wa chadema. Vijana wa ccm walifanikiwa kwa hilo.

  Ndg mwenyekiti, hivyobasi, naomba umkanye ndugu Juma Tembo ambaye mara zote amekuwa akikichafua chama chenu hapa morogoro kwa siasa zake za vurugu, akiwa mgombea wa ubunge jimbo la morogoro mashariki ambapo alishindwa vibaya na mgombea wa ccm ndg Innocent Kalogerez, Juma Tembo mwaka huo wa 010 alipata mkong'oto wa nguvu kutoka kwa greengard wa ccm ambapo ghafla akilitumia gari la chadema aliuingilia msafara wa ccm katikati ambao ulikuwa umetoka kwenye kampeni kata ya sultan, nikiwa ndani ya gari la greengard pamoja na katibu wa uvccm w beatrice tuliwaruhusu vijana wamtandike vizuri sana juma tembo, na vijana wakiongozwa na massawe walimpa discpline ya nguvu mpaka kakimbilia polisi ambapo alionekana mjinga kwa kuingilia msafara ambao haumuhusu.

  Mwenyekiti waambie vijana wako kwamba, watambue

  1 msibani sio eneo la kufanya siasa, ni eneo la majonz na linalowakutanisha watu wa iman tofaut, si vyema kugawa watu kwa misingi ya vyama na siasa.

  2 kutukana viongoz wa nchi ni kuvunja sheria za nchi, ni upuuz, ni ushamba wa siasa, ni ujinga uliopitiliza na kutaka kuifanya nchi yetu isitawalike. Hatujengi, tunabomoa

  3 Demokrasia isiyofuata sheria ni janga na maafa kwa taifa, marazote chama chenu kimekuwa ni chanzo cha vurugu, maandamano na mikutano isiyofuata taratibu, matusi na makelele yasiyo na maana, si vyema

  Dada yangu mkt, waelimishe makada wako na umwambie Juma na wakili tarimo, iwe mwanzo na mwisho, wamevumiliwa sana, siku nyingine wakileta vurugu msibani kama vile, hakika vijana wetu watazirejesha nidhamu zao kwa vitendo. Juma anajua vizuri sana

  Jumapili njema..."
  By Mdau - Morogoro.

  Familia zimegawanyika katika mazishi ya mtoto kutokana na itikadi za kisiasa. - YouTube


  My take: Iwapo jitihada hizi zingeelekezwa kwenye upatikanaji wa maji safi au uboreshaji wa shule zetu na huduma za afya pamoja na miundombinu, tungekuwa mbali sana kimaendeleo. Badala yake watu wanashindana kununua chakula misibani na kupeperusha bendera zao kwenye magari ya kubeba jeneza!!!

  Ni wapi tunakwenda?
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Huyo mtoto wa ccm au cdm? Maana kwangu Youtube mtihani.
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mtoto wa kada wa CCM lakini CDM wamedonate chakula na then wakaleta magari yenye bendera za CDM kubeba mwili wa marehemu, viongozi wa CCM wakaingilia kati kukataa magari yenye bendera za CDM yasibebe mwili kwenda makaburini. Matokeo yake kukawa na mvutano. Serikali ikatoa amri kuwa mwili ubebebwe na gari lisilo na bendera.
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hapo nimekupata mkuu,naunga mkono hoja...Kwamba jitihada hizo zingefanywa kwenye maendeleo tungekuwa mbali sana.
   
 5. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  kwenu ccm uongo imekua jadi, nyie ndo vijana mpo kwenye mafunzo ya uongo
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 6,027
  Trophy Points: 280

  Haikupatwa kunenwa kwamba akufaaye wakati wa dhiki ndiye rafik wa kweli? Au, mahali pengine haikuandikwa kwamba " ... na jirani yangu ni nani?" CCM bana hata haya hamna?
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mbona mnakuwa na jazba? Hapa kilichotolewa ni taarifa na hakuna aliyesema nani yuko sahihi au amekosea. Kinachoonekana dhahiri ni kwamba ushindani ungeelekezwa kwenye shughuli za maendeleo tungekuwa mbali, lakini cha ajabu shughuli za maendeleo tuko radhi kuzihujumu lakini umaarufu wa hapa na pale tuko tayari kuvuliana mashati...
  Lengo letu liwe kusonga mbele...
   
 8. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Cha ajabu kipi? Acheni kuiga kauli za wakata tamaa CCM. Siasa ni everywhere! Jikoni, sebureni, shambani, kiwandani, kazini, arusini, msibani na popote itapowezekana? Wapi utaikwepa siasa??? Ukienda Hospitalini ukakosa dawa, utawalaumu watawala, si siasa hiyo?! Ukikodi gari la kusafirishia maiti kwa bei kubwa sababu ya petrol kupanda bei utalaumu watawala si siasa hiyo??
   
 9. t

  tenende JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unakuuza mambo kuliko uhalisia. Hakuna jipya hapa, zaidi ya unafiki!.. Ni kitu gani kigeni kwako katika misiba? Hujawahi kuona wafiwa wakiwa na mgogoro na majirani? Hujawahi kuona mvutano kati ya ndugu wa mke na ndugu wa mume kuhusu mazishi? hujawahi kuona mvutano wa kidini katika mazishi?. Chadema ikijitokeza kwenye misiba inakohusika mnapiga kelele! Ikiwekewa mizengwe mnaleta UDINI. Ndiyo maana mnyika alisema bungeni ninyi "MACHIZI!"
   
 10. t

  tenende JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuna aibu kwa CHADEMA hapa ni uhuni na ushabiki tu. Habari hii imeripotiwa pia na ITV, hii familia imegawanyika kiitikadi, sasa kwa nini CDM isiende kumfariji mwanachama wake aliyefiwa? After all, watu wote waliosikiliza ITV watashangaa kusoma ***** ulioleta jamvini. CCM ndiyo walioleta mvutano huo ili walinde maslahi ya ya chama.
   
 11. t

  tenende JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Habari umeipamba ili mradi cdm waonekane wabaya! Kuna ubaya gani cdm kugawa chakula msibani?

  Wasipo kuja mnasema hawana utu, wakija lazima mzushe!
   
 13. t

  tenende JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huu ni ushabiki wa kipuuzi mno, ni sawa na propaganda zilizotolewa na POLISISIEM na sisiemu kuwa CDM wamemrushia MWANGOSI kitu kizito.
   
 14. t

  tenende JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CDM wauaji wa wagombea wetu hawa hapa!.. ZE marcopolo ni kiongozi wa Green guard, na mpiga watu. Ni mtu hatari saana!.. CDM jihadharini naye. Mpo naye hapo morogoro.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  Mkuu haiwezekani kufanywa jitihada za kuleta maendeleo wakati uchumi wa nchi umeshikwa na mafisadi na wageni. Wale BoT wanadai uchumi unakuwa kila mwaka lakini wanaozidi kuneemeka ni mafisadi na wageni.

   
 16. t

  tenende JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ujumbe uliopo You tube unajieleza vizuri CCM waliingilia baadaye ili waonekane wanajali.
   
 17. t

  tenende JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CDM mjue - green guard si walinzi wa amani. Ni wapigaji na wauaji. Bila shaka mauaji ya Igunga na Singida yalipangwa na kufanywa na hawa hawa akina marcopolo. GREEN GUARD NI JANGA LA TAIFA!. Green guard ni Hizbollar na Alshabab ya Tanzania. Kuwepo kwao ni hatari kwa amani ya nchi yetu!. Ipo siku mtabip na raia watapiga!.
   
 18. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi kuna sehemu wabunge wamepitishwa wawe wa kudumu? Maana naona hapa ''Mh. Abood mbunge wa kudumu Mororgoro mjini''. Ushabiki wa kisiasa,upambe,propaganda au nn hasa?
  Ushindani kama huo uwe katika kuwapatia wananchi huduma bora za jamii na sio kugombea kubeba maiti.
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Angalia vizuri video ya yourtube. Kulikuwa na ulazima gani kupeleka magari yenye bendera za chama katika msiba wa mtoto ambaye siyo mwanachama wala kiongozi wa chama.
  Sijaribu kusema kuna upande uko sahihi, ninachojaribu kusisitiza ni kujikita zaidi kwenye kushindania mambo ambayo outcome yake ni maendeleo. Ingefurahisha zaidi kuona vyama vya siasa vinagombania kutoa michango ya vitabu mashuleni, kuchimba visima etc.
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  tenende umeshindwa kuelewa.
  Nilichofanya mimi ni kuleta habari. Mimi sio mwandishi wa habari husika.
  Kuleta habari JF kutoka vyanzo mbalimbali ni jambo la kawaida hapa JF, wewe inawezekana hujui hilo kutokana na ugeni wako.
  Ukitaka kusoma maoni yangu angali kwenye "my take".
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...