Mishahara ya walimu wa vyuo

Mishahara ya walimu wa vyuo

DASA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
1,031
Reaction score
302
Hivi inakuaje mishahara ya walimu wa vyuo Tanzania haina mfanano. Mishahara ya walimu kama UDSM ni midogo sana ukilinganisha na vyuo vingine hapa nchini hata vile vinavyofundisha ngazi za chini.

Mfano ukiajiliwa leo kama Lecturer kwenye vyuo hivyo vingine mshahara wako utakuwa ni mkubwa sana kuliko Lecturer wa UDSM mwenye miaka mingi kwenye hiyo post hata kama ulianza kazi kama Tutorial Assistant. Je ni kweli huu ni mkakati wa kuuwa hivi vyuo vikongwe hapa nchini!!.

Kuna baadhi ya walimu tunawaona wanahangaika kwenye maofisi zetu wakitafuta kazi mbalimbali za ziada badala ya kutulia vyuoni na kujipanga kufundisha vizuri vijana wetu. Chuo kama UDSM sasa hata miundo mbinu pale ni choka mbaya.

Hostel zake ni choka mbaya, barabara choka mbaya, madarasa choka mbaya. Wanafunzi choka mbaya. Sasa hivi hata ukitangaza ajira pale UDSM utaishia kupata TAs tu, wengine hata hawata-apply.

Na hata hao waliopatikana ni mguu nje mguu ndani. Hivi hiki chuo kitakuwepo kweli baada ya miaka 10 hivi na heshima yake ikawa ni ileile!!!, nina wasiwasi mwingi sana kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuvikomboa hivi vyuo vyetu vikongwe.

Inanisikitisha sana kama mwalimu wangu aliyenifundisha UDSM anakuja kubangaiza kwenye ofisi zetu mtaani. Tatizo ni nini!!.

Walio serikalini hawakusoma kwenye hivi vyuo au!!, Au Serikali yetu Elimu ni jambo la mwisho.
 
Ni kweli, but ni chuo bora kwa walimu vichwa, wanafunzi wenye akiri nyingi, walimu wa udsm hawategemei mishahara, kazi yao kubwa ni research za world bank, eu,undp etc, walimu wanauwezo mkubwa kufanya consultancy na uwezo mkubwa wa kufanya research. Ondoa shaka ndio maana kinaongoza africa kasoro south africa
 
Ni kweli vyuo binafsi vinapackage ya kuwavutia wahadhiri ila kwa mtu asiyependa kusukumwa na kuwapigia watu magoti, vyuo vya serikali ikiwemo udsm ni best choice.
 
Back
Top Bottom