sir.JAPHET
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 699
- 133
Dk Slaa aionya Serikali ya Kikwete | Send to a friend |
Friday, 24 August 2012 23:21 |
Venance George, Morogoro KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibroad Slaa, amesema kuwa kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini posho na marupurupu ya wabunge na viongozi wa ngazi za juu Serikalini na kugoma kutoa nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa kada nyingine ni kitanzi kitakachoing'oa Serikali yake. Akizungumza katika mikutano ya hadhara kwenye vijiji mbalimbali vya kata za Mvuha na Mtamba, Jimbo la Morogoro Mashariki, Wilaya ya Morogoro juzi, alisema kitendo cha Serikali ya Rais Kikwete kuendelea kukandamiza makundi mbalimbali katika jamii, hasa wafanyakazi, wakulima na wafugaji, huku ikikwepa kujadili na kushughulikia vyanzo vya manung'uniko yao ya muda mrefu kutaendelea kuiweka kitanzini Serikali yake. Alisema, Kikwete amekuwa akiidhinisha mishahara mikubwa na marupurupu mengine kwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano hadi kufikia Sh11 milioni kwa mwezi, huku wakati huo huo akiwaambia watumishi wa kada zingine kuwa Serikali yake haina fedha za kuwalipa. Dk Slaa, aliwataka wafanyakazi kote nchini kutohamishia hasira zao kwa wananchi badala yake waendelee ‘kukabana koo' na Serikali ya Rais Kikwete kwani ndiyo adui yao mkubwa. "Juzi nimesoma kwenye mtandao, naona walimu wanatumiana meseji, (ujumbe mfupi) kwenye simu zao ambao kama kweli wataufanyia kazi maskini wa watoto wetu hawa walioko shuleni na taifa lote tumekwisha. Kama kweli ujumbe ule wa kwenye simu wanaotumiana walimu ambapo wanaelekezana kuwafundisha uongo wanafunzi ikiwa ni ishara ya kuonesha kinyongo chao cha kupuuzwa kwa madai yao ya msingi na Serikali ya Kikwete…kama kweli wataamua kuufanyia kazi taifa hili litaangamia zaidi ya lilivyoangamia hivi sasa," alisema. Katibu mkuu huyo wa Chadema, aliwaomba walimu kupunguza hasira na kuwataka wasihamishie hasira zao watoto wasiokuwa na kosa na kuongeza kuwa kila mtu mwenye akili timamu anajua madai ya msingi ya walimu hao na kudai kuwa adui mkubwa wa walimu hao ni Serikali. "Mkabeni koo kwa namna yoyote mnayoweza lakini msiwafundishe uongo watoto wetu, watoto wa dada zenu, watoto wa ndugu zenu walioko shuleni...taifa hili limeshaangamia kiasi cha kutosha, limeshazama kiasi cha kutosha, mkifanya hivyo walimu wangu mnakwenda kulimaliza kabisa," alisisitiza Dk Slaa. Dk Slaa alisema, binafsi anatambua uhalali wa madai ya walimu hao lakini Rais Kikwete mara nyingi amekuwa akiwaambia watu kuwa Serikali yake haina fedha za kuwaongezea mishahara na kuwalipa posho za mazingira magumu walimu na wafanyakazi wengine. "Kikwete huyo huyo ndiye juzi amesaini kupanda kwa mishahara ya wabunge kutoka Sh7 milioni na ushee na kuwoangezea milioni tatu na ushee, hivyo sasa wabunge wanachukua Sh11 milioni kila mwezi," alisema. Alidai kuwa Rais Kikwete anafanya hivyo wakati anajua askari polisi mishahara na posho zao ni midogo, japokuwa imeongezwa kidogo baada ya wabunge wa chadema kupiga kelele bungeni na kwamba kwa sasa kima cha chini cha askari polisi kimeongezeka kutoka Sh100,000 hadi Sh150,000. Dk Slaa alisema, pamoja na kada zingine za utumishi wa umma kama walimu kudharauliwa, ikiwamo Serikali kupuuza maslahi yao, huku wakiendelea kutimiza wajibu wao katika mazingira magumu yanayowafanya waonekane wanafanya kazi za kujitolea, bado ndizo zenye mchango mkubwa zaidi kwa taifa lolote linalotaka kuendelea. Alisema kuwa vitendo vya Serikali vimekuwa vikiwatia vishawishi baadhi ya watumishi kama walimu vya kulazimika kufanya kazi zingine, akitolea mfano wa walimu wa kike ambao wanalazimika kupika na kuuza maandazi au vitumbua kupata fedha za kujikimu na kuendesha maisha ya familia zao. |
[h=2][/h] Jumamosi, Agosti 25, 2012 06:41 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibroad Slaa, amesema kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini nyongeza ya mishahara na marupurupu ya wabunge hadi kufikia Sh milioni 11 kwa mwezi hakiwezi kukubalika.
Amesema kwamba, pamoja na kwamba lengo la Rais Kikwete ni kuwafanya wabunge wafanye kazi kwa moyo, hatua hiyo italeta manung'uniko kwa kuwa wafanyakazi wengi wamekuwa wakilalamikia maslahi madogo wanayolipwa.
Dk. Slaa alitoa shutuma hizo juzi alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara katika vijiji vya kata mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mashariki, Wilaya ya Morogoro.
Katika mikutano hiyo, Dk. Slaa aliwataka wafanyakazi kote nchini, kutohamishia hasira zao kwa wananchi badala yake waendelee kuikaba koo Serikali kwa kuwa ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha yanayowakabili.
"Tangu juzi nimekuwa nikisoma taarifa mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, naona walimu wanatumiana ujumbe mfupi wa simu katika simu zao na kama kweli wataufanyia kazi, masikini watoto wetu hawa walioko shuleni na taifa lote tumekwisha.
"Kama kweli ujumbe ule wa kwenye simu wanaotumiana walimu ambapo wanaelekezana kuwafundisha uongo wanafunzi ikiwa ni ishara ya kuonyesha kinyongo chao cha kupuuzwa kwa madai yao ya msingi na Serikali ya Kikwete, tunaelekea pabaya. Kama kweli wataamua kuufanyia kazi taifa hili litaangamia zaidi ya lilivyoangamia sasa.
"Chonde chonde walimu wangu, naombeni hasira zenu msizihamishie kwa watoto wangu hawa wasiokuwa na kosa lolote, kila mtu mwenye akili timamu anajua madai yenu ni ya msingi sana, lakini adui yenu ni Kikwete, adui yenu ni Serikali," alisema Dk. Slaa.
Aidha, alisema hivi sasa kumekuwa na matamshi mabaya dhidi ya walimu ambapo wanaambiwa Serikali haina fedha za kuwalipa stahiki zao.
"Wakati Serikali ikiwambia wananchi hakuna fedha, leo hii sekta ya ya afya haina dawa wala vitendea kazi hospitalini.
"Pamoja na hali hiyo, bado Rais Kikwete anaamua kupandisha mishahara na marupurupu ya wabunge kutoka milioni 7 hadi kufikia Sh milioni 11.
"Kwa hali hii, hakika Rais Kikwete pamoja na Serikali yake ya CCM haiwatendei haki wananchi wa taifa hili, kwani hivi sasa vijana wetu ambao ni maaskari polisi, mishahara yao ni kidogo.
"Yaani hata posho yao wametetewa na wabunge wangu huko bungeni ndiyo imepandishwa kwa maneno kutoka 100,000 hadi 150,000.
"Bado wanafanya hivyo wakati wanajua makundi mengine wakiwamo walimu, madaktari, wanajeshi na makundi mengine wana malalamiko ya msingi, sasa ni kitu gani hiki?.
"Lakini, kumbukeni kwamba, mambo ya namna hii yanaweza kufanywa na uongozi mbovu usiozingatia vipaumbele katika kusukuma maendeleo na ustawi wa watu wake," alisema Dk. Slaa.
Alisema vitendo hivyo vya Serikali vimekuwa vikiwatia vishawishi baadhi ya watumishi kama walimu na kulazimika kufanya kazi zingine jambo ambalo siyo zuri wa ustawi wa taifa.
Alitolea mfano wa walimu wa kike ambao wanalazimika kupika na kuuza maandazi au vitumbua, ili kupata fedha za kujikimu na kuendesha maisha ya familia zao.
[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
Dk slaa raisi wangu uliye jaa ndani ya moyo wangu umenena jambo zuri sana pambana uzidi kuweka histor kwenye taifa hili tuna kutegemea na tuna amini wewe ndiye raisi wa nchi hii ingawa auna escot ya usalama wa taifa na mabenz na mapikipiki una ulinzi wa mungu na watu unao waongoza, tunakuombea sana
hizo siasa tu, hapo ndio uwongo wa wanasiasa unapo onekana.
Mbona wabunge wake hawakupinga?
Kwenye kuongezwa mishahara au posho ndo unafiki wa wabunge unapodhihirika, sio upinzani wala ccm. Wote kwenye hela wananywea.
Katiba mpya itabidi itusaidie kuondoa hili tatizo.