Mishahara ya wabunge: Dk. Slaa amshukia JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara ya wabunge: Dk. Slaa amshukia JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 25, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Jumamosi, Agosti 25, 2012 06:41 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibroad Slaa, amesema kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini nyongeza ya mishahara na marupurupu ya wabunge hadi kufikia Sh milioni 11 kwa mwezi hakiwezi kukubalika.

  Amesema kwamba, pamoja na kwamba lengo la Rais Kikwete ni kuwafanya wabunge wafanye kazi kwa moyo, hatua hiyo italeta manung’uniko kwa kuwa wafanyakazi wengi wamekuwa wakilalamikia maslahi madogo wanayolipwa.

  Dk. Slaa alitoa shutuma hizo juzi alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara katika vijiji vya kata mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mashariki, Wilaya ya Morogoro.

  Katika mikutano hiyo, Dk. Slaa aliwataka wafanyakazi kote nchini, kutohamishia hasira zao kwa wananchi badala yake waendelee kuikaba koo Serikali kwa kuwa ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha yanayowakabili.

  “Tangu juzi nimekuwa nikisoma taarifa mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, naona walimu wanatumiana ujumbe mfupi wa simu katika simu zao na kama kweli wataufanyia kazi, masikini watoto wetu hawa walioko shuleni na taifa lote tumekwisha.

  “Kama kweli ujumbe ule wa kwenye simu wanaotumiana walimu ambapo wanaelekezana kuwafundisha uongo wanafunzi ikiwa ni ishara ya kuonyesha kinyongo chao cha kupuuzwa kwa madai yao ya msingi na Serikali ya Kikwete, tunaelekea pabaya. Kama kweli wataamua kuufanyia kazi taifa hili litaangamia zaidi ya lilivyoangamia sasa.

  “Chonde chonde walimu wangu, naombeni hasira zenu msizihamishie kwa watoto wangu hawa wasiokuwa na kosa lolote, kila mtu mwenye akili timamu anajua madai yenu ni ya msingi sana, lakini adui yenu ni Kikwete, adui yenu ni Serikali,” alisema Dk. Slaa.

  Aidha, alisema hivi sasa kumekuwa na matamshi mabaya dhidi ya walimu ambapo wanaambiwa Serikali haina fedha za kuwalipa stahiki zao.

  “Wakati Serikali ikiwambia wananchi hakuna fedha, leo hii sekta ya ya afya haina dawa wala vitendea kazi hospitalini.

  “Pamoja na hali hiyo, bado Rais Kikwete anaamua kupandisha mishahara na marupurupu ya wabunge kutoka milioni 7 hadi kufikia Sh milioni 11.

  “Kwa hali hii, hakika Rais Kikwete pamoja na Serikali yake ya CCM haiwatendei haki wananchi wa taifa hili, kwani hivi sasa vijana wetu ambao ni maaskari polisi, mishahara yao ni kidogo.

  “Yaani hata posho yao wametetewa na wabunge wangu huko bungeni ndiyo imepandishwa kwa maneno kutoka 100,000 hadi 150,000.

  “Bado wanafanya hivyo wakati wanajua makundi mengine wakiwamo walimu, madaktari, wanajeshi na makundi mengine wana malalamiko ya msingi, sasa ni kitu gani hiki?.

  “Lakini, kumbukeni kwamba, mambo ya namna hii yanaweza kufanywa na uongozi mbovu usiozingatia vipaumbele katika kusukuma maendeleo na ustawi wa watu wake,” alisema Dk. Slaa.

  Alisema vitendo hivyo vya Serikali vimekuwa vikiwatia vishawishi baadhi ya watumishi kama walimu na kulazimika kufanya kazi zingine jambo ambalo siyo zuri wa ustawi wa taifa.

  Alitolea mfano wa walimu wa kike ambao wanalazimika kupika na kuuza maandazi au vitumbua, ili kupata fedha za kujikimu na kuendesha maisha ya familia zao.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 2. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"] Dk Slaa aionya Serikali ya Kikwete [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 24 August 2012 23:21 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Venance George, Morogoro
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibroad Slaa, amesema kuwa kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini posho na marupurupu ya wabunge na viongozi wa ngazi za juu Serikalini na kugoma kutoa nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa kada nyingine ni kitanzi kitakachoing'oa Serikali yake.

  Akizungumza katika mikutano ya hadhara kwenye vijiji mbalimbali vya kata za Mvuha na Mtamba, Jimbo la Morogoro Mashariki, Wilaya ya Morogoro juzi, alisema kitendo cha Serikali ya Rais Kikwete kuendelea kukandamiza makundi mbalimbali katika jamii, hasa wafanyakazi, wakulima na wafugaji, huku ikikwepa kujadili na kushughulikia vyanzo vya manung'uniko yao ya muda mrefu kutaendelea kuiweka kitanzini Serikali yake.

  Alisema, Kikwete amekuwa akiidhinisha mishahara mikubwa na marupurupu mengine kwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano hadi kufikia Sh11 milioni kwa mwezi, huku wakati huo huo akiwaambia watumishi wa kada zingine kuwa Serikali yake haina fedha za kuwalipa.

  Dk Slaa, aliwataka wafanyakazi kote nchini kutohamishia hasira zao kwa wananchi badala yake waendelee ‘kukabana koo' na Serikali ya Rais Kikwete kwani ndiyo adui yao mkubwa.

  "Juzi nimesoma kwenye mtandao, naona walimu wanatumiana meseji, (ujumbe mfupi) kwenye simu zao ambao kama kweli wataufanyia kazi maskini wa watoto wetu hawa walioko shuleni na taifa lote tumekwisha. Kama kweli ujumbe ule wa kwenye simu wanaotumiana walimu ambapo wanaelekezana kuwafundisha uongo wanafunzi ikiwa ni ishara ya kuonesha kinyongo chao cha kupuuzwa kwa madai yao ya msingi na Serikali ya Kikwete…kama kweli wataamua kuufanyia kazi taifa hili litaangamia zaidi ya lilivyoangamia hivi sasa," alisema.

  Katibu mkuu huyo wa Chadema, aliwaomba walimu kupunguza hasira na kuwataka wasihamishie hasira zao watoto wasiokuwa na kosa na kuongeza kuwa kila mtu mwenye akili timamu anajua madai ya msingi ya walimu hao na kudai kuwa adui mkubwa wa walimu hao ni Serikali.

  "Mkabeni koo kwa namna yoyote mnayoweza lakini msiwafundishe uongo watoto wetu, watoto wa dada zenu, watoto wa ndugu zenu walioko shuleni...taifa hili limeshaangamia kiasi cha kutosha, limeshazama kiasi cha kutosha, mkifanya hivyo walimu wangu mnakwenda kulimaliza kabisa," alisisitiza Dk Slaa.

  Dk Slaa alisema, binafsi anatambua uhalali wa madai ya walimu hao lakini Rais Kikwete mara nyingi amekuwa akiwaambia watu kuwa Serikali yake haina fedha za kuwaongezea mishahara na kuwalipa posho za mazingira magumu walimu na wafanyakazi wengine.

  "Kikwete huyo huyo ndiye juzi amesaini kupanda kwa mishahara ya wabunge kutoka Sh7 milioni na ushee na kuwoangezea milioni tatu na ushee, hivyo sasa wabunge wanachukua Sh11 milioni kila mwezi," alisema.

  Alidai kuwa Rais Kikwete anafanya hivyo wakati anajua askari polisi mishahara na posho zao ni midogo, japokuwa imeongezwa kidogo baada ya wabunge wa chadema kupiga kelele bungeni na kwamba kwa sasa kima cha chini cha askari polisi kimeongezeka kutoka Sh100,000 hadi Sh150,000.

  Dk Slaa alisema, pamoja na kada zingine za utumishi wa umma kama walimu kudharauliwa, ikiwamo Serikali kupuuza maslahi yao, huku wakiendelea kutimiza wajibu wao katika mazingira magumu yanayowafanya waonekane wanafanya kazi za kujitolea, bado ndizo zenye mchango mkubwa zaidi kwa taifa lolote linalotaka kuendelea.

  Alisema kuwa vitendo vya Serikali vimekuwa vikiwatia vishawishi baadhi ya watumishi kama walimu vya kulazimika kufanya kazi zingine, akitolea mfano wa walimu wa kike ambao wanalazimika kupika na kuuza maandazi au vitumbua kupata fedha za kujikimu na kuendesha maisha ya familia zao.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni MTAJI wa Chadema 2015
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,506
  Trophy Points: 280
  Serikali ina uwezo wa kupandisha mishahara ya Wabunge tu, kwa madaktari, walimu na wafanyakazi wengine Serikali haina uwezo.
   
 5. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu Padri mwongo sana mbona hasemi chadema yeye wanamlipa shilingi ngapi? kama sio mshahara huo huo wa mbunge? mtu huyu ndio alikuwa anategemewa awapeleke wakristo kwa mungu, kazi kweli kweli!!!
   
 6. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  CCM ni janga na kero kubwa sana TZ.
   
 7. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willbroad Slaa amelaani kitendo cha Rais Jakaya Kikwete cha kuidhinisha mishahara mikubwa na marupurupu kwa wabunge wakati watumishi wa kada zingine wakiambiwa serikali haina fedha za kuwalipa stahiki zao.

  Amesema kuwa siku za hivi karibuni Rais Kikwete ameidhinisha malipo kwa wabunge hadi kufikia Sh milioni 11 kwa mwezi huku akishindwa kuwaongezea mishahara walimu pamoja na madaktari.

  Akizungumza katika mikutano ya hadhara kwenye vijiji vya kata mbalimbali za Jimbo la Morogoro kusini, mkoani hapa, Dk. Slaa aliwataka wafanyakazi kote nchini kutohamishia hasira zao kwa wananchi baada ya kushindwa kutekelezwa kwa madai yao badala yake waendelee kuibana serikali kwani ndiyo adui yao mkubwa.

  Alisema kuwa anashangazwa na Rais Kikwete katika hotuba yake ya hivi karibuni wakati akihutubia Taifa na kuwaambia walimu na madaktari hakuna fedha za kuwaongezea mishahara na kuwalipa posho za mazingira magumu wala kuboresha sekta ya afya lakini ameshasaini nyongeza ya wabunge kutoka Sh. milioni 7 hadi milioni 11 kwa mwezi.

  Alisema kuwa kitendo cha serikali kuendelea kukandamiza makundi mbalimbali katika jamii, hasa wafanyakazi, wakulima na wafugaji, huku ikikwepa kujadili na kushughulikia vyanzo vya manung’uniko yao ya muda mrefu kutaendelea kuiweka kitanzini hivyo kupunguza ari ya wananchi katika juhudi za kujitafutia maendeleo.

  “Niliona kwenye mtandao, nikaona walimu wanatumiana meseji, ujumbe mfupi kwenye simu zao ambao kama kweli wataufanyia kazi maskini watoto wetu hawa walioko shuleni na taifa lote watakuwa katika hali mbaya,” alisema Dk Slaa.

  Aliwataka watumishi hao wa kada mbalimbali kuacha kuzihamishia hasira zao wananchi ikiwa pamoja na wanafunzi ambao hawana kosa lolote badala yake waendelee kuikataa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kushindwa kuwalipa madai yao.

  “Chondechonde walimu wangu naombeni hasira zenu msizihamishie kwa watoto wetu kwani hao hawana kosa lolote, kila mtu mwenye akili timamu anajua madai yenu ni ya msingi sana, lakini adui yenu ni Rais Kikwete, anayeongoza Serikali ya CCM,” alisema Dk Slaa.

  Alisema kuwa Chadema inajua uhalali wa madai ya wafanyakazi na kwamba kinachofanywa na Serikali si kwamba haina fedha za kuwalipa bali imekuwa ikipuuzia madai hayo ambayo andapo rasilimali za nchi hii zingeweza kutumiwa vizuri madai mengi yangetekelezwa.

  Katika hatua nyingine, akizungumza katika mikutano ya hadhara katika vijiji mbalimbali vya Kata za Ngerengere na Makambarai, Dk. Slaa aliwaambia wananchi kuwa serikali ya CCM ambayo imetawala kwa miaka 50 imeshindwa kuwahudumia hasa kutengeneza fursa za wananchi kujitafutia na kupata maendeleo kwa ajili ya ustawi wao.
  CHANZO: NIPASHE

   
 8. peri

  peri JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  hizo siasa tu, hapo ndio uwongo wa wanasiasa unapo onekana.
  Mbona wabunge wake hawakupinga?
  Kwenye kuongezwa mishahara au posho ndo unafiki wa wabunge unapodhihirika, sio upinzani wala ccm. Wote kwenye hela wananywea.
  Katiba mpya itabidi itusaidie kuondoa hili tatizo.
   
 9. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Wabunge wa chama gani wameongezewa mishahara......tawala au na wa vyama vya upizani pia wameongezewa hiyo mishahara??????

  Hakutoa msimamo wa chama chake yeye kama katibu mkuu..........?????
  Hajaitisha maandano this time arround????


  Unapokuwa na kiu mtu anakuja na kerosene........siku ukiwa uanhitaji kerosene uwashe moto huyo huyo tena nakuja na maji safi.....duuuh kazi ipo
   
 10. h

  holypotato Senior Member

  #10
  Aug 26, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 107
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nafikiri huyu jamaa siye anayeendesha nchi, he is just a figure-head, kuna wanaoendesha hii nchi ambao ndio wanafanya maamuzi yote kupitia huyu figure-head. Else haingii akilini haya yanayofanyika. Kuwaongezea marupurupu wabunge kwa lipi hasa???? Au ndio kuwapoza ili wasiibananishe govt.... No wonder maazimio hayafanyiwi kazi na govt na wabunge wapo kimya tuu....
  Niliiipenda tz nchi yangu ila sasa mmh.....
   
 11. R

  Rwey Senior Member

  #11
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  porojo tu
   
 12. peri

  peri JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mbona wabunge wa upinzani hawakukataa hiyo nyongeza?
  Mbona hawakushinikiza serekali itoe nyongeza pia kwa waalim na madaktari kama walivyoshinikiza maswala ya ufisadi au sheria ya mafao?
  Hapo ndo unafik wa wanasiasa unapo onekana, kwenye maslahi yao wote ni kitu kimoja bila kujali chama.
  Hizo kelele za dr slaa ni porojo tu kwani yeye kama ktb mkuu wangeweza kuchukua hatua kama chama lkn hawakufanya.
   
 13. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  sina maoni.
   
 14. m

  majebere JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  yeye mbona anakula 7m na hakuna anae lalamika. Huyu mzee kweli ni Mnafiki.
   
 15. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hili la mishahara ya wabunge ni janga la Taifa, haijalishi chama.
   
 16. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wote wezi tu
   
 17. z

  zamlock JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Dk slaa raisi wangu uliye jaa ndani ya moyo wangu umenena jambo zuri sana pambana uzidi kuweka histor kwenye taifa hili tuna kutegemea na tuna amini wewe ndiye raisi wa nchi hii ingawa auna escot ya usalama wa taifa na mabenz na mapikipiki una ulinzi wa mungu na watu unao waongoza, tunakuombea sana
   
 18. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Unamuombea mnafiki kaazi kweli kweli mbona hajatoa msimamo wa kukataa hizo posho mpya kwa wabunge wake? Mbona yeye mwenyewe analamba sawa sawa na wabunge? Think twice brother nawe usiwe mnafiki kama huyu Padri aliyeasi kanisa
   
 19. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  kuna haja ya kujua wabunge wa CDM wanasemaje katika hili. maana kama kweli wameridhia, itabidi tuwe na wasiwasi nao. watuambie tu, walifanya nini kuzuia hili, hata kama walipinga lakini wakazidiwa nguvu na wale jamaa wa ndioooooooooo!!!! tuna haja ya kujua ili tujiridhishe.
   
 20. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pampafu wewe slaa wanayekuita dr kweli umeishiwa zinakuuma. Ungekuwa mbunge na wewe ungepata. Mbona 7m ambazo na wewe ulishiriki kujilipa husemi. Acha kupata pressure wambie mbowe na wife wake wakuongezee na wewe .nakukumbu$ha mkataba mliokubaliana na cdm juu ya masharti ya kuwa vuvuzela wao. Lazima wakulipe 11m soon. Acha wivu wa k... Mzee.
   
Loading...