Unatoa pongezezi za ahadi!?!?Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Watumishi wa umma kaeni mkao wa kupokea mishahara minene. Kwa muda mrefu sasa tangu Dr Magufuri aanze kurekebisha mifumo ya utawala wa nchi, watumishi wa umma walionekana kama wametengwa sana hadi baadhi yao kupelekea kukata tamaa ya maisha. Sasa mkae mtulie…mambo yenu yameiva!
Kuna taarifa kwamba Serikali imepanga kuongeza mishahara ya watumishi wa umma maradufu ifikapo September baada ya kufanikiwa kuwaondoa watumishi na wanafunzi hewa na kupunguza mishahara ya baadhi ya watumishi waliokuwa wakilipwa mamilioni ya shilingi huku wengine wakilipwa mishahara uchwara, hivyo fedha zote zilizookolewa zimeelekezwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakilalamikia udogo wa mishahara kwa muda mrefu. Aidha, taarifa zinadai kuwa watumishi wote wanaostahili kupanda vyeo/madaraja watapandishwa na kuanza kulipwa mishahara mipya mara moja.
Ifahamike kwamba wakati Dr Magufuri anaomba ridhaa ya kuongoza nchi hii aliwaahidi maslahi bora watumishi wa umma, hivyo ahadi yake ndio inaanza kutekelezwa sasa. Kumbe lilikuwa ni suala la wakati tu. Sasa civil service imeanza kupata mwanga uliokuwa umekosekana kwa muda mrefu na kupelekea watumishi wa umma kuvunjika mioyo ya kuwatumikia wananchi. Hongerza sana Dr Magufuri kwa kuwajali watumishi wa umma.
Wakati wa kanpein kila mradi mkubwa ulizinduliwa mara general tyre, mara gas II kinyerezi mara flyover sasa hiyo miradi iko wapiKwa nini kila kitu kinaangukia September mosi?
wewe utakuwa mwalimu tuAsee bora ametukumbuka maana hali ilikua mbaya Sanaa uku maofisini
Umesahau kupatwa kwa juaSeptember 1:
Maandamano ya UKUTA nchi nzima.
September 1:
Siku ambayo jeshi la wananchi Tanzania litafanya usafi huko Arusha.
September 1:
Imetajwa kua siku ya kuongezwa mishahara kwa wafanyakazi wa uma, ikiwemo kupandishwa vyeo kwa wanao stahili.
September 1:
Dr Slaa ana timiza mwaka mmoja kuanzia pale 1 September 2015, alipo tangaza rasmi kujingatua Chadema na kujiondoa kwenye siasa.
Wazee wa kupinga kila kitu.....!!!Kwa bajeti ipi iliyopitishwa na bunge, itakuwa ni kuingilia muhimili mungine wa dola
Usiache la kupatwa na jua mkuu!September 1:
Maandamano ya UKUTA nchi nzima.
September 1:
Siku ambayo jeshi la wananchi Tanzania litafanya usafi huko Arusha.
September 1:
Imetajwa kua siku ya kuongezwa mishahara kwa wafanyakazi wa uma, ikiwemo kupandishwa vyeo kwa wanao stahili.
September 1:
Dr Slaa ana timiza mwaka mmoja kuanzia pale 1 September 2015, alipo tangaza rasmi kujingatua Chadema na kujiondoa kwenye siasa.
Na hizi pia zina husika tarehe moja.Umesahau kupatwa kwa jua
U
Usiache la kupatwa na jua mkuu!
mkuu, kuanzia septemba mishahara itapanda na watumishi wanaostahili kupanda vyeo watapandishwa na kuanza kulipwa mishahara yao mara moja.
Madeni yenyewe yamewashinda kuwalipa watumishi ,miaka nenda rudi ni uhakiki na ahadi zizizo na ukomo;je Leo uwezo wa kuongeza mishahara watatoa wapi?Mkuu tpaul hiyo hela yenyewe ya kuongeza mishahara mara mbili itatoka wapi? Ni jambo zuri kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa umma hata mara tatu, lakini Serikali hii haina pesa na mapato ya Serikali yanaanguka kwa kasi ya kutisha labda wakaombe mkopo mwingine wa trilioni kadhaa Exim Bank ya kule China ili waweze kufanya hivyo.