Mishahara kulipwa na Benki Kuu,je wana uzoefu au ndio issue za kuchelewesha mishahara?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,634
7,010
Nimeingiwa na wasiwasi kuwa huenda sasa baada ya miaka 20 ya watumishi kuzoea kulipwa mshahara kati ya tarehe 22 na 25 ya kila mwezi,sasa itaanza kuchelewa baada ya jukumu hilo kupewa watu wa Benki Kuu.

Nina wasiwasi kuwa hawatakuwa na hofu ya kuichelewesha kwani nani atawafanya nini!Hawahitaji customer care kwa sababu wanabaki kuwa Benki Kuu hata wakiwa na kiburi.

Ni kwanini hasa imekuwa hivyo iwapo NMB inamilikiwa na serikali kwa ubia na wawekezaji?Kwanini serikali haioni usumbufu unaoweza kujitokeza?
 
Watu tumeshapata wasiwasi kuhusu hilo suala, nadhani mfumo mpya unapoanzishwa unaweza leta usumbufu
 
Mimi nimeanza kupata wasiwasi na serekali yetu ya sasa.Kwani kazi ya Benki Kuu ni zipi!kama hata hazina haiwezi kulipa mishahara ya watumishi wa serekali issue ni nini!Nahisi kuna mambo yamefichwa nyuma ya pazia hatujui ila hii ni dalili sio nzuri .Kuna mawili,Hela hakuna sasa wanajaribu kutumia BOT kuhakikisha wanafukia mashimo na soon hela zitachapishwa kuingizwa kwa mzunguko or sasa serekali itakuwa na hela zote wao kuanza kugawa kwa wananchi which is not possible.ILA Soon ,we'll know
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapa itakuwa tunapokea kila trh 31....hahaaaa
Si kila mwezi una tarehe 31,Hata ikiwa ikiwa kila tarehe 31. Usumbufu utakuwa utakuwa ni kwa mwezi wa mwanzo kutokea kuanza kutumika kwa mfumo huu. Baada ya hapo muda utakuwa ni uleule, sawa na unavyopokea kila tarehe 22. Maana toka tarehe 22 hadi 22 nyingine ni sawa na kutoka tarehe 30 hadi 30 nyingine (ya mwezi unaofuatia)
 
Uko sahihi kabisa
 
Mimi hilo halinipi hofu sana, linalonipa hofu kubwa ni suala la kuondolewa salary slip.
 
Ngoja tuingie kwanza then hayo maswali yako yatakuwa na majibu mazuri tu na jinsi ya kuzipata hizo salary slip.
Niko na hofu kwa kuwa kuna muajiri wangu aliwahi kunikata fedha kwa ajili ya mfuko wa hifadhi ya jamii lakini hakuipeleka hivyo kwa kesi kama hiyo stakabadhi ni muhimu sana kwa muajiriwa kuihifadhi.
Sawa tusubiri tuone.
 
Si kila mwezi una tarehe 31,Hata ikiwa ikiwa kila tarehe 31. Usumbufu utakuwa utakuwa ni kwa mwezi wa mwanzo kutokea kuanza kutumika kwa mfumo huu. Baada ya hapo muda utakuwa ni uleule, sawa na unavyopokea kila tarehe 22. Maana toka tarehe 22 hadi 22 nyingine ni sawa na kutoka tarehe 30 hadi 30 nyingine (ya mwezi unaofuatia)
Hata mi nashangaaga wanavyong'ang'ania mpaka tarehe fulani ilihali urefu ndo ule ule! Hata ukipewa tarehe 10 si utasubiri mpaka 10 nyingine ya mwezi mwingine? Ni yale yale yaani
 
Back
Top Bottom