Mishahara hewa yaizundua Serikali

Mishahara hewa yaizundua Serikali

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Mwigulu-Nchemba.jpg

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba


Aziza Masoud,Dar es Salaam

SERIKALI imekabidhi majina ya taasisi na kampuni mbalimbali zilizohusika kutoa mishahara hewa na kuisababishia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha kwa vyombo vya usalama ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.

Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba alisema baada ya kupata taarifa za ubadhilifu huo wizara iliunda timu ambayo ilifanya uchambuzi katika baadhi ya taasisi na kugundua tatizo hilo ambalo lilikuwa linafanywa na viongozi wa makampuni husika.

"Wale waliokuwa wanachukua fedha na kuwalipa watumishi hewa tumeshakabidhi majina yao katika vyombo vya usalama…siwezi kuliongelea kwa undani kwa sababu ya kuogopa kupoteza ushahidi,"alisema Mwigulu. Alisema vyombo vilivyokabidhiwa kazi hiyo ni pamoja na Taasisi ya Kuzuia Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)na jeshi la polisi.

Alisema ili kupambana na ubadhilifu huo, wizara imeagiza taasisi na mashirika yote yanayolipwa na serikali kuhakikisha wafanyakazi wao wana akaunti za benki mbazo zitakuwa zinatumika kuinigiza mishahara moja kwa moja kutoa wizarani tofauti na ilivyokuwa awali ambapo fedha hizo zilikuwa zinakabidhiwa kwa kampuni.

Alisema uchambuzi huo,utasaidia kufuta majina ya malipo kwa watu waliopo katika kampuni na mashirika ambao wamefikisha umri wa kustaafu na badao wanalipwa mshahara na waliokufa. "Kuna ofisi nyingine walikuwa wanachukua pesa mpaka za watu waliofukuzwa,hatuwezi kukubali watu wanajituma wanapokea mishahara midogo wakati tunaendelea kulipa mishahara hewa.

"Tunaendelea kuwabana waajiri kabla ya tarehe kumi kila mwezi wawe wamewasilisha taarifa ya watu waliofanya kazi kwa mwezi huo na wanastahili kulipwa na tunalipa wizara lengo ni tujue hiyo hewa ipo wapi na kuepusha ucheleweshwaji wa mishahara haiwezekani mishahara tuwai kuutoa karibu tarehe 25 alafu watu walipwe mpaka tarehe kumi," alisema Nchemba.

Alisema wizara imeanza kufanya uhakiki wa ndani kwa wafanyakazi wote. Alisema mpango huo, pia utahusisha watendaji wa halmshauri na wilaya ambapo fedha za mishahara na mambo mengine zitakuwa zinawekwa katika tovuti ya wizara kabla hazijapaelekwa katika ofisi za mikoa kwa ajili ya malipo.

"Kwa sasa ofisi za wakuu wa mikoa zinagawa fedha kwa wilayani, lakini kuna malalamiko mengi watu wanapata mishahara midogo kwa sababu fedha zinazopatikana haziwatoshi, kwa sasa tutakuwa tunaweka cheki za halmshauri zote katika tovuti ya wizara ili kila halmshauri ijue imepata shilingi ngapi kupunguza ubadhilifu mikoani" alisema Nchemba.

CHANZO: Mtanzania
 
Unakumbuka blanketi kumepambazuka
 
Huyu mwigulu ni mtafuta sifa tu hana lolote anachosema hao wapeleke accounts zao hazina kwani hawawezi pia kupeleka accounts hewa? Kuna Freelancer kibao wanalazimisha kufungua accounts kwenye bank zao kwahiyo ni possible kwa hao wapigaji kuwafungulia accounts wote hewa na kuendelea kupiga pesa,wewe mwigulu kama mmegundua wizi huo wa zaidi ya 40b kwa mishahara hewa basi hao wezi lazima wakamatwe wafilisiwe na wafungwe hatutaki porojo mara sijui nimepeleka takukuru oh nimepeleka polisi na bla bla kibao mbona yule aliyekwepa kodi zaidi ya 7b ulimuweka hewani?

Cc: Tema Mate
 
Last edited by a moderator:
Unakumbuka blanketi kumepambazuka

Huu mwingine ujinga ulitaka afanye nini kwani ameanza kuwa waziri wa fedha lini msifanye kila kitu siasa wehu nyie mtu akifanya kizuri kero mnataka nini sasa.
 
Huyu mwigulu ni mtafuta sifa tu hana lolote anachosema hao wapeleke accounts zao hazina kwani hawawezi pia kupeleka accounts hewa? Kuna Freelancer kibao wanalazimisha kufungua accounts kwenye bank zao kwahiyo ni possible kwa hao wapigaji kuwafungulia accounts wote hewa na kuendelea kupiga pesa,wewe mwigulu kama mmegundua wizi huo wa zaidi ya 40b kwa mishahara hewa basi hao wezi lazima wakamatwe wafilisiwe na wafungwe hatutaki porojo mara sijui nimepeleka takukuru oh nimepeleka polisi na bla bla kibao mbona yule aliyekwepa kodi zaidi ya 7b ulimuweka hewani?

Cc: Tema Mate

kwa akili yako unadhani akipelekewa acount ndiyo ataishia hapo tatizo hujamsikiliza unakukurupuka bawacha bana.
 
Huyu naye anatafuta Uwaziri Kamili, hakuna lolote, watendaji wengi wanabugia mishahala kwa kushirikiana kwa karibu na wizara yake.
 
Ndio sababu nchi za wenzetu uwezi kukuta auditor wa serikari ni mmoja, kila kitengo cha serikari kina external auditors wake locally na wao wanaripoti kwa auditor wakuu wa kitengo wa hiyo sector, iwe ni afya, serikari za mitaa, taasisi za serikari etc, na kama ni ukaguzi wa afya unaanzia kwenye zahanati mpaka wizarani jinsi tender zinavyotoka na ndivyo mapendekezo bora yanapoweza kuja kuzuia mirija, kuboresha usimamizi/accountability, kuweza boresha sera na kuakikisha hela ya serikari inaenda mbali kwenye kuwafikia walengwa.

Isitoshe ingawa kuna mkaguzi maalum locally lakini yeyote kati ya wakaguzi wa kitengo anaweza kuzuka anytime kukagua hili kuhakiki kazi ya wengine na kila mara serikari inapewa namna za kuzuia fraudulent acts. Kwa sasa it is very hard to monitor things from central government hivi CAG akague kila sehemu how is that possible ndio maana miaka yote kumekuwa na mishahara hewa naamini this is just a start, maana mafuta, gharama zingine zikipekuliwa kutakuwa na yale yale si hata wizara iliposema i-hakiki madeni ya tender wakakuta badala ya trillioni na zaidi wanadaiwa billion 100 tu.

CAG is a weak institute kutokana na pesa zote hizi zinaozoonekana kupotea kila mwaka kuna sababu muhimu sana ya kuivunja na kuunda sectorial auditing bodies expensive but the benefits outweighs government losses in policy deliverance and getting value for their money.
 
Wahaya wanasema "Better late than never"


Usitegemee mabadiliko, tumetoka tunasikia zamani sana habari za mishahara hewa, naye huyo akiwa kwenye chama hichohicho, kwanini hakupiga kelele bungeni na kupendekeza waliohusika wachukuliwe hatua kali ili kukomesha tabia hiyo, kumbuka kuna wabunge walilalamika kuwa wapo kwenye pay roll za MUCE na OUT, wakati hawajawahi hata kutuma applications za kutaka kazi huko, je, waliohusika wapo wapi?
 
Huu mwingine ujinga ulitaka afanye nini kwani ameanza kuwa waziri wa fedha lini msifanye kila kitu siasa wehu nyie mtu akifanya kizuri kero mnataka nini sasa.

Jenga hoja usikimbilie kujibu kwa lugha mbovu, anyway, pamoja na mtazamo wako usitegemee mabadiliko, tumetoka tunasikia zamani sana habari za mishahara hewa, naye huyohuyo akiwa kwenye chama tawala, kwanini hakupiga kelele bungeni na kupendekeza waliohusika wachukuliwe hatua kali ili kukomesha tabia hiyo, kumbuka kuna wabunge walilalamika kuwa wapo kwenye pay roll za MUCE na OUT, wakati hawajawahi hata kutuma applications za kutaka kazi huko, je, waliohusika wapo wapi?
 
Ana wakabidhi wa tumishi wa umma kwenye vyombo vya usalama kwa kuwa hakuna wakuwatetea mbona mafisadi wanaofisadi nchi mabilioni na mabilioni hakabidhi majina kwenye vyambo vya usalama ili watendewe kama iwapasavyo au mafisadi wanalindwa kwa ukuta wazege ambao Mwigulu hawezi kuuvunja?.
 
Hivi mishara hewa inatoka wapi naomba mnijuze wananzuon? Mimi nashangaa kuona gvt inasema imekoa pesa kwa kupitia hazina. Nijuze?
 
Tatizo hapa si kukabidhi majina kwa vyombo vya usalama,tatizo ni kuwa madili ya mishahara hewa yanapigwa na baadhi ya wakurugenzi na watumishi kutoka hapohapo wizarani kwake kwa kushirikiana na watumishi wa mikoa na halmashauri mbalimbali mikoani,hivyo kazi bado ni pevu zaidi zaidi hao watumishi wa hapo hazina wanawamghiribu tu Nchemba na Nkuya.
 



Lini hii Serikali iliyojaa mafisadi itazinduliwa na wizi wa bilioni 200 za Escrow, na mikataba feki ya madini na gesi inayoikosesha Serikali mapesa chungu nzima? Ule mkataba na kampuni ya Saitoil toka Norway utaikosesha Serikali zaidi ya $55 billion ni lini hii Serikali fisadi ya mafisiem itazinduka?
 
Wahaya wanasema "Better late than never"

Kumbe huu msemo upo kwa Wahaya na Waingereza pia?!

Tukiachana na haya uko sahihi kabisa kwamba tusiache kuchukua hatua kurekebisha jambo hata kama tulishachelewa! Afadhali faida kidogo kuliko kukosa kabisa...!
 
kuna maelezo mengi humu inaonyesha hajui anachosema,hususan pesa inayopitia mikoani kwenda wilayani.sijamuelewa anaongelea pesa ipi
 
Wizara ya Fedha imeziagiza taasisi zilizokabidhiwa jukumu la kuchunguza wakuu wa mashirika na taasisi za umma waliojihusisha katika kughushi malipo hewa ya wafanyakazi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 40 kila mwezi wafichuliwe.

Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mungulu Nchemba, akisema wakuu hao pamoja na waajiri wametumia mwanya wa wafanyakazi wao katika ubadhirifu wa fedha kwa maslahi yao binafsi.

Kadhalika, wizara inawataka maafisa utumishi na waajiri kuhakiki upya taarifa wanazoweka katika mfumo ni sahihi ili watumishi wao wawekewe malipo yao katika akaunti kwa wakati mwafaka.

“Zoezi hili ni endelevu, hivyo tumebaini tatizo na tunatafuta njia ya kulimaliza na hii tuliyowaagiza waajiri itakuwa njia ya kutokea, hivyo tutalinganisha taarifa zao na muda wa watumishi wao tuone tatizo lilikuwa wapi,” alisema.

Pia, alisema hakuna sababu ya wizara kuendelea kulipa malipo hewa wakati kuna kundi la wafanyakazi katika taasisi na mashirika hayo, ambao kazi yao ni kuhakiki mafaili na wanalipwa mishahara mikubwa huku wale wanaojituma wakiendelea kujaziwa mishahara hewa.

Aliwaagiza waajiri na maafisa hao kufikisha orodha ya majina ya watumishi wakiambatanisha na taarifa sahihi ya mishahara tarehe za mwanzo za kila mwezi zifanyiwe kazi mapema ili kuwepo na uwajibikaji katika sehemu za kazi.

Alisema fedha za miradi katika taasisi hizo zitatolewa kulingana na mchanganuo wa malipo yao, “Hatuwezi kuendelea kutoa malipo hewa kinyemela tena, hivyo wataalamu wetu watashirikiana na wakuu hao wa maradi kuangalia kama unakidhi kutekelezewa,” alisema.


CHANZO:
NIPASHE
 
Mwigulu usilete comedy fanya kazi hatutaki porojo mbonqa yule mwenye kiwanda mlimkata? Iweje hawa ulete porojo?

Cc: Tema Mate
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom