Yohana 4:23
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Yohana 15:1
Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
Mathayo 26:29
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Binafsi napenda sana "mafundisho ya Mlimani na mafundisho ya Last Supper"
Mathayo 5: 13-14 Ninyi ni chumvi ya Dunia, lakini chumvi ikiwa imeharibikiwa itatiwa Nini hata ikolee? Haifai Tena kabisa ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Nini ni nuru ya Ulimwengu, mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya Mlima. Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya pishi Bali juu ya kiango nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate kuyaona matendo yenu mema na wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.