Misaada ya lwakatale yakataliwa bukoba

gambalakobe

Member
Jul 1, 2015
55
73
Baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali.

Mbunge huyo mwishoni mwa wiki alikuwa akisambaza vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati, lakini wasimamizi walikataa kuvipokea, huku wengine wakikimbia wakidai walipewa maelekezo na viongozi wao kutovipokea.

source.Mwananchi communication Ltd.
 
huu ndio ujinga mkubwa sana wa watu kuzingatia chama kuliko maendeleo. sisi wapinzani tumeshakubali kuwa magufuli ni rais wetu na tupo tayari kushirikiana, anapotokea mtu mlevi fulani hivi, amekula malimao fulani hivi halafu anajifanya anataka kutugawa tena hata kwenye masuala ya msingi kama hayo, huyo atakuwa adui wa tz namba moja. hivi siasa tangu lini ilishawahi kuleta maendeleo? mtu hataki kupokea msaada toka mtu wa chadema kwasababu tu mtu wa ccm amemwamrisha asipokee? ati pengine cdm isijeonekana inafanya kazi? ujinga huu.waandishi wa habari ndio wanataka kwenda huko wakawauliza, na lwakatale hakutakiwa aende peke yake, ukiona unaenda kufanya jambo kama hili nenda na waandishi wa habari ili wakikataa habari irushwe kwamba hospitali fulani wamekataa na watz wote wajue wapi kuna watu wa akili za kijinga naman hiyo.
 
Dah! Kama ni kweli hili ni tatizo la serikali yetu mpya. Ina maana hata wabunge wa ccm wasichangie hizo huduma za afya? Au kwa sababu tu ni mpinzani?
 
Back
Top Bottom