Misaada ninayompa inamkosesha raha na kumkondesha

msemakweli2

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
1,627
Reaction score
1,886
Wadau mimi nilizaliwa nje ya ndoa miaka hiyo,baba yangu mzazi na mama yangu wa kambo kwa pamoja hawakupenda hata kuniona,nimelelewa na mama mpk nilipopata akili,nilikuwa nikinyanyua simu kumpigia baba hata kumsalimia tu anafoka sana na wakati mwingine kunikatia simu kabisa,nilisononeka lakini mwisho wasiku nikayazoea maisha hayo.

Niliendele kupigana huku na huko nikafanikiwa kumaliza hadi chuo kikuu, nikapata ajira ya kudumu,baada ya umri wa mzee na mkewe kusogea nimekuwa nikifululiza misaada ya namna tofauti tofauti bila kinyongo chochote,lakini naona jinsi ninavyotoa ndivyo wanavyokosa amani kwakuwa nadhani wanakumbuka mabaya waliyonifanyia,mimi nimeziba masikio nazidi kumimina nilichonacho tu najua mungu alikuwa na kusudio lake kuniongoza mpaka kufika hapa nilipo na pia mungu pekee ndiye mgawa riziki.
 
Kama vipi kaa nae na muongee ile kiume kua hauna kinyongo maana kwa kawaida lazima ajishtukie
 
Hi story yanikumbusha mbali dada mmoja alilelewa na mama yake mzazi na baba wa kambo lkn mama ndo alikuwa anamtesa sana binti yake alimtreat km mfanyakazi hakumpenda kabisa mpaka bint akakuwa mkubwa mateso ya mama yake yalimfanya aamue kuolewa alipoolewa kwenyewe kukutana na majanga kurudu kwao hawezi kwa mume nako full mateso yaana hadi anajiona km ana mkosi maana hajawahi enjoy life ila mazaake hakupenda aolewe ili aenddlee kumtumia km housegirl maana saa zingine anamshawishi arudi nyumbani aachane na mume ila karma km ipo itampata huyo mama
 
najua mungu alikuwa na kusudio lake kuniongoza mpaka kufika hapa nilipo na pia mungu pekee ndiye mgawa riziki.
Kama vipi kaa nae na muongee ile kiume kua hauna kinyongo maana kwa kawaida lazima ajishtukie.

Samehe saba mara sabini. Ndivyo maneno ya Mungu yasemavyo. na kama unafahamu kwamba Mungu ndiye mgawa riziki, tambua kwamba ili ubarikiwe zaidi, kusamehe na kuachilia pia ni kigezo.
kaa nao muongee na uwatamkie kuwa umewasamehe na wao watambue wazi kuwa ni kweli umewasamehe, usiwe na kinyogo tena na usiwaambie watu tena hayo yaliyotokea. huo ndo msamaha wa kweli. kila la heri
 
Wadau mimi nilizaliwa nje ya ndoa miaka hiyo,baba yangu mzazi na mama yangu wa kambo kwa pamoja hawakupenda hata kuniona,nimelelewa na mama mpk nilipopata akili,nilikuwa nikinyanyua simu kumpigia baba hata kumsalimia tu anafoka sana na wakati mwingine kunikatia simu kabisa,nilisononeka lakini mwisho wasiku nikayazoea maisha hayo.

Niliendele kupigana huku na huko nikafanikiwa kumaliza hadi chuo kikuu, nikapata ajira ya kudumu,baada ya umri wa mzee na mkewe kusogea nimekuwa nikifululiza misaada ya namna tofauti tofauti bila kinyongo chochote,lakini naona jinsi ninavyotoa ndivyo wanavyokosa amani kwakuwa nadhani wanakumbuka mabaya waliyonifanyia,mimi nimeziba masikio nazidi kumimina nilichonacho tu najua mungu alikuwa na kusudio lake kuniongoza mpaka kufika hapa nilipo na pia mungu pekee ndiye mgawa riziki.
Mbona ujamalizia stor Mkuu au ndo speed ya mwendo kas [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hi story yanikumbusha mbali dada mmoja alilelewa na mama yake mzazi na baba wa kambo lkn mama ndo alikuwa anamtesa sana binti yake alimtreat km mfanyakazi hakumpenda kabisa mpaka bint akakuwa mkubwa mateso ya mama yake yalimfanya aamue kuolewa alipoolewa kwenyewe kukutana na majanga kurudu kwao hawezi kwa mume nako full mateso yaana hadi anajiona km ana mkosi maana hajawahi enjoy life ila mazaake hakupenda aolewe ili aenddlee kumtumia km housegirl maana saa zingine anamshawishi arudi nyumbani aachane na mume ila karma km ipo itampata huyo mama
huyo mama anamchukia jamaa alomzalisha..sasa kwa kuwa jamaa hawezi kumfanyia ubaya ndo anamalizia kwa mwanae
 
Back
Top Bottom