Misa wangu

Misa wangu

Mr Eggo

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Posts
2,027
Reaction score
1,052
Nimatumaini kila mmoja anaendelea vyema, ambao hawako sawa Allah awafanyie wepesi kwenye magumu yao.

Leo nimekumbuka kisa kimoja nikiwa O-Level nakwasababu niko safarini sina cha maana cha kufanya nimeona niwachangamshe.

Tupo kidato cha tatu miongoni mwa kidato cha kwanza alikua dada mmoja anaitwa Hamisa, alikua pisi moja kali mnoooo. Alikua na umbo lililoshiba, mweupe, tabasamu lake ni hisani, msafi.

Kimsingi kila mmoja angependa kuwa na huyu mtoto, na kila mmoja alikua anamtongoza kwa muda wake isipokuwa hakuna ambaye alionekana kuuteka moyo wa binti.

Upande wapili kuna mimi baharia, kwanza shule nilikua sipendi na nlikua nakaa day. Naweza kwenda shule angalau siku 2-3 kwa wiki ukiondoa j3 (nilikua naamini hii siku mwalimu wa zamu anakuwa na wenge maana ndiyo mwanzo wa wiki, kwaiyo kuepusha vurugu nikawa siendi kabisa labda kuwe na tukio la lazima kama mtihani).

Sasa miongoni mwa waliokua wanamvizia ni pamoja na mimi, kuna wakati nilikuwa nimetumia barua ila sikutaka ajue ni mimi. Nilikua naonyesha dalili zote za kumtaka isipokuwa kumwambia sikuwahi.

Nikamaliza shule, nikawa mji mwingine ila mara moja moja bado nikawa namfata kwao kumsalimia.

Tupeleke mbele maisha yameenda miaka yakutosha imepita, ni mwaka jana nikapata mawasiliano naye. Kwanza alifurahi kunipata halafu akaniambia mimi alikuwa ananipenda sana, alikuwa akisubiri mimi nifunguke, na ile barua nilimtumia alipata hisia ni yangu (yaani alimaanisha aliamini ni yangu ingawa hakuwa na uhakika).

Hii taarifa kwa kweli iliuvunja moyo wangu vipande vipande maana kumbe ningekuwa na ujasiri huenda sasa hivi ningekua na mwanamke ambaye alinipenda tangu enzi (kwa dunia ya sasa hivi tunahitaji sana wanawake wa aina hii, hawa wakuokotana mjini wote mnajua sehem kubwa ni tatizo). Nilikuwa na nafasi moja ya kuwa na mwanamke wa ndoto yangu, nikaleta uboya.

Ameolewa na watoto watatu na bado ananiona mimi kama mpenzi wake wa kwanza na wa milele.

Wakuu kama kuna kosa nimewahi kufanya ni hii ya kutokujiongeza kwa huyu mrembo.

Funzo la funzo la hadithi, tusiwe domo zege, inaweza kutukosesha bahati za maisha.
 
Ulimtamani kwa shape lake Enzo hizo,Toto white
Vipi sasa yukoje?
 
Siku zote nasema kama umemuelewa mtu omba namba akikunyima shauri zake huna cha kupoteza.

Ukitaka kunyanduana na mtu mwambie akikunyima shauri zake huna cha kupoteza

Tupunguze malalamiko na majuto siku za mbele.
 
Mapenzi ya kisekondari mengi yanaishia njiani hata kama true love ipo.
Ile mnamaliza shule kila mtu anaenda kwao halafu mnakuja kwenda shule/vyuo tofauti mnakutana na watu wengine tofauti.
Mnajikuta mnaachana automatically.
magombe junior
 
Hii ipo sanaaa,ila kama wangejua wangekomaa tu watoboe maana kua na mtu ambae mlikua na pure love nirahisi sana rship kumove smooth
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom