Mirathi itanitoa roho, naombeni ushauri la kufanya

Mirathi itanitoa roho, naombeni ushauri la kufanya

Strawberry

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
274
Reaction score
108
Habari wana Jukwaa.Mimi ni mwanamke wa umri wa miaka 32.nilifiwa na mme wangu sasa ni miezi sita toka afariki.
Alifia hapa DSM na kuzikwa kijijini kwao huko mkoa flani sitaki kuutaja jina kwa kuhofia usalama wangu.
Aliumwa nikauguza na akanifia mie mwenyewe.Tumejenga Nyumba moja na tuna shamba.Tulifunga ndoa ya kanisani.

Tatizo linakuja kwenye kufungua mirathi ya mme wangu.Maana alikuwa mtumishi wa serikalini.
Shemeji zangu wanataka mirathi tufungulie kijijini kwao.na mie nataka tufungulie hapa DSM maana ndipo tunapoishi na kujenga tumejenga hapa na kufia kafia hapa pia cheti cha kifo kinaonesha kafia hapa DSM.

Hawa shemeji zangu hawana nia njema na mie maana tayari wameshaanza chokochoko za kutaka kunitoa kwenye nyumba niliyojenga na marehemu mme wangu.Kwa kisingizio ipangishwe ili watoto wapate ada ya shule.
Tulifanikiwa kukaa kikao cha kuteua misimamizi wa mirathi mwaka jana Dec na wakaniteua mie nikisaidiwa na shemeji yangu.ila kwa ugomvi mkubwa sana walitaka wao wawe wasimamizi.
Mwisho wasiku tukaafikiana na wao kazikatalia zile karatasi za kuteua msimamizi wa mirathi wakazipeleka weyewe mahakamani bila mimi kunishirikisha.Hakimu akawarudisha akaaambia waje adi mie niwepo.

Basi wapendwa naomba msaada kwa yeyote anae jua wapi nianzie ili niweze kufanikisha kufungua mirathi huku hata kama ni shirika au taasisi yeyote inayoweza kunisimamia kwa hilo.
 
Pole kwakuondokewa na mumeo mungu atakuongoza na kusimamia haki yako
 
Pole kwa msiba wa mume wako na pia pole kwa masaibu ya mashemeji kwa ushauri wangu tafuta ofisi za WLAC au TAWLA hapo Dar watakusaidia naamini haki ya mwenye haki itakaa juu yake . hawajui sheria ya mirathi ndiyo maana wanakusumbua ukifika hapo nlipokuelekeza watakusaidia bure maana wana legal officer wenye uzoefu wa mahakama za zote
 
Pole mumy kwa kufiwa na mmeo Mungu atakusimamia katika kutafuta haki zako. Mali ni ya watoto hao ndugu ni waroho tu.
 
Pole kwa msiba wa mume wako na pia pole kwa masaibu ya mashemeji kwa ushauri wangu tafuta ofisi za WLAC au TAWLA hapo Dar watakusaidia naamini haki ya mwenye haki itakaa juu yake . hawajui sheria ya mirathi ndiyo maana wanakusumbua ukifika hapo nlipokuelekeza watakusaidia bure maana wana legal officer wenye uzoefu wa mahakama za zote

Fuata ushauri huu utafanikiwa.
Hapo wote hamjui sheria ndo maana mnasumbuana
coz kisheria najua ndugu hawana lao hapo mali ni ya watt na mke full stop!

Cc wanasheria mlioko humu jamvini au wanaelewa
 
Pole sana.

Msimamizi wa mirathi aliyechaguliwa kwa wosia au kikao cha wana-ndugu ndiye(pekee) mwenye mamlaka kisheria kusimamia mali za marehemu bila shuruti wala bughudha toka kwa yeyote ambaye hakupendekezwa na kikao kuwa msimamizi.

Hivyo, nenda kafungue shauri la mirathi mahakamani-kwani mahakama hutoa nafasi ya wote wenye mapingamizi kujitokeza. Ndipo sababu za shemeji zako(wanaokupinga/wenye kuleta zogo) zitaamuliwa mahakamani na mahakama itathibitisha uteuzi wako na kukupa nguvu kisheria kuanza usimamizi pasipo usumbufu.

kila heri.
 
pole sana
kuna rafiki yangu alipitia mkasa kama wako
lakini mwishoe alifanikiwa..kua na mwanasheria wako atakusaidia
 
Natumaini umeshafungua hiyo mirathi ... bandugu inakuwaje wanandugu kutolea mimacho mali ya marehemu? Labda itokee mfiwa ni mfujaji wa msli lakini vinginevyo haiingii akilini!
 
shemeji pole sana.....usiwe na hofu, wote waliotangulia wamekushauri vema. hutopoteza chochote, vyote ni mali yako, wapangishe nyumba???yaoooo???, kwani uliwaambia watoto hawana ada......pu.....fuu zao..... simamia mali zetu kwa faida ya watoto wako, na wewe usibweteke......jishughulishe....
 
komaa nao hao wajinga usikubali, watu wengine bana kujidhalilisha tu, mali achume mwingine wengine watolee macho..

tafuta mwanasheria au nenda WILAC au LHRC pale mwananyamala au Tanganyika Law Society watakusaidia..usichelewe sana uende watakupa maelekezo na pia wanaweza kukusaidia cha kufanya..

kwenye hiyo nyumba usiondoke hata kwa greda, kaa hapo hapo na wanao..na pia document zote za nyumba, gari au shamba ficha mbali hata ikibidi usiweke nyumbani kwako tafuta sehemu salama uziweke, zinaweza kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha ukashangaa nyumba imepigwa mnada wewe ukiwa ndani..
usikubali kusainishwa chochote hadi mbele ya mwanasheria wako na usiwa entartain sana hao wanweza kukurestisha in piece uwaache watoto full yatima ili wafaidi hizo mali..
kwa kweli mtanisamehe sana wandugu ila kwa kweli ndugu za mume? si watu kabisa..badala ya kusaidia yatima wao wanawazia mali za marehemu kaka yao..
 
kuna rafiki yangu mmoja alifiwa na baba yake akapigiwa simu tukamsindikiza kwao, tulipofika tukamkuta mama yao analia, huyo rafiki yangu akamwambia mama hebu noo chumbani mara moja, wakaingia..akamwambia mama yake kabla ya kulia na kukusanya watu wengi hapa nyumbani hebu leta kwanza hati zote za nyumba zetu, hati za mashamba, document za biashara, kadi za magari n.k, tukae nazo na kuziweka sehemu ya salama..
yule rafiki yangu akaniita na kuniomba nimuhifadhie zile document zoooote hadi msiba utakapoisha ndio atazichukua lakni hakutaka zikae pale ndani wakati wa msiba mana hawana imani na ndugu za baba yao (yaani baba wadogo/wakubwa na mashangazi)..
nilishangaa sana lkn kweli yule rafiki yangu alimsaidia sana mama yake kwani mashangazi walipekua sana ile nyumba utafikiri kuna kitu wanatafuta na baada ya hapo wakati wa usimamizi ulizuka mgogoro mkubwa sana, sema tu kilichosaidia baba yao aliandika usia ambao aliwapa watoto wake kila kitu na ndugu zake hawakupewa chochote kitu ambacho kilisababisha watoto wa yule mzee kutengwa kabisa na ndugu wa baba yao..
nikasema hizi mali hizi kweli zitatoa watu roho
 
law suites should follow wasikubabaishe hayo ni matatizo ya familia nyingi za kiafrika lakini sheria ndo msumeno
 
hivi kweli unagombeaje jasho la mwenzio aliyekufa na kaacha urithi yaani watoto,... pole sana mpenzi me sina namna ya kukusaidia
 
Nishajua marehem mume wako mpendwa alitoka mkoa gani,mana wanajulikana kwa tabia hizo,kwao wanasema vita ni vita mura,komaa na utashinda tu.
 
pole sana hakikisha unasimama KIDETE
mpaka upate haki zako zote usiwachekee kabisa hao ndugu wa mume potelea mbali hata wakikutenga mungu atakuwa upande wako siku zote
 
kuna rafiki yangu mmoja alifiwa na baba yake akapigiwa simu tukamsindikiza kwao, tulipofika tukamkuta mama yao analia, huyo rafiki yangu akamwambia mama hebu noo chumbani mara moja, wakaingia..akamwambia mama yake kabla ya kulia na kukusanya watu wengi hapa nyumbani hebu leta kwanza hati zote za nyumba zetu, hati za mashamba, document za biashara, kadi za magari n.k, tukae nazo na kuziweka sehemu ya salama..
yule rafiki yangu akaniita na kuniomba nimuhifadhie zile document zoooote hadi msiba utakapoisha ndio atazichukua lakni hakutaka zikae pale ndani wakati wa msiba mana hawana imani na ndugu za baba yao (yaani baba wadogo/wakubwa na mashangazi)..
nilishangaa sana lkn kweli yule rafiki yangu alimsaidia sana mama yake kwani mashangazi walipekua sana ile nyumba utafikiri kuna kitu wanatafuta na baada ya hapo wakati wa usimamizi ulizuka mgogoro mkubwa sana, sema tu kilichosaidia baba yao aliandika usia ambao aliwapa watoto wake kila kitu na ndugu zake hawakupewa chochote kitu ambacho kilisababisha watoto wa yule mzee kutengwa kabisa na ndugu wa baba yao..
nikasema hizi mali hizi kweli zitatoa watu roho

Tutatoana roho yarabiiiii kwa mali alizo acha baba
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom