Miradi ya Umeme Mwanza-Kwa Nini Miradi Mingi Inahamishwa Kinyemela?

chibingo

Member
Feb 7, 2009
46
8
Wana JF

Kwenye Bunge la Mwaka jana Mh. Anna Kilango Malecela alilalamika sana kuhusu miradi ya umeme vijijini (REA) kupelekwa Sengerema wakati kuna baadhi ya wilaya hazina umeme! Kinachoendelea hivi sasa kuna mradi wa MCC umeanzia tena Sengerema na baadae ndio makandarasi hao ndio wahamie Mwanza, ambapo dhana inayonekana kwa watu wasio wa Sengerema kuwa ni upendeleo au kampeni za chinichini. Hoja yangu ni kwa nini huu mradi wa MCC usianzie Mwanza kwenye sehemu ambazo zimejengwa muda mrefu na zimesubiri umeme huu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa!!! Sikatai wananchi wa Sengerema kupata umeme kwani ni haki yao ya msingi kuwa na umeme, lakini kwa hili wizara na Tanesco walitakiwa kufanya checks and balance na kuangalia ni sehemu gani ina tija hasa kwa Tanesco ambayo inahitaji fedha zaidi kujiendesha kibiashara. Na hili la kuhamisha miradi ya umeme kwenda sehemu nyingine kiupendeleo hapa Mwanza sio geni kwani mradi wa umeme wa Nyamuhongolo umefanikishwa na kigogo mmoja wa Tanesco mkoani Mwanza anayeishi huko, mradi huo ulikuwa uende Buswelu. Wizara/Tanesco jaribuni kuangalia sehemu kama Buswelu, Nyegezi, Bugarika, Luchelele etc wananchi wanaoishi huko wana shida sana ya umeme!
 
Infact Ngereja anafanya kila liwezekanalo ashawishi wananchi wa Sengerema,
Ni kweli ule mradi nguzo na nyaya zimeshawekwa tokea Sengerema hadi Kamanga (Est 34Km).

Nashukuru umeyaona maeneo kama ya luchelele ingawa tayari ile Luchelele ya shadi (Lavena Beach)wameshapeleka. Luchelele yenyewe kabisa haina umeme na pia kuna chuo cha ufundi. Huko ndiko kwenye mgogoro kumbuka lile kundi la matapeli wa viwanja lilipima na kutaka kufukuza wananchi bila kuwalipa.

Ule mradi wa upimaji umekwamisha watu kujenga kwa sababu toka 2009 wamepima lakini hadi leo hawajagawa viwanja, huu ni upuuzi.

Maeneo mengine yanayohitaji umeme ni pamoja na Ilemela, Hata Mkolani nyuma ya makao makuu yao ya Nyamagana(mpya) kuna nyumba nyingi za kisasa watu hawana umeme pia kuna shule ijulikanayo kama Buhongwa Centrla Secondary School.

Ndg yangu tuko ktk msafara unaoongozwa na majuha, hilo fahamu.
 
Back
Top Bottom