Miradi ya NHC inafanyika kwa upendeleo

Miradi ya NHC inafanyika kwa upendeleo

yohana charles

Senior Member
Joined
Mar 21, 2013
Posts
134
Reaction score
10
NHC ni shirika la kitaifa,inakuwaje mkoa au mji mmoja unakuwa na miradi ya mabilioni ya shilingi inayoendelea halafu miji mingine haina hata mradi mmoja?

Kuna maeneo kuna nyumba za NHC tena unakuta ni moja tu lakini inachukua miaka kukamilika wakati huko kwingine kunajengwa nyumba nyingi tena kwa muda mfupi tu.

Jamani kila mji/mkoa wanahitaji maendeleo.Fanyeni usawa katika kugawa hiyo miradi yenu,acheni kupendelea.!
 
Siku zote mie naàmini mipango ya maendeleo ya Tz ni ya kibaguzi sana,kuna baadhi ya maeneo yanabaguliwa sana tena bila kificho huku maeneo mengine ya nchi moja yakipewa supoti kubwa sana ...Hii hari ikiachwa ikaendelea hivi ipo siku wahusika wataamua hatma yao
 
Mm nahisi hawapendelei ila wanaangalia pale penye mzunguko wa pesa na watu we ye uwezo Wa kununua hizo nyumba.
 
NHC ni shirika la kitaifa,inakuwaje mkoa au mji mmoja unakuwa na miradi ya mabilioni ya shilingi inayoendelea halafu miji mingine haina hata mradi mmoja?

Kuna maeneo kuna nyumba za NHC tena unakuta ni moja tu lakini inachukua miaka kukamilika wakati huko kwingine kunajengwa nyumba nyingi tena kwa muda mfupi tu.

Jamani kila mji/mkoa wanahitaji maendeleo.Fanyeni usawa katika kugawa hiyo miradi yenu,acheni kupendelea.!

Umeghusa penyewe mkuu.Hii miradi inafanyıka kwa mbinu flani za kiushawishi.Kuna maeneo yanakuwa ya mwisho kwa kıla mradi wa serikalı.
 
kama nyumba zilizojengwa chlinze hii haiko nhc ni mashirika mengi wanafanya hivyo baadae utaina viongozi wao wanaenda kugombea ubunge huku wakijinadi kuwa wamefanya hiki au kile kwa kutumia pesa za umma
 
Mm nahisi hawapendelei ila wanaangalia pale penye mzunguko wa pesa na watu we ye uwezo Wa kununua hizo nyumba.

Sio sahihi mkuu!Kama zimelenga hasa watumishi wa chini na kati, hawa wapo nchi nzima.Hata hvyo mzunguko wa hela popote unaletwa na uwepo miradi ya kimaendeleo.Makazi bora yanachochea kuchangamka kwa uchumi.
 
Kwanza zao nyingi wanauzia raia wa kigeni tu hasa wahindi chek pale upanga
 
Sio sahihi mkuu!Kama zimelenga hasa watumishi wa chini na kati, hawa wapo nchi nzima.Hata hvyo mzunguko wa hela popote unaletwa na uwepo miradi ya kimaendeleo.Makazi bora yanachochea kuchangamka kwa uchumi.
Nyumba vyumba vitatu wanauza more than 45 million,alafu eti ni za bei nafuu kwa mfanyakazi wa hali ya chini
 
Sio sahihi mkuu!Kama zimelenga hasa watumishi wa chini na kati, hawa wapo nchi nzima.Hata hvyo mzunguko wa hela popote unaletwa na uwepo miradi ya kimaendeleo.Makazi bora yanachochea kuchangamka kwa uchumi.
Hiyo miradi inatolewa kwa kuangalia ni kiongozi gani mkuu yuko pale
 
IJENGE nyumba harafu iuze??? wizi mtupu kwani wananachi hawawezi kukopa wakajenga wenyewe??? hiyo ya kuwajengea inatoka wapi na kwa gharama ya nani??? wizi mtupu, Serikali ilipaswa kuandaa sera bora ya nyumba na vifaa vya ujenzi basi wananchi wakafaidika na sera za viwanja bei nafuu, vifaaa vya ujenzi bei nafuu, injinia ujenzi wasomeshwe kibao ili watoe utalaam kwa bei nafuu, hiyo ndo kazi ya serikali sio kujifanya inajenga nyumba kwa taifa zima kumbe ni kupiga cha jUUU KOMENI WEZI CCM
 
Mm nahisi hawapendelei ila wanaangalia pale penye mzunguko wa pesa na watu we ye uwezo Wa kununua hizo nyumba.

Mambo ya msingi kuwa mwerevu,sasa hiyo iliyo na mzunguko Wa pesa huo mzunguko umejitengeneza? hizo taasisi zilizoko zilijijenga? na haya maeneo unayodai hayana mzunguko Wa pesa unataka nani akatengeneza huo mzunguko ama hizo taasisi za kuchochea mzunguko zitoke wappi kama mipango yenyewe ndo hii? najua hautaweza kukubali kwa sababu zako binafsi lakini ilo haliwazuii hawa watanzania wenzetu kupaza sauti zao na kama viongozi wataendelea kuwa na hoja kama zako katika kugawa keki ya Tz IPO siku hawa watu watachukua hatua za wazi
 
Sio sahihi mkuu!Kama zimelenga hasa watumishi wa chini na kati, hawa wapo nchi nzima.Hata hvyo mzunguko wa hela popote unaletwa na uwepo miradi ya kimaendeleo.Makazi bora yanachochea kuchangamka kwa uchumi.

Hawa jamaa wanaangalia faida. Tunachotakiwa kudai ni shirika hili lirudishwe kwa Watanzania kwa ajili ya kutoa huduma ya makazi badala kuendelea kulifanya ni kampuni ya kibiashara inayolenga kutengeneza faida.
 
Mnalalamika tu bila ya kutoa mifano wapi pameachwa na wapi wamependelewa.Huyo alietaja chalinze kagusa tu kakikimbia.Vijumba vya chalinze vilijengwa zaidi ya miaka 10 iliopita na ilikua mahsusi kwa wafanyakazi wa serikali pale kama,TRA,MIZANI,TANESCO,NSSF,POLISI NA USALAMA WA TAIFA.Tajeni miji mingine ili tuwahukumu NHC.
 
Wanaangalia faida.. huko bara kuna mtu atanunua nyumba kwa milioni 300!! wacha wakomae huku kwa wezi wa EPA na ESCROW
 
Jamaa wana kanda zao, kuna Jiji moja linanyanyapaliwa sana ila sema Lina roho ya paka.
Bora wamepigwa Ban tu
 
Haya maswala ya majengo watu jawakujipanga kabisa. Nilwahi kuongea kua ujenzi wa hizi nyumba na bei zake unaliweka taifa mtegini hivyo wakuu wa haya mashirika walipaswa kuchunguzwa sana na vyombo vya usalama.
Wamekopa bank ili waweze kujenga matokeo majengo yake mengi hadi hivi sasa yamekosa kabisa watu pamoja na usanii waliouchonga kutuonyesha eti nyumba hizo zinapiganiwa, ukweli ni kuwa bank zitaanza kuipiga mnada hii miradi ili wapate hela yao na hapo ndipo wao kwa kupitia mlango wa nyuma watanunua wenyewe kwa bei halisi ya soko na kuanza kuendesha miradi hii huku shirika likiwa limeshajifia.
Upandw wa mashirika ya hifadhi ya jamii wao ndiyo kabisa watasababisha chaos nchini kwani wametumia hela ya wananchi kutengeneza hizo projects hivyo itakuw ni vurugu kubwa kipindi mashirika hayo yatakapokuwa bankrupt baada ya uwejezeji wao kutotengengeneza faida sababu ya gharama kubwa za pango
 
sasa mkuu ulitaka wajenge mahali ambapo wanajua kabisa hakuna return ya investment ili uje na thread nyingine kuwa jamaa ni wazembe na hawastahili kua hapo kwa kulisababishia hasara shirika kutokana na kufanya miradi isiyokua na tija?
 
Back
Top Bottom