Mipango miji.. Chuo cha mipango Dodoma

mtk eng

Member
Oct 18, 2021
96
223
Ndugu wanajamhuri ya Jf nini litoto langu pale nyumbani. Nililisomesha mipango dodoma akasoma coarse ya urban planing .. sasa najiuliza ataajiliwa kama nani maaana hata sielewi naomben msaada maana naona ajira zinatoka anasema zao bado naona ananichanganya tu mwaka wa 4 huu.. maaana kashaanza kutolea macho urith wa babu yake.

Nawasilisha

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Course mtiti sana hzo yan sio poa ad uwe na connections kama zote aende halmashaur akajtolee kama anajua pia software ndio itapendeza enewei znakuja mchakato wake uko njiani but bado ila kuna mda zltoka sema zilihtaj wa degree
 
Hizo cozi ni kisanga, kwanza hata chuo chenyewe cha mchongo hicho huwa mnawapelekaje nduguzenu hapo?

Coz nyingi pale ni Useless kwa Taifa maana tofauti na kubaki na cheti baada ya kumaliza hakuna mahala utakitumia kwakua vitu vifundishwavyo pale hapa nchini bado havihitajiki ama serikali haina mpango navyo kiufupi viko nje ya mstari, coz nzuri lkn manufaa kwa jamii hakuna labda kwa vikozi vya certificate&diploma, but the rest are useless,
 
Kusema kuwa ni chuo cha mchongo unataka kutuaminisha kuwa wanaohitimu pale hawaajiriwi ?
Kama chuo kinaendelea kupata wanafunzi maana yake kinaaminika
 
Programu nyingi zinazofundishwa Chuo cha Mipango ni janga kwa wahitimu. Wameanzisha programu nyingi za degree ambazo kimsingi hazikutakiwa kutolewa na Chuo cha Mipango. Mfano mzuri Human Resourse Planning and management na hicho cha Urban Planning. Nchi waajiri wengi na Taifa tunajua masuala ya Utawala Chuo chake ni Mzumbe na Urban Planning inatakiwa kutplewa Chuo cha Ardhi. hata mimi ningekuwa mwajiri lazima Mtawala nitamchukua wa Mzumbe na Afisa Mipango Miji nitamchukua wa Chuo cha Ardhi wakati mtaalamu wa Mazingira nitamfuata SUA na Mlimani na Maendeleo ya Jamii nitaenda kumpata Tengeru.

Mipango wanatakiwa kubaki na programu zao za kuandaa Maafisa Mipango kupitia Regional Development Planning, Population Studies and Development na Development Economics. Hao hata huku sokoni na makazini uwezo wao unaonekana na waajiri wana amani na imani.

Nawasilisha maoni yangu Mzee wa Kikushi toka Southern Cushitic.
 
Kama wakiitwa kwenye interview wote wana nafasi sawa inategemea na mtu alivyojipanga kujibu maswali ya interview
 
Tatizo hawaitwi kwa sababu muundo ya taasisi nyingi za Serikali ina kada za wachumi na watakwimu. hazina kada za maafisa Mipango katika miundo yao. hivyo hata katika tanganzo la ajira sifa zinazoainishwa na aina ya watu wanaotakiwa hamna Planning Officers.
 
Mbona hizo kada zipo na watu wanaitwa kwenye interview.
Kwenye kada ya Afisa mipango miji,degree ya Ragional Development Planning inakubali
Maendeleo ya Jamii course ya Project Planning and Management inakubali
Sasa hizo course unazosema wewe hazitambuliki ni zipi ndugu
 
Unajua vizuri Regional Development Planning au umekuja tu huku mbio mbio. Unajua sawa sawa Afisa Mipango Miji ni nani ha graduate wa Regional development Planning aweze kuwa Afisa Mipango Miji?

Usibeze malalamiko ya wadau kwamba graduate wa Mipango wanapata changamoto katika soko la ajira.
 
Labda nikuulize wewe unayeongea bila uthibitisho. Ninaongea kwa kutazama ushahidi
Ingia sasa hivi kwenye mfumo wa ajira (recruitment portal) kisha angalia mtu wa Ragional Planning hana qualification za kuomba hiyo kazi.
Nenda kwenye kada ya Maendeleo ya Jamik angalia mtu aliyesoma Project Planning and Management uone kama hana qualification za kuombe hiyo kazi.
Mimi nimekupa uthibitisho ingia na wewe kisha ndipo urudi uthibitisho wa kuwa ninachosema ni uongo.
 
Mbona hizo kada zipo na watu wanaitwa kwenye interview.
Kwenye kada ya Afisa mipango miji,degree ya Ragional Development Planning inakubali
Maendeleo ya Jamii course ya Project Planning and Management inakubali
Sasa hizo course unazosema wewe hazitambuliki ni zipi ndugu
2.0 AFISA MIPANGO MIJI DARAJA LA II (TOWN PLANNER) – NAFASI 1 2.1 MAJUKUMU YA KAZI i. Kuandaa mipango ya maeneo yaliyoendelezwa kiholela. ii. Kuandaa michoro ya Mipangomiji. iii. Kupokea michoro ya Mipango miji na taarifa za maeneo ya ardhi yanayopendekezwa kuiva kwa ajili ya uendelezaji kimji. iv. Kuchambua takwimu na taarifa kwa ajili ya maandalizi ya mipango mipya ya makazi. v. Kupokea na kuweka kumbukumbu za maombi ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi na umegaji wa viwanja. vi. Kuhakikisha kuwa mabadiliko ya matumizi ya ardhi yanaingizwa katika michoro. 2.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa mwenye Stashahada ya juu/Shahada katika fani ya Mipangomiji kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi au Vyuo Vikuu au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na Serikali.

HIZO HAPO JUU KAZI ZA AFISA MIPANGO MIJI. HIZO KAZI REGIONAL DEVELOPMENT PLANNER SIYO KAZI ZAKE.
 
Mbona hizo kada zipo na watu wanaitwa kwenye interview.
Kwenye kada ya Afisa mipango miji,degree ya Ragional Development Planning inakubali
Maendeleo ya Jamii course ya Project Planning and Management inakubali
Sasa hizo course unazosema wewe hazitambuliki ni zipi ndugu
hizi hapa chini sifa na kazi za AFISA MIPANGO.

POST CATEGORYS BANKING, ECONOMICS AND FINANCIAL SERVICES
HR & ADMINISTRATION
LAND MANAGEMENT
PROJECT, PLANNING AND POLICY MANAGEMENT
EMPLOYER Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
APPLICATION TIMELINE 2021-07-20 2021-08-02
JOB SUMMARY N/A
DUTIES AND RESPONSIBILITIES

MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandaa taarifa ya miradi na mipango ya maendeleo, idadi ya watu,
rasilimali watu, maendeleo ya jamii, mazingira endelevu, program za maliasili
na uwekezaji na fedha;
ii. Kuwasaidia wananchi kuandaa mpango shirikishi wa jamii;
iii. Kubainisha vipaumbele vya ustawi wa maendeleo ya jamii, mazingira

endelevu, program za maliasili na uwekezaji na fedha;

iv. Kuandaa taarifa za tathmini za athari za mazingira zinazotokana na miradi
Enviromental Impact Assessment – eia;
v. Kukusanya taarifa kwa ajili ya uandaaji wa mipango na bajeti;
vi. Kukusanya na kuweka kumbukumbu za idadi ya watu na rasilimali watu; na
vii. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

QUALIFICATION AND EXPERIENCE

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya juu ya Mipango kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali ambao wamejiimarisha Major katika mojawapo ya

fani zifuatazo; Mipango ya Maendeleo ya Mikoa, Mipango ya Menejimenti ya
Mazingira, Mipango ya Maendeleo ya Idadi ya Watu Population and Development
Planning, Mipango ya Uwekezaji na Maendeleo ya Fedha, Mipango ya Menejimenti
ya Rasilimali watu, Menejimenti ya Mazingira na Maendeleo ya Miji, na
Maendeleo ya Uchumi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom