Minyoo, Amoeba na malaria zisizoisha

Jun 28, 2014
16
7
Jamani naombani msaada, nina tatizo la kuugua magonjwa hayo matatu kwa muda wa miaka sita, nikitumia dawa napata nafuu ila baada ya wiki mbili nikipima na kuta bado ipo, hili tatizo linasababishwa na nini? Na dawa gani nitumie ili haya magonjwa yaishe
 
Pole sana! Labda mwambie daktari hili tatizo kama kuna dawa zingine akubadilishie.
Pili chunguza sababu ya wewe kupata hayo magonjwa... Kama ni chakula au maji unayotumia au mazingira unayoishi! Soma jinsi ya kuzuia hayo magonjwa
 
Kinga ni bora kuliko tiba..haya magonjwa mara nyingi usipo tumia mbinu za kujikinga utameza kila aina ya dawa..chunguza ulaji wako..maji unayotumia..matumizi ya kachumbari ambazo hazijaandaliwa katika mazingira ya usafi..kwa malaria utumiaji wa chandarua n.k
 
Jamani naombani msaada, nina tatizo la kuugua magonjwa hayo matatu kwa muda wa miaka sita, nikitumia dawa napata nafuu ila baada ya wiki mbili nikipima na kuta bado ipo, hili tatizo linasababishwa na nini? Na dawa gani nitumie ili haya magonjwa yaishe
kama unataka kumaliza tatizo lako basi fuata ushauri wangu huu
Ugonjwa wa Typhod,Amiba na Minyoo limekua ni tatizo kubwa kwa watu wengi kwa nyakati hizi na hii inatokana na usumbufu ambao watu wanaupata kutokana na hii tiba ya kisasa, sipendi nieleze zaidi kuhusu hilo ila kila mtu anajua amehangaika kiasi gani kutafuta tiba ya Typhod au Amiba mahospitalini bila mafanikio
ila leo nitaelezea jinsi ya kutengeneza dawa ya za magonjwa hayo kama ifuatavyo
MALIMAO
MAANDALIZI
Chukua 1• Majani ya mpera ya kutosha yasiwe chini ya saba
2• Malimao matatu
3• Punje za vitunguu thaumu 21
Vyote hivyo vitwange pamoja ila limao kamua maji yake kisha changanya pamoja
MATUMIZI
Kunywa dawa hiyo yote asubuhi kabla hujala chochote kwa muda wa siku saba.
 
Nakushauri uwe unakunywa week moja katika kila mwezi. Yawezekana mazingira unayoishi kuna mtu ni carriel wa magonjwa hayo.
 
kama unataka kumaliza tatizo lako basi fuata ushauri wangu huu
Ugonjwa wa Typhod,Amiba na Minyoo limekua ni tatizo kubwa kwa watu wengi kwa nyakati hizi na hii inatokana na usumbufu ambao watu wanaupata kutokana na hii tiba ya kisasa, sipendi nieleze zaidi kuhusu hilo ila kila mtu anajua amehangaika kiasi gani kutafuta tiba ya Typhod au Amiba mahospitalini bila mafanikio
ila leo nitaelezea jinsi ya kutengeneza dawa ya za magonjwa hayo kama ifuatavyo
MALIMAO
MAANDALIZI
Chukua 1• Majani ya mpera ya kutosha yasiwe chini ya saba
2• Malimao matatu
3• Punje za vitunguu thaumu 21
Vyote hivyo vitwange pamoja ila limao kamua maji yake kisha changanya pamoja
MATUMIZI
Kunywa dawa hiyo yote asubuhi kabla hujala chochote kwa muda wa siku saba.
Sasa mkuu huwa Unakunywa kijiko au kikombe...?
 
Issue si kunywa dawa au wewe kupima Mara kwa Mara.Kwasababu hayo mgonjwa ni communicable disease yaani mgonjwa ya kuambikizwa.

Sasa unaweza ukawa unapima na kutibu lakini utapata maambikizi mapya au unapata kutoka ulipopata Yale ya zamani..re infection

Unatakiwa ukate njia zote za maambikizi

Pia unatakiwa kutumia dawa zinazotibu.

Unatakiwa kujikinga na MARADHI yote
 
Jamani naombani msaada, nina tatizo la kuugua magonjwa hayo matatu kwa muda wa miaka sita, nikitumia dawa napata nafuu ila baada ya wiki mbili nikipima na kuta bado ipo, hili tatizo linasababishwa na nini? Na dawa gani nitumie ili haya magonjwa yaishe
Nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia ili uweze kupona.
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
Back
Top Bottom