Mindsets (akili) bado ni za zamani, hawajabadilika kifikra na hawa wapo wengi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Kuna hili suala la mindsets (mitazamo), hili lina ukweli mkubwa sana ndani yake. Wapo wengi wenye mawazo ya kuona zinaundwa tume nyingi kwa kutatua matatizo yenye kuweza kutatuliwa leo hii.

Kwenye mindsets kuna suala la watu kulindana, kuoneana aibu, kulalamika wakati mlalamikaji anayo mamlaka ya utatuzi wa tatizo.

Wale waliozoea maisha ya kimwinyi, ya kujiendea tu kizembezembe bila ya kuangalia kama utendaji unaendana na tija inayotegemewa, hawa wana mindsets za zamani.

Huu ni wakati wa kubadilika kimtazamo, kuachana na mawazo ya kirasimu, kuachana na tabia ya kuahirisha utatuzi wa matatizo.

Ni kazi ngumu kuweza kubadilika ndani ya miezi michache lakini mabadiliko ya kimtazamo yanawezekana. Na yakishawezekana naamini taifa zima litapiga hatua za kiuchumi na kisiasa.
 
Back
Top Bottom