Ninavyojua ni makampuni ya simu kama Tigo, Airtel, Voda, TTCL...
Halafu pia kuna makampuni ya minara kama Helios, TTCL na kampuni mpya inaitwa Minara...
Kwa watu binafsi huwa wanakuwa na eneo, hayo makampuni tajwa hapo juu huja kuyakodi na kisimika minara yao, halafu yanamlipa pango mwenye eneo...
Sasa mtu binafsi kumiliki mnara ni hadi pale ambapo kampuni iliyokodi eneo imeshindwa kulipa pango, then kesi ikaenda mahakamani na ikaamuliwa assets za kampuni zipigwe mnada kufidia deni...