Minara ya Halotel yahatarisha usalama wa ndege

Minara ya Halotel yahatarisha usalama wa ndege

Minara ya halotel iliyojengwa sehemu mbali mbali nchini inahatarisha usalama wa ndege. Kwa mujibu wa maofisa wa mamlaka ya anga waliofanya ukaguzi ilibainika minara mingi iliyoko katika mikoa mbali mbali imekiuka vigezo vya usalama wa ndege.

Mfano katika eneo la uwanja wa ndege ulioko Sumbawanga mjini kuna minara miwili, mmoja pembeni mwa uwanja ndani ya mita 50 ma mwingine uko usawa wa njia ya ndege kuruka kiasi kwamba ndege ikichelewa tu kupaa unaugonga huo mnara.

Hali hii iko katika mikoa karibia yote ambapo baadhi ya minara inatakiwa kuondolewa kabisa na mingine ipunguzwe urefu. maofisa wa mamlaka ya usalama wa anga walifanya ukaguzi wao miezi ya April hadi August na kubaini makosa hayo, ambapo waliandika ripoti kwa mamlaka zinazohusika lakini hakuna utekelezaji uliofanyika.

Nafikiri hizi bomoa bomoa zinazoendelea nchi nzima ziguse na eneo hili maana ni hatari sana kwa maisha ya watanzania na wasafiri wote!!

Walikuwa likizo wakati hiyo minara inajengwa! hiyo idara inawatumishi bomu wanaopaswa kutumbuliwa majipu.kwanini wasubiri ujenzi.ukamilike ndio watoke maofisini na kuandika viripoti uchwara! my TZ.always reactive instead of pro active
 
Mshaanza kuwaonea gere kwa Huduma na net nzuri,kwa tz hii kwa sasa hakuna mtandao bora wowote kwa internet zaidi ya Halotel,uko spidi na ni uhakika haikati kama hiyo mengine,tunapoingia porini kikazi mitandao yote inakata na kuandika no service isipokuwa Halotel pekee,hongereni wavietnam.
 
Kudadeki kumbe jamaa wanakamua mb za kufa people kimyakimya? Kesho naenda nunua line ya halotel fasta.

Majungu kazini . Mtandao wa Halotel kwa hivi sasa bila ushabiki wanatisha upande wa network haichagui vijijini na mijini ikija kwenye internet mda wote ni H+ full HD Nipo Daruni Tanga vijijini na enjoy muda wote VIVA HALOTEL wacha waendelee kukupigia majungu watakukubali tu.
 
Halotel hadi mechi nacheki kwenye sim yangu. Hakuna kustack wa scratch, ni mwendo mdundo tu
 
1. Mkuu mita 30 unaijua??? Unajua minara mingi ni 30-50m hii ipo uraiani? Maeneo ya airport mnara hautakiwi kuzidi 10-20m

Sio minala ni minara.....
Ahahahahaa nimecheka sana hapo kwenye mita 30 kama naijuwa. Asante kwa kunirekebisha, uraiani na vijijini huko kuna hado 70 meters
 
Huu Uzi una mwelekeo wa majungu watz tunataka ushindani kwa nini mitandao yote vifurushi vilingane kama sio kuwahujumu wananchi mbona vituo vya Mafuta viko tofauti na bei zimetofautiana

Haloteli ndio habari ya mjini na vijijini.
 
Halotel ameshaanza kuwa tishio hivyo wabaya wake wanaleta fitina! Kwa kasi hii ya internet Voda,tigo na airtel mtasubiri sana. Voda MPESA,Tigo-Tigopesa,Airtel-calls&sms. HALOTEL for internet!
 
Sumry sio mabasi ni bajaji zile???

hakuna sumry ya dar sumbawanga sumry ilikua inaanzia mbeya swanga..na arusha sema jinsi yalivyo mabovu bora upande bajaji kwenda arusha linatumia siku 2..
 
Ahahahahaa nimecheka sana hapo kwenye mita 30 kama naijuwa. Asante kwa kunirekebisha, uraiani na vijijini huko kuna hado 70 meters

Watz kwa ujuaji hamjambo....
70m kwa hapa dar bado sijakutana nayo mkuu.... Kuna mita 70 pale zenji ni hataree ukipanda juu unaona ngoma inaanguka...

Anyway are you involved in this field au unaongea kwa ujuZi tu?
 
Nijuwavyo..
1. Kujenga mnara karibu na airport kuna maximum length ya tower... Nadhani haitakiwi kuzidi mita 30
2. Unaposema kuchelewa kuruka unamaanisha nini..???
3. Kujenga mnara sehemu yoyote unahitajika upate vibari vya
- Mwenye eneo
- Watu wa mazingira (NEMC -
- Kwa eneo la karibu na airport lazima watu wa airport wahusike...

Sasa unaposema hayo sijui mpaka hiyo minala inajengwa wahusika walikuwa wapi

#Faiza Foxy# kuja haraka kuna Mteja wako hapa LOL
 
Kama wamezidisha urefu haina budi kuipunguza, nakumbuka mnara wa tigo pale songwe mbeya upande wa kushoto km unaelekea tunduma ulipunguzwa toka 40m to 15m..... Huwezi jenga jenga tu kiholela na viminara vyenyewe vile vyembamba vya kamba..... Halafu havina taa za usalama aviation light
 
Minara ya halotel iliyojengwa sehemu mbali mbali nchini inahatarisha usalama wa ndege. Kwa mujibu wa maofisa wa mamlaka ya anga waliofanya ukaguzi ilibainika minara mingi iliyoko katika mikoa mbali mbali imekiuka vigezo vya usalama wa ndege.

Mfano katika eneo la uwanja wa ndege ulioko Sumbawanga mjini kuna minara miwili, mmoja pembeni mwa uwanja ndani ya mita 50 ma mwingine uko usawa wa njia ya ndege kuruka kiasi kwamba ndege ikichelewa tu kupaa unaugonga huo mnara.

Hali hii iko katika mikoa karibia yote ambapo baadhi ya minara inatakiwa kuondolewa kabisa na mingine ipunguzwe urefu. maofisa wa mamlaka ya usalama wa anga walifanya ukaguzi wao miezi ya April hadi August na kubaini makosa hayo, ambapo waliandika ripoti kwa mamlaka zinazohusika lakini hakuna utekelezaji uliofanyika.

Nafikiri hizi bomoa bomoa zinazoendelea nchi nzima ziguse na eneo hili maana ni hatari sana kwa maisha ya watanzania na wasafiri wote!!

hayo ni majungu mumeona mumeshikwa pabaya maana hakuna matangazo redioni wala kwenye tv wanajitangaza kwa ubora wao munawaanzishia figisu figisu toa hiyo kitu
 
Majungu kazini...mimi sijali kampuni ni ya nani ninachotaka ni huduma nzuri tu,naona ma monopoly wa sekta ya mitandao ya simu wameanza fitina.
mkuu una akili sana mie mwenyewe nilikuwa najiuliza kweli sio njama za hawa waliounda monopoly power kutaka kuwazorotesha wenzao!? Ila kama ni kweli alichoandika jamaa ngoja tutasikia timuatimua nyingine maana haiwekani mnara ujengwe 50 metre name wahusika wanaangalia afu waanze kusema halotel wamekiuka taratibu
 
Back
Top Bottom