Mwaka huu ulipokuwa unaaza nilimwomba Mungu anipe moyo wa kutenda matendo ya huruma na upendo na nianze na wale wa karibu yangu.
Ukweli kile nilichokiomba ndicho nilichopewa kwa mwaka huu.Nimefanikiwa zaid kutenda matendo ya huruma hata kwa watu wasiokuwa ndugu zangu wa karibu hapa sifa nampa yeye Mungu mwenyewe. katika mambo mengi ya upendo na huruma niliyotenda napenda kuwashuhudia jambo moja ambalo limenikuna zaid.
Kama mjuavyo familia hazina watu wenye uelewa mmoja na pia hazikosi mtu ama watu wenye tabiza zisizovumilika. Kwenye familia yetu tulikuwa na kaka (binamu) huyu ni mtu mzima 36 by age amekuwa ni mhanga wa madawa ya kulevya kwa muda wa miaka 15. alianza kwa kunywa pombe since akiwa sekondari, aka-advance kwenye marijuana na sasa akaingia kwenye heroin. Kwa miaka 7 ambayo amekuwa akitumia heroin + marijuana iliyomfanya awe kama mgonjwa wa kansa hivi, alifika hatua hawez kula kabisa anashinda kwa kula biscuit na jojo, ukimlazimisha kula basi portion yake ni ndogo kuliko mtoto wa mwaka anavyoweza kula.
kwa kuwa na tabia hii hakupenda kukanyika wala kuskia ushauri wa mtu yeyote yule, tulimwogopa kama ukoma, alifikia mahali akaanza kuiba, alijiibia yeye mwenyewe hadi akajifilisi akageukia kwa ndugu yani ukimkaribisha ndani mwako ujue atakuliza alipoona ndugu wana mkwepa akageukia kitaa akawa anaibia watu pochi na hadi kupanga dili zakuiba kwenye nyumba za watu yaani mchora ramani za wizi. kwasababu ya kukosa nguvu nayo hii ikamshinda akageukia kuokota makopo na kuuza na hela zote hizi akipata yeye anampelekea mzungu tuu ili apate kete zake ambazo kwa maeneo anayokaa alikuwa ananunua kwa sh 1500-2000 kwa kete moja. Uvutaji wake ulikuwa ule wa kuvuta kama sigara na sio ule wa kuchoma kwenye kigae ama kujidunga.
mwezi uliopita nilikutana nae akiwa kama chizi, niliogopa sana na nikasema kwakua ni ndugu yangu wa damu lazima nifanye jambo kwaajili yake. Nilimface bila kushirikisha ndugu wengine nikaongea nae juu ya kutaka kumsaidia apate tiba, alikuwa mkali sana sikukata tamaa nikaenda kwa mshauri nasaha nikamwomba aongee nae ili atibiwe apone. Baada ya kubembelezana sana alikubali kutibiwa.
Wapendwa wangu nilianza taratibu za kumtibia hapa Muhimbili,wiki iliyopita siku ya j4 lakin kutokana na kukosa huduma ya kumlaza nikamhamishia kwenye hospitali moja maeneo ya makumbusho. Nilipata changamoto sana manake siku moja tu alokaa pasi kupata madawa yake aliugua kama vile anakufa, aliharisha kama mgonjwa wa kipindupindu vile non stop, akapata homa kali kama vile mgonjwa wa UTI yaani nikaanza kuogopa tena kwamba huenda ukishaanza kuyatumia hutakiwi kuacha. Dr alinishauri nisiogope atapona tuu kwani hii ni zile sumu za yale madawa zinatoka. alipatiwa matiibabu kwa muda wa siku kumi tu na nikaona tofauti ya ajabu kabisa kwake. Yaani binamu yangu huyu amepona ingawa bado kakonda lakini haumwi popote pale na ameoga na kunyoa nywele na ndevu anaonekana ni mtu.Ninamshukuru Mungu sana kwamba amemponya na sasa ni mzima kabisa. Ninayofuraha sana kuona nimethubutu kumtibia na sasa nimeweza kwani amepona kabisa.
Na wewe mwana jf mwenzangu hebu angalia kwenye familia yako kama yuko ndugu ama mtoto mwenye tatizo hili thubutu kumsaidia naamini kama tukifanaikiwa kupunguza idadi ya watumiaji basi ni wazi kwamba hata hao waagizaji nao watakosa pa kuuzia.