Mimi ni wapekee kwenye familia yetu naomba mawazo na uwa nabaguliwa!

Sep 14, 2014
92
31
Amani iwe kuwenu, Nimejiuliza maswali mengi sana juu ya upekee wangu katika familia yetu. Tangu kuzaliwa kwangu na kukua kwangu nimeona mengi sana kwenye familia, Mimi ni mtoto wa kwanza kwa mama yangu kati ya watoto tisa lakini pia mzee wangu (BABA) ameoa wake wanne akiwemo mama yangu kipenzi lakini mimi niko tofauti na watoto wote kwenye familia. Kwenye elimu mimi tu nimfanikiwa kufikia elimu ya juu kwa juhudi zangu mwenyewe, wengine wameishia darasa la 7 ikiwemo na wadogo zangu na wengne hawajui kusoma licha ya kusoma na mimi ndyo mwenye akili tu, pia mimi ni kiongozi wakati kwenye ukoo hakuna hata balozi na mengne nimetofautiana nao. Je kuna jambo lolo kwani mimi nitofauti
 
WEWE MWENYEWE NDO UNAJINYANYAPAA HUJICHANGANYI NAO WAKAHISI UNAJIONA MSOMI mfano wakipika ugali mlenda huli, wakienda shambani kulima wewe unachati huendi unategemea nini? JIREKEBISHE ACHA KUJINYANYAPAA
 
unajibagua mwenyewe kwa kujiona wa pekee, kumbe wa kawaida sana. Mswahili akipata...
 
Mleta mada hiyo elimu unayoona umewazidi hao ndugu zako wengine haijakukomboa kabisa. Huwezi kusema wewe ndo unaakili kuliko wadogo zako wote, hata kama wewe pekeako ndo umepata nafasi ya kwenda shule.

Hata kama wao ni wakulima, wanaakili sana kama binadamu wengine, ondoa hiyo dhana ya kuwadharau kwanza na ujishushe mlingane na uwachukulie na kuwasaidia kama ndugu zako/wadogo zako. Ukiweza kufanya hivyo wote watakuheshimu na hawatakutenga. Kumbuka "ndege wanaofanana huruka pamoja", hivyo ukiwaona wenzako kama "tai" alafu wewe kama "njiwa" basi hao tai wataruka pamoja, nawewe njiwa wakikutana nawe unaliwa tu. Badilika ndugu yangu.
 
Pole sana jombaa. Kama kweli weye ndio mwenye "akiri" kuliko wote kwenye huo ukoo, tafadhali weka hapa jina la huo ukoo tusije jikuta tumeoa au hata kuzaa kwenye huo ukoo kwani mbona balaa?? IQ ya mtoto hutokana na mamake. Sasa ukizaa na mwanamke kutoka ukoo huu si itakuwa balaa??
Unasema kuwa una akili kumbe ni fyatu, sasa tutegemee nini?
Pole kwa hilo tumbo lililokuzaa weye wa kipekee. Natamani ungesema hata kuwa weye ndo wa mwisho kuzaliwa kwenye hilo tumbo lakini ka ndo ulianza na uko vile, baas nyingine mbona ziliharibika??
Siruhusiwi kumchukia aliyezaliwa na mwanamke ila weye, hata Muumba anisamehe. Kumbe bado tuna watu wa jinsi yako wanaodharau hata nduguze wa kuzaliwa? Ukikutana na mimi utasemaje? Ati weye ni kiongozi. Dah! Usijekuwa labda ni balozi wa nyumba kumi ukajiona umemaliza. zaidi ya hapo, JPM hamalizi mwaka huu 2015 kabla hajakutimulia mbali, Pole sana kiongozi mmbaguzi kuliko hata kaburu. Asiyethamini hata kwao, hawezi ongoza hata majuha
 
Back
Top Bottom