Mimi ni Polisi: My Muiseke Nyamughe

hii stor sijui mimi naiita stor tunaingojeeeeeeeeeea weee

Kisa: kilichonitokea


Inamaanisha dadangu wewe hichi kisa cha huyu wifi yako wa kikurya hujakielewa? Niyo sababu ya mimi kuchelewa kumalizia kisa kile cha mke wa waziri...
 
Mimi ni Polisi: “Muiseke wangu Nyamughe


Uliishawahi kukutana na mtu ambaye kuanzia dakika ya kwanza kuongea (hapana, kuonana) ulijiona umeshaoa, umezaa naye watoto na kwa mbali mpo na wajukuu wenu wanacheza cheza wakiwazunguka?

20th December 2013, Ijumaa..Stendi ya mabasi Ubungo

Nilikuwa nimeomba likizo ya dharura kutoka kituo changu cha kazi mkoa wa kipolisi Ilala nikidhamiria kufunga safari kwenda Moshi kusherehekea sikukuu za Christmas pamoja na wazazi wangu kule kijijini Old Moshi. Ni muda mrefu tangu nimalize likizo yangu ya kwanza miaka mitatu iliyopita na sikuwa nimewaona. Kwa bahati nzuri mkuu wangu wa kazi kituoni Salendar Bridge alikuwa akinipenda sana. Sijisifii ila naamini utendaji wangu wa kazi ulinitangulia na kurahisisha mimi kupewa ruhusa kirahisi ukichukulia jinsi ambavyo kuhitajika kwa nguvu kazi kulivyo kukubwa hasa zifikapo siku za sikukuu.

Niliomba ruhusa ya siku saba tu hasa nikiwa na lengo la kwenda kumjulia hali mama yangu kwani niliambiwa hali yake haikuwa njema sana. Ndiyo, hakuwa amelazwa ila kwa kiasi nilitamani kumuona kwani ni miaka miwili na miezi kadhaa hatujaonana tangu nilipokwenda Moshi kwa likizo yangu kubwa ya mwaka 2011.

Nilishuka kwenye daladala pale Ubungo na kibegi changu cha mgongoni kuelekea kwenye geti la kuingilia penye mabasi ya kwenda mikoani.

Alikuwa na umbo la kawaida tu kwa nyuma ila lilitosha kunivutia na kunipa morali kama nipandaye kilima cha ‘Mr Price’ wakati wa mchakamchaka wa asubuhi na kunifanya niongeze mwendo ili kuweza kumfikia. Kwa kuwa nilikuwa na kabegi kamoja tu haikuwa kazi ngumu ukiongezea na yeye kuwa na begi fulani zito, nilimfikia na kumwangalia usoni.

Nisikilize kwa makini; pata picha ya ngozi ya Jacquile Ntuyabaliwe, laini, maji ya kunde, yenye mng’ao, sura nyembamba ndefu, pua ndogo ilichongoka vyema katikati ya macho yaliyolegea, meupee maangavu yakitiwa doa leusi linalong’aa katikati. Ndiyo, mrefu mwembamba kiasi lakini mwenye umbo ambalo kamwe hutochoka kumwangalia. Kwa haraka nilijiaminisha huyu kama si Mnyarwanda basi ni hawa ndugu zetu wa kutoka Ngara aliyechanganyia labda na damu ya mama wa Kihaya.

“Hey, mambo” Nilimsalimia

Akatabasamu, “Poa”

Nilimwambia aniachie begi nimsaidie kwani niliona lilivyokuwa likimpa shida na nilijua lingempa shida kupita nalo kwenye vile vigeti vya orange vya kuingilia Ubungo. Alikubali nikampa kibegi changu akabeba na mimi nikachukua la kwake na kumwambia tupitie geti kubwa (hili linalotumiwa na magari). Nilijua kufanya vile ni kuvunja amri ila mtanisamehe, mbele ya mrembo kama yule, “If love is a crime …”

Nilimsindikiza hadi ndani na alikuwa akielekea Morogoro. Nilimsaidia kupata basi na kwa bei nzuri kwani kipindi hiki cha sikukuu wao huamua nauli wanayotaka.

“Wow, it’s like you are my angel today. Thanks!” alinitamkia kwa tabasamu lileee. Baada ya kuhakikisha amepata basi na kujua muda wa kuondoka (ambao haikuwa hadi nusu saa baadaye) niliondoka na mimi kwenda kutafuta basi la kunipeleka mamndenyi kwetu.
Ni wakati naelekea zilipokuwa ofisi za Scandinavia Express kwa ajili ya kupunguza mafuta (haya mabasi yaliendaga wapi vile???) nilipomuona tena. Nilipomuona mara ya kwanza nilijitahidi (kwa kweli) kuwa ‘a good guy’yani kutoa msaada tu na si zaidi. Ila sasa mara hii ya pili nilisema ‘Liwalo na liwe…!’

Nilimfuata kwa nyuma na kumgusa bega (alikuwa ameenda kununua biskuti). Aligeuka na kutabasamu. Aaargh! Hakuwa akijua kila akitabasamu anaharibu mpangilio mzima wa mawazo kichwani mwangu. Nilijikuta nimesahau mistari yote niliyopanga. Kwa kweli sikumbuki nilichokisema ila tulijikuta tukipiga stori hadi wakati basi lake lilipopiga honi kuashiria kuanza kwa safari yao.

“Hey naitwa Aden by the way”, nilijitambulisha.

Siku nyingine…

“Amayana Mura!” Ilikuwa SMS kutoka kwa Nyamughe akinijulia hali ya asubuhi kama ambavyo amekuwa akifanya tangu nianze kujifunza Kikurya.


Nyamughe

Ni yule binti niliyekutana naye stendi ya mabasi Ubungo. Alikuwa akielekea Morogoro na kisha nyumbani Tarime wilayani Rorya kijiji cha Utegi. Sikuamini siku aliyoniambia yeye ni Mkurya. Nilikuwa nimekremu kuwa wao huwa kama picha Fulani hivi niliyozoea kuiona ikisambaa kwenye mitandao ya bibi aliyeko kwenye kikao akiwa na panga pajani. Nakumbuka siku ananiambia yeye ni Mkurya nilimtania kwa kumwambia, “Hapana aisee! Lazima tumuulize mama yako vyema”

Nyamughe alikuwa amemaliza shahada ya kwanza ya sheria Chuo Kikuu cha Dar es salaam almaarufu Mlimani na alikuwa akienda nyumbani kwao kuwasalimu wazazi kabla ya kurejea jijini Dar kujiandaa na masomo ya ‘School of Law’.

Tuliongea mengi sana kwenye simu na hata baada ya kurudi Dar es salaam, hakuonesha mabadiliko yeyote. Hapa ndipo natakiwa kusema, nilianza kuwaona wajukuu zetu wakicheza pembeni yetu.

On our first serious date, oops! Nyamughe ananifanya afande niandike Kiingereza kingine sijawahi kukiandika. Anyway, Siku yetu ya kwanza kushinda pamoja ilikuwa kama ‘a day spent in Heaven’..pure and fun! Ni vigumu kuielezea kwa maneno…

Nyamughe alikuwa mwanamke wa ndoto zangu. Tulifahamiana kwa muda mfupi tu lakini ilikuwa rahisi kujua huyu ndiye. Mara nyingi mtu unakuwa umejiwekea vigezo vya mwanamke unayemtaka na unakuwa na vile vya msingi na vya nyongeza. Nyamughe alikuwa navyo vyote. Hadi vile unavyoweza kuviita vya kitoto.

Ngoja, mfano kidogo. Pamoja na uafande wangu, hakuna somo nililokuwa nalipenda shuleni kama Hisabati. Nifaulu au nifeli nilikuwa nimejiwekea akilini kuwa sitoungana na wale wanaosema 'Hisabati ni ugonjwa wa taifa' asilani. Na ndoto yangu ilikuwa kumpata binti ambaye, si kwamba awe alipata 'A' kwenye somo hilo, lakini ambaye alilithamini kama somo mama kwenye maisha ya mwanadamu. Nisingependa kuona mama anayewaambia watoto, “Mh! Mmefeli Hesabu, wala msijali wanangu..huo ugonjwa wa taifa.”

Nyamughe alinifanya niote. Nyamughe alinifanya nione sikuchelewa bure. Wengi wa wale tuliomaliza nao depo mwaka ule wa 2008 walikuwa wameshaoa ama wana watoto tayari. Kwa ratiba ya kiaskari nilikuwa nimechelewa.

Mwezi wa nane mwaka huu nilitakiwa tena kuchukua likizo yangu kubwa ya miezi mitatu kwani tayari nilikuwa nimemaliza miaka mitatu tangu likizo yangu ya kwanza kuisha. Akili yangu iikuwa imeshapanga kuwa nitamweleza Nyamughe nia yangu ya kumfanya mke wangu kwani mara nyingi nilikuwa nikimweleza kama utani anaishia kucheka. Nilitaka nitakapoenda nyumbani tena, nimpeleke akawaone wazazi wangu na kupaona nilipozaliwa na kukua. Aje tu kama rafiki kwanza.

Ilinibidi kuanza kumchombeza Nyamughe mapema kujua utayari wake. Aliniambia hana uhakika na ratiba yake lakini ataangalia nami nikamtania kuwa hata ikibidi kuumwa lakini twende Moshi.

07 May 2014

Nilimpigia simu kumjulia hali Nyamughe wangu lakini haikuwa ikipokelewa. Nilijipa moyo kuwa labda ni ubize wa shule na baadaye tutaongea. Jioni Nyamughe alipokea simu na kunijulisha kuwa amechoka sana angeomba tuongee siku itakayofuata. Nilikata simu na kulala nikiamini Nyamughe wangu amechoka ila walau ni mzima.

9th May 2014, Ijumaa, 1535hrs

“Girl you know I care
So, if you ever seem to lose your way
Don’t have no fear Hold my hand
I’ll be there girl you know I care girl…
”

Ilikuwa ringtone ya simu yangu (you can’t blame me, afande is in love). Na hakuwa mwingine bali Nyamughe. Nilikata simu na kumpigia kujua anataka kuniambia nini Nyamughe wangu Ijumaa hii. Moyoni nilikuwa nawaza something nice kama kukutana pale KFC mpya karibu na IFM au kwenda movie Dar es salaam Free market.

“Hello Aden”

“Hey Nyamughe, niambie mamii”

“Am good, ” akandelea, “I want to tell you something Aden”

Mh! Akili yangu ikawaza kwa haraka kuwa huwa hakuna jambo zuri linalotokana na sentensi hiyo. Nilijikaza kumsikiliza.

“Sitoweza kwenda na wewe Moshi”

Nilitamani kumuuliza kwa nini. Nilitaka aendelee lakini ghafla simu ikakatika. Kuangalia kumbe ni muda wa maongezi umeisha. Nilijaribu kununua kifurushi kupitia Airtel Money lakini nikawa najibiwa, “Muhamala wako haukukamilika TXN Id: MP1405**.****.A*****. Service is Busy.Please try again later”

Nilijaribu pia kwa CRDB lakini ilikuwa kama gundu nilishindwa kununua kifurushi kabisa na nilitakiwa kurudi kwenye dawati kuendelea na kumsikiliza mteja aliyekuwa amewasili muda ule. Nilijiambia nitampigia simu baadaye kujua sababu ya Nyamughe kukataa kwenda Moshi na mimi. Nilikuwa nimeanza kumuandikia ujumbe mfupi wa kutaka kumweleza hali iliyojitokeza na nia yangu ya kumpigia simu baadaye.

Sikuhutaji kusubiri hadi jioni kwani Nyamughe aliamua kuiridhisha hamu yangu ya kutaka kujua kwa kunitumia ujumbe ambao ulinifanya nishindwe kuandika tena maelezo ya mteja yule. Kifupi nimekuwa katika hali ya ganzi tangu Ijumaa ile.

13 May 2014

Nipo nyumbani leo baada ya kutoka zamu usiku. Kidogo baada ya kusikia matatizo ya wateja waliokuja kituoni nimejifariji na kujiona langu si tatizo. Katika kupitia pitia simu yangu ndipo nimekutana na mawasiliano yangu ya mwisho na Nyamughe. Alikuwa ameniandikia;

“Am sorry Aden, but am seeing someone else, and I love him.”

Nami katika hali ile ya kuchanganyikiwa nilijikuta kumbe nilikuwa nimeituma meseji ile niliyokuwa nimeanza kuiandika bila hata kuimalizia, “Muiseke wangu Nyamughe…”


Wasalaam wapendwa,
Mentor.


Duh,hali kama hii huwa inatokea ila kwa case hiyo hadi nimekuonea huruma jembe,jipe moyo mkuu...
 
Nimebaini uongo mwingi sana.miaka ya kuanza kazi imetofautiana katika stori zako mbili. Labda kama ni stori ya kutunga lakini kama ni kisa halisi mentor acha kudanganya watu. Vinginevyo uko fresh katika kupangilia hadithi. Unaonaje ujiajili kwa kuandika hadithi katika magazeti hasa ya udaku??? Utajipatia kipato cha ziada.
 
Nimebaini uongo mwingi sana.miaka ya kuanza kazi imetofautiana katika stori zako mbili. Labda kama ni stori ya kutunga lakini kama ni kisa halisi mentor acha kudanganya watu. Vinginevyo uko fresh katika kupangilia hadithi. Unaonaje ujiajili kwa kuandika hadithi katika magazeti hasa ya udaku??? Utajipatia kipato cha ziada.

Ulitaka niandike kila kitu ili mnijue??!
 
kwa hayo machache ya ukweli mbona mimi tayari nimekufahamu au kwa lugha nyingine nimekusoma kwa nguvu ya ....mentoooor
 
Back
Top Bottom