Mimi ni muathirika wa UKIMWI

Mimi ni muathirika wa UKIMWI

Protein

Member
Joined
Apr 18, 2019
Posts
53
Reaction score
194
Mimi ni member mkongwe humu. Ninaishi Sweden na nina passport kwa sasa.

Nilikutana na kijana Mtanzania aliyekuwa na viza ya uanafunzi 2007 kumbe alikuwa muathirika. Nilimkaribisha nyumbani kwa chakula bila kufahamu lengo lake.

Kawakuwa nilikuwa mpweke sana alijenga mazoea ya kuja kwangu hasa weekends.

Alionyesha dalili zote za mapenzi, nilimuambia tukapime kwanza. Siku moja alijiforce kwangu na ukawa mwanzo wa mapenzi bila kupima.

Yule kijana alirudi Tanzania, niliendelea na maisha. Nilimsahau kabisa. Mwaka 2017 nilipata kazi wizara ya afya Sweden, occupation health walinipa form ya kujaza. Nilikwenda kwa daktari na kumwambia sitajali kama atatick box zote. Aliniuliza una uhakika unataka kupima HIV? Nikasema ndiyo.

Alinipa karatasi niende nayo lab. Baada ya wiki moja nilipigiwa simu nirudie vipimo. Sikuwa na wasiwasi. Baada ya wiki nilirudi kwa daktari. Aliniambia Protein una HIV. Nilidhami anaongelea mtu mwingine.

Alianza kunieleza kuwa matibabu sikuhizi yameboreshwa sana. Nenda kwenye kitengo.

Nimefika kwenye kitengo walikuwa wanafunga kwa chakula cha mchana. Ilibidi niende nyumbani. Nilisali sana kuomba huruma ya Mungu.

Saa nane nilirudi kwenye kitengo. Walichukua vipimo upya. Majibu kutoka HIV+. Nilipewa nurse alinipa counselling kuanzia saa tisa mchana mpaka 11:00 wakati wanafunga ofisi. Safari yangu kama muathirika ilianzia hapo.

Nyumbani kwetu hawafahamu zaidi ya kaka yangu ambae aliumia sana. Alisema tulikupeleka Ulaya upate maisha bora leo hii unapata HIV Ulaya?

Haya ndiyo maisha yangu mapya kama muathirika.

Baada ya maambukizi nilikaa miaka 10 bila kujijua. Nilikuja kumjua aliyeniambukiza baada ya kupata list ya wa Tanzania aliowaambukiza. Kuna uwezekano niliwaambukiza watu wawili au watatu kwani nilikuwa single nikijaribu bahati ya relationship.
 
Una uhakika gani ulikaa nao miaka 10 bila kujua? Una uhakika gani yeye ndiyo kakuambukiza?
Je unajua siyo lazima ufanye mapenzi na mwathirika na wewe uambukizwe?
Ninachosema ni kwamba unaweza kusema tuu kwamba yeye ndiyo kakuambukiza kama tuu ndani ya hiyo miaka 10 haukuzini na mwanamke/mwanaume mwingine.
Btw kuwa na UKIMWI siyo mwisho, jitunze kuna magonjwa hatari zaidi ya huo na yanaambukizwa kwa zinaa pia.
 
Una uhakika gani ulikaa nao miaka 10 bila kujua? Una uhakika gani yeye ndiyo kakuambukiza?
Je unajua siyo lazima ufanye mapenzi na mwathirika na wewe uambukizwe?
Ninachosema ni kwamba unaweza kusema tuu kwamba yeye ndiyo kakuambukiza kama tuu ndani ya hiyo miaka 10 haukuzini na mwanamke mwingine.
Btw kuwa na UKIMWI siyo mwisho, jitunze kuna magonjwa hatari zaidi ya huo na yanaambukizwa kwa zinaa pia.
Maelezo yake ni kama mwanamke.
 
Mimi ni dada, hawa watu niliyokutana nao baada ya kuacha a na jamaa walipima kabla lakini mimi nilijihakikishia sina maambukizi.

Huyu kijana aliambukiza watu wengi hata baada ya Mimi. Alifika Tanzania na kuoa kanisani mke aliambukizwa
 
Watu wana underestimate spread ya ukimwi, yaani ukifanya mapenzi bila kinga ukabahatika shukuru sana, watu wengi they simply don't care wakidhani waathirika ni wachache, waathirika ni wengi zaidi ya watu wanavyofikiria, waliopima ni wachache.
 
Yaa kwa kujiamini kuwa niko Ulaya nilihakikisha wanapima kwanza. Ninakumbuka nilipima 2005 nikawa mzima. Basi kila aliyeniuliza nilisema ninepins.

Kuna siku nikiwa kwenye shrehe watu walimuongelea Zabron slivyoumwaga Ukimwi Stockholm ndipo masikio yalinifunguka.
Duuh, pole. Songa mbele usikate tamaa.
 
Watu wana underestimate spread ya ukimwi, yaani ukifanya mapenzi bila kinga ukabahatika shukuru sana, watu wengi they simply don't care wakidhani waathirika ni wachache, waathirika ni wengi zaidi ya watu wanavyofikiria, waliopima ni wachache.
Ni kweli kabisa mkuu. Baada ya leo Protein anaondoka leo ameamua kufunguka
 
Back
Top Bottom